Naomba kujua ukweli kuhusu 'kiama'

Naomba kujua ukweli kuhusu 'kiama'

Hivi huyu ISRAEL mtoa roho mnayemzungumzia yukoje ameainishwa kwenye maandiko msaada tafadhali
 
Huyo ni kiumbe wa Allah, kiumbe atakeyekuwa wa mwisho kufa. Kiumbe mwenye kuzitoa roho za waja kwa idhini alopewa na Allah.

Kwa mawazo haya sisi waafrika tutabaki nyuma kila siku!

Karibu katika ulimwengu huru!

..........Free ideas....
 
wasomi na wachambuzi wa mambo hatuendi hivyo ukiona hakuna cha maana unatoa hoja ndugu Mohamedy ee bwana waislamu wanasema 'usipo jua jambo uliza'

"Usipojua jambo uliza" sawa kabisa. Lakini usihadaiwe na hilo jina la Mohamedy ukadhani ni mwislam, hapana. Huyo hana chembe ya uislam, waislam hawako hivyo na majibu yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
 
Ndugu k_dizle
acha nikupe huu mukhtasari hivi:-

Dunia ni siku tatu.. (jana,leo,kesho)
1. Jana tumeikidhi na kuishi hivyo hatorudi tena !!
2. Leo tunaishi na kuitenda lakini haitodumu tena !!
3. kesho hatutojuwa wapi tutakuwepo au kijacho tena !!

Sasa kiri kuwa Mwenyeezi Mungu ni mmoja na miliki wa vyote....

Good Luck
 
Habari zenu wana JF,

Kuna kitu nimekiwaza na kukitafakari kwa muda wa kama siku 3 hivi lakini bado sijapata majibu yake. ...

Suala kubwa linalonitatiza ni kuhusu ukweli wa siku ya kiama, jehanamu na pepo. Je kweli hivi vitu vipo kweli? Nikiri wazi kabisa kwamba mimi ni mkristo mkatoliki na nimekua nikifundishwa haya kama sio kukaririshwa toka nikiwa mdogo katika mafundisho ya komunio ya kwanza na kipaimara kwamba kuna hivyo vitu 3 nilivyovitaja.

Yafuatayo ni maswali ambayo najiuliza na ningefurah kama nitapata majibu ya kina na kuridhisha.
1. Je ni kweli kuna siku ya kiama?....
Shukrani.

Link 1 Matthew 24:36 "But about that day or hour no one knows, not even the angels in heaven, nor the Son, but only the Father.

Link2. https://www.islam-guide.com/ch3-5.htm

Link3. Part 3: Some Signs of Day of Resurrection



Link4. The Noble Quran - القرآن الكريم

Link5. The Noble Quran - القرآن الكريم

Link6. The Noble Quran - القرآن الكريم

Link7. The Noble Quran - القرآن الكريم

 
Siku ya kufufuliwa tutatoka ktk tumbo la ardhi na kuulizana ardhi hii leo ina nini?!na kila atakaejiuliza amekaa mda gn kaburini jibu lake ni siku moja au ktk shm ya siku tu!km umelala then ukaamka.
Izrail mtoa roho kabla ya kiama atatumwa atoe roho viumbe wote waliobaki akimaliza atamuuliza mungu nimeshamaliza mungu atamjibu bado jamaa atarudi atazunguka kote hadi kw malaika atakuta wamekufa kisha atamrudia mungu kumueleza kwmb hamna kilichobaki.
Hapo mungu atamjibu ni ww pekee ndo umebaki jitoe roho unikabidhi ataitoa huku akilia kwa uchungu.
Baada ya hapo huku duniani itanyesha mvua ya shahawa na watu wataanza kufufuka na kujiuliza kuna nini tena tunaamshwa usungizi ulikuwa mtamu?!
Hapo ndo mungu muumba atasimama na kusema leo ndo siku ya haki hakuna atakaeonewa isipokuwa kwa aliyoyatenda.hii siku haina shaka ndugu zangu sbb huku duniani hakuna haki mkubwa anaonea mdogo tajir anatesa maskini
 
"Usipojua jambo uliza" sawa kabisa. Lakini usihadaiwe na hilo jina la Mohamedy ukadhani ni mwislam, hapana. Huyo hana chembe ya uislam, waislam hawako hivyo na majibu yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
asante kwa msaada wako
 
"Usipojua jambo uliza" sawa kabisa. Lakini usihadaiwe na hilo jina la Mohamedy ukadhani ni mwislam, hapana. Huyo hana chembe ya uislam, waislam hawako hivyo na majibu yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

Kwahyo ww ni muislam?
 
