Kingsharon92
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 7,843
- 10,321
Hivi huyu ISRAEL mtoa roho mnayemzungumzia yukoje ameainishwa kwenye maandiko msaada tafadhali
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo ni kiumbe wa Allah, kiumbe atakeyekuwa wa mwisho kufa. Kiumbe mwenye kuzitoa roho za waja kwa idhini alopewa na Allah.
Maelezo mengi alafu yote pumu
Hamna cha maana ulichoandika
wasomi na wachambuzi wa mambo hatuendi hivyo ukiona hakuna cha maana unatoa hoja ndugu Mohamedy ee bwana waislamu wanasema 'usipo jua jambo uliza'
Habari zenu wana JF,
Kuna kitu nimekiwaza na kukitafakari kwa muda wa kama siku 3 hivi lakini bado sijapata majibu yake. ...
Suala kubwa linalonitatiza ni kuhusu ukweli wa siku ya kiama, jehanamu na pepo. Je kweli hivi vitu vipo kweli? Nikiri wazi kabisa kwamba mimi ni mkristo mkatoliki na nimekua nikifundishwa haya kama sio kukaririshwa toka nikiwa mdogo katika mafundisho ya komunio ya kwanza na kipaimara kwamba kuna hivyo vitu 3 nilivyovitaja.
Yafuatayo ni maswali ambayo najiuliza na ningefurah kama nitapata majibu ya kina na kuridhisha.
1. Je ni kweli kuna siku ya kiama?....
Shukrani.
asante kwa msaada wako"Usipojua jambo uliza" sawa kabisa. Lakini usihadaiwe na hilo jina la Mohamedy ukadhani ni mwislam, hapana. Huyo hana chembe ya uislam, waislam hawako hivyo na majibu yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
kaka hakuna andiko hapo kuna maelezo tupitia hapo juu mkuu nimeweka kwenye bandiko langu yakutosha kabisa
"Usipojua jambo uliza" sawa kabisa. Lakini usihadaiwe na hilo jina la Mohamedy ukadhani ni mwislam, hapana. Huyo hana chembe ya uislam, waislam hawako hivyo na majibu yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
Huyo ni kiumbe wa Allah, kiumbe atakeyekuwa wa mwisho kufa. Kiumbe mwenye kuzitoa roho za waja kwa idhini alopewa na Allah.
Yuko wapi?Ndugu kama unaamini kuwa Mungu yupo, wasiwas wako nini?
Kwa nini Mungu atunyooshe Wakati we unadai ndio katuumba? Why atudhuru?hukumu(kiama) ya mwanadamu inaanza mara tu baada ya mtu kufa. aliyetubu dhambi na kupatana na Mungu atapelekwa Mbinguni na asiyetubu ataenda motoni. wale wa zamani walioangamizwa sio kwamba ni waovu zaidi yetu bali ni matashi ya Mungu kuchagua njia ya kutunyoosha viumbe wake. ulichofundishwa ktk imani yako ni kweli kabisa, kishike. tenda mema acha mabaya. penda kutubu kila unapomkosea Mungu.
Kwanza ukiyasoma hayo mavitabu yamejaa uongo mwingi, na yanapingana sana. We kama tunaambiwa eti ukizaliwa tu, basi Mungu anajua hatima yako eti kama utaenda motoni au mbinguni, sasa kama anajua tutakakoangukia, kwa nini tuswali, na kwa nini tumuombe na kumlazimisha atupeleke ambako yeye hakutupangia?Haya mambo ya kiroho kwa kiasi kikubwa yana utata sana. Tunaambiwa mtu yaani nafsi anapatikana kutokana na muunganiko wa mwili na roho (pumzi ya uhai) na kwamba mtu huyo anapokufa mwili uoza lakini roho ubaki ikisubiri siku ya kiama. Sasa swali ni kwamba kama kiama kinaanza muda au siku ile mtu anapokufa iweje adhabu iwe ni kwa roho tu na siyo kwa mwili pia wakati kipindi cha kutenda dhambi vilikuwa pamoja?
Na kama mateso yanaanza mara moja baada ya mtu kufa basi ni dhahiri kwamba wale wenzetu waliofariki karne nyingi zilizopita hadi siku ya kiama itakapofika watakuwa wamepata mateso makubwa zaidi (ya muda mrefu) kuliko wale watakao wamekufa miaka michache (mfano mwaka mmoja, miwili kumi n.k.) kabla ya hiyo siku ya kiama. Na kama wakianza kutumikia adhabu zao baada ya kiama hao waliokufa na kupata mateso karne nyingi zilizopita kuliko wengine watapunguziwa adhabu au la?!
Kingine mtu anazaliwa na kudumu duniani kwa dakika, masaa, siku au miaka michache tu lakini siku ya kiama anakuja kutumikia adhabu jehanamu milele! Daah...mimi hata sielewi bana.
Nani kakuambia?Kwakuwa umeuliza kwa imani zote nami nisemi kidogo. Katika uisilam kiama ni siku ngumu kuliko ugumu wowote ambao mwanadamu anaweza waza. Ni siku ya hukumu. Kabla ya kusimama kiama ni wazi kuwa viumbe wote watakafu(wakiwemo maaika wote mpaka mtoa roho-Izraeli).
Kisha watu watafufuliwa kutoka katika matumbo ya ardhi wakiwa katika hali tofauti tofauti.kulingana na matendo yao. Hata hivyo bado siku hiyo itakuwa ngumu sana isipokuwa tu kwa wale waliridhiwa na mola wao.
Hapo ndipo watu watahukumiwa kwa matendo yao. Kuna mchakato mrefu.sana siku hiyo. Hakuna kujuana hapo baba hatamjua mwana wala mwana hatamjua mama. Kila mtu nafsi yake itakuwa imeshughulishwa na mambo yake. Kisha watu watahukumiwa kwa kuulizwa juu ya.yale waloyatenda. Na pindi watakapo danganya,itafungwa midomo yao kisha kila kiungo kipekee kitatoa ushahidi wa kila ulichokifanya.
Kwa wale wanodhani ukifa ndio kiama chako,hakika hawapo sahihi hata.kidogo. Kufa ni katika kitendo cha kufika.mwisho.wa dumia.na mwanzo wa akhera. Kaburi watu watu wataanza kukutana na kheri zao ama shari zao kulingana na matendo yao. Hapo ni adhabu kwa makosa hadi itakapo fika kiama. Na adhanu hii haipunguzi.adhabu atakayoipata mwanadamu siku ya kiama baada ya kuhukumiwa.
Hakika kiama ni siku nzito na tunamuomba Molla wetu atufishe.ili hali yu radhi na sisi ili tuweze kuongoka adhabu zake. Amin.