Hii kwanya iliundwa na wakimbizi kutoka burundi waliokua wakiishi ulyankuru tabora, mwanzoni mwa miaka ya 2000 serikali iliwahamisha na kuwapeleka kambi za kigoma ikiwemo nduta, kanembwa na nyarugusu, baadhi walipata nafasi za kwenda ulaya, australia na amerika kupitia unhcr na wengine kurudi kwao burudi, nilikua nafanya biashara na baadhi yao na bado tunawasiliana hata baada ya kwenda majuu, huwa wananitumia hela nawanunulia bidhaa kama nguo, dagaa na vyombo vya nyumbani, unaweza kushangaa kusikia mtu yuko us ila ananunua nguo na vyombo afrika ila ndio hali halisi.
Sent using
Jamii Forums mobile app