Kumbe wengi walikuwa nayo hii album aisee home nilikuwa dogo basi kila leo inapigwa hii album mbaka waislam wengi sana waliipenda kuna wimbo ulikuwa unaitwa ima nikuwa nayo hakikaa kwa mambo yatarajiwayo... Niliipenda sana kwakweli nilikuwa dogooOoh no, hope sahiv watakuwa wazee jamani
ππ, niliwapenda sana, na nyimbo zao ni bomba mbaya
"Kazi nzuri sana ya muda wote. Mungu awajaalie huko waliko"
Wasalimie mkuu, waambie Bushmamy pamoja na Bushdady bila kusahau bush's children wanawasilimia sana.Hii kwanya iliundwa na wakimbizi kutoka burundi waliokua wakiishi ulyankuru tabora, mwanzoni mwa miaka ya 2000 serikali iliwahamisha na kuwapeleka kambi za kigoma ikiwemo nduta, kanembwa na nyarugusu, baadhi walipata nafasi za kwenda ulaya, australia na amerika kupitia unhcr na wengine kurudi kwao burudi, nilikua nafanya biashara na baadhi yao na bado tunawasiliana hata baada ya kwenda majuu, huwa wananitumia hela nawanunulia bidhaa kama nguo, dagaa na vyombo vya nyumbani, unaweza kushangaa kusikia mtu yuko us ila ananunua nguo na vyombo afrika ila ndio hali halisi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee ni kweli,kujua hizo nyimbo lazima uwe kwenye familia ya utumishi au anamjua Mungu,enzi hizo nilikuwa nazunguka na mzee kwenye mikutano ya Injili,usiku kuanzia saa moja nawasha jenereta naweka tapes za hizo nyimbo halafu mida ya saa mbili mkanda wa Mateso ya Yesu au Samson & na delila tunaweka,l.
Basi watu wanajaa,pale kwenye mateso ya watu wanaanza kulia na kutubu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaaa umenikumbusha siku nilipokutana na Babangida, Mamangida na ngida mwenyeweWasalimie mkuu, waambie Bushmamy pamoja na Bushdady bila kusahau bush's children wanawasilimia sana.
Pia sio mbaya ukitupia picha zao tuwaone walivyo hivi sasa π€π€
Daaaa,Nakulilia Jehovah ni wimbo wao Bora.Hizo kwaya tulikuwa tunasindikizwa na Sungura mjanja.
Miaka ya 90 mwanzoniIlitoka miaka ya 90 katikati huko, Ilivumaga sana kwa kweli,
Ndio zilikuwa nyimbo bora za wakati huo
Mtoto mdogo sana ww kumbe....!!?Hivi hiyo Album imetoka mwaka gani.?
Kinachofanya nizipende hizi nyimbo Mama alikua anapenda sana kuimba akiwa anatuogesha au akitwanga muhogo huo wimbo wa viumbe vyote. Kwaya nyingine ni ile ya kasulu waliimba Mke mwema..sijui wako wapi. Na wale wa Tabata waliimba sipati picha sijui walipotea wapi
View attachment 1404431
Naombeni mwenye ana audio za hizi nyimbo plz, ni hazina sana wakuu
ππππMungu katuumba kwa mfano wake
Katutofautisha na vingine
Katutofautisha na wanyama
Wasio na akili
Katupa kujua mema mabaya
Ili.
Walimwengu wengine hawajui
Aliye mkombozi
Atakayerudi kuchukua
......
Ajabu Yao, akili walipewa hawakujua aliyewapa
Kwa viumbe vyote
Old is gold
Sent using Jamii Forums mobile app