Naomba kujulishwa ni Spray gani itanifanya ninukie vizuri?

Naomba kujulishwa ni Spray gani itanifanya ninukie vizuri?

Romance for men, fighting temptation hizi no deodorant body spray hizi utapata kwa elfu tano au sita kila moja.
Leau d'Issey chupa ya 5mls utapata kwa elfu 10. Hii in original kabisa na harufu yake ni amazing.
Bellagio (rave culture na Ventura) deodorant.
Nivea for men hapa ndo funga kazi ingawa nyingi zinaacha rangihasa ikiwa inaelekea kuisha. Ila ziko poa hutojuta.
Zote ni chini ya elfu 10
 
Habari zenu wanajukwaa..,Mimi naomba kujulishwa ni Spray gani itanifanya ninukie vizuri yaani ki (Gentleman) ya Bei Rahisi kwanzia Buku5-10...??

NOTE:HALI YANGU YAKIPATO NI NDOGO NDIO MAANA NIKAULIZIA SPRAY NA SIO PERFUME..Ahsanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda kwenye duka la cosmetics waambie wakupe spray za Rasasi sasa nusa harufu unayoipenda katika hizo nunuwa mojawapo.

Kariakoo kwenye maduka ya jumla ni shilling 5000/= lakini mitaani ni sh 8000/=
 
Nyinyi ndio watu mnaonuka kama beberu kwenye daladala kwa kuwa mawazo yenu yamejiaminisha uturi ni kitu cha bei kubwa wakati deodorant spray kariakoo kwenye maduka ya jumla zipo mpaka za shillings 3500/= tena za kijanja kabisa.
Hahaha....mkuu punguza hasira
 
Hivi kwann mtu kauliza swali tena kwa ustaarabu kabisa halafu baadhi ya watu mnajibu vibaya jamani au kwa sababu kasema kipato chake kidogo?,kama unaona huwezi kumsaidia au kujibu soma tu na upite kimya kimya...yupo jukwaa husika kabisa..acheni hizo ndugu zangu.
Hongera sana mkuu mungu akubariki akuongeze hekma
 
Deodorant unayo tayari?!

Kwa bei hiyo unayotaka zipo spray nyingi sn mkuu tena nzuri ww nenda kwny duka la vipodozi tu
 
Pole mtoa mada kwa majibu ambayo hukuyategemea, ila jamani c lazima kuchangia kila mada, waweza soma then ukapotezea ukahamia jukwaa lingine tu. Kuhusu body spry mimi huwa situmii, natumia pafyumu inaitwa bondage ni nzuri na inakaa kwa nguo kwa mda mrefu tu! Ahsante
Nzuri sana. Huwa naitumia pia
 
Habari zenu wanajukwaa..,Mimi naomba kujulishwa ni Spray gani itanifanya ninukie vizuri yaani ki (Gentleman) ya Bei Rahisi kwanzia Buku5-10...??

NOTE:HALI YANGU YAKIPATO NI NDOGO NDIO MAANA NIKAULIZIA SPRAY NA SIO PERFUME..Ahsanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu IPO spray inayotokana na samli, bei ni sh. Buku tano tu. Wewe mwenyewe tu. Wahi coz order ni kubwa.
 
Back
Top Bottom