Hakuna kitu kama hicho. Mambo ya kijinga sana kuamini sijui kiama, moto, sijui peponi ni ujinga tu. Kifupi mambo ya Dini ni ya kufikirika tu ili kukutisha uwe mtumwa wa imani, na ukizidisha maimani ya hizo riwaya zilizoletwa kwenye majahazi, unaishia kuua watu bure na kuwa hata gaidi kwa kudhani unafanya kazi ya Mungu kumbe umesharukwa akili. We ishi kwa amani, usiue, usidhulumu, na machafu achana nayo utaishi vizuri basi.
 
hukumu(kiama) ya mwanadamu inaanza mara tu baada ya mtu kufa. aliyetubu dhambi na kupatana na Mungu atapelekwa Mbinguni na asiyetubu ataenda motoni. wale wa zamani walioangamizwa sio kwamba ni waovu zaidi yetu bali ni matashi ya Mungu kuchagua njia ya kutunyoosha viumbe wake. ulichofundishwa ktk imani yako ni kweli kabisa, kishike. tenda mema acha mabaya. penda kutubu kila unapomkosea Mungu.
Kwa nini Mungu atunyooshe Wakati we unadai ndio katuumba? Why atudhuru?
 
Haya mambo ya kiroho kwa kiasi kikubwa yana utata sana. Tunaambiwa mtu yaani nafsi anapatikana kutokana na muunganiko wa mwili na roho (pumzi ya uhai) na kwamba mtu huyo anapokufa mwili uoza lakini roho ubaki ikisubiri siku ya kiama. Sasa swali ni kwamba kama kiama kinaanza muda au siku ile mtu anapokufa iweje adhabu iwe ni kwa roho tu na siyo kwa mwili pia wakati kipindi cha kutenda dhambi vilikuwa pamoja?

Na kama mateso yanaanza mara moja baada ya mtu kufa basi ni dhahiri kwamba wale wenzetu waliofariki karne nyingi zilizopita hadi siku ya kiama itakapofika watakuwa wamepata mateso makubwa zaidi (ya muda mrefu) kuliko wale watakao wamekufa miaka michache (mfano mwaka mmoja, miwili kumi n.k.) kabla ya hiyo siku ya kiama. Na kama wakianza kutumikia adhabu zao baada ya kiama hao waliokufa na kupata mateso karne nyingi zilizopita kuliko wengine watapunguziwa adhabu au la?!

Kingine mtu anazaliwa na kudumu duniani kwa dakika, masaa, siku au miaka michache tu lakini siku ya kiama anakuja kutumikia adhabu jehanamu milele! Daah...mimi hata sielewi bana.
Kwanza ukiyasoma hayo mavitabu yamejaa uongo mwingi, na yanapingana sana. We kama tunaambiwa eti ukizaliwa tu, basi Mungu anajua hatima yako eti kama utaenda motoni au mbinguni, sasa kama anajua tutakakoangukia, kwa nini tuswali, na kwa nini tumuombe na kumlazimisha atupeleke ambako yeye hakutupangia?
 
Kwakuwa umeuliza kwa imani zote nami nisemi kidogo. Katika uisilam kiama ni siku ngumu kuliko ugumu wowote ambao mwanadamu anaweza waza. Ni siku ya hukumu. Kabla ya kusimama kiama ni wazi kuwa viumbe wote watakafu(wakiwemo maaika wote mpaka mtoa roho-Izraeli).
Kisha watu watafufuliwa kutoka katika matumbo ya ardhi wakiwa katika hali tofauti tofauti.kulingana na matendo yao. Hata hivyo bado siku hiyo itakuwa ngumu sana isipokuwa tu kwa wale waliridhiwa na mola wao.
Hapo ndipo watu watahukumiwa kwa matendo yao. Kuna mchakato mrefu.sana siku hiyo. Hakuna kujuana hapo baba hatamjua mwana wala mwana hatamjua mama. Kila mtu nafsi yake itakuwa imeshughulishwa na mambo yake. Kisha watu watahukumiwa kwa kuulizwa juu ya.yale waloyatenda. Na pindi watakapo danganya,itafungwa midomo yao kisha kila kiungo kipekee kitatoa ushahidi wa kila ulichokifanya.
Kwa wale wanodhani ukifa ndio kiama chako,hakika hawapo sahihi hata.kidogo. Kufa ni katika kitendo cha kufika.mwisho.wa dumia.na mwanzo wa akhera. Kaburi watu watu wataanza kukutana na kheri zao ama shari zao kulingana na matendo yao. Hapo ni adhabu kwa makosa hadi itakapo fika kiama. Na adhanu hii haipunguzi.adhabu atakayoipata mwanadamu siku ya kiama baada ya kuhukumiwa.
Hakika kiama ni siku nzito na tunamuomba Molla wetu atufishe.ili hali yu radhi na sisi ili tuweze kuongoka adhabu zake. Amin.
Nani kakuambia?
 
Mwisho wa Dunia siku ukifa wewe tu.. wengine wanaendelea Dunia hii ina miaka trillion na bado ipo sana tu
 
Back
Top Bottom