Naomba kujuzwa gharama za msingi kwa nyumba ya ghorofa moja

Sihitaji polee, najitambua na najua ninachokifanya, pole unahitaji wewe unayejidai Engineer halafu kichwani mtupu, unajisifu ujenzi umeanza zamani, hujui hata wahuni pia wanazeeka?
Endelea kudhihirisha uzito wa kichwa chako kwa kuingilia taaluma za watu. Napiga kazi, wateja wanaridhika na maisha yangu yanaenda swaaafi kabisa. Endelea kubwabwaja kujiona unajua kila kitu kumbe wanaojua wanakuchora tu.
 
Ni kweli chuma iko juu Sana, Ila 50M ni mbali Sana mkuu. Hiyo ramani yake hata sio kubwa kivile.
Nimejenga msingi mkubwa kuzidi huo kwa size na ugumu wa mazingira. Ila umekula around 22M, tena ni mkoa wenye vitu bei juu zaidi.
Kaka unaweza niunganisha na jamaa waliokujengea msingi
 
Mkuu unaweza niunganisha na mafundi wako msaada
 
Duuu
 
Kumbe bado nilikuwa sijafika kwenye ujenzi wa ghorofa, Muda huu nipo Kwa slab inataka kunitoa roho, nitaleta mrejesho.
Nimeanza kusoma tokea mwanzo, comment kwa comment. Nimejifunza mengi. Hongera kwa uthubutu mkuu. Na pia usiache kutupa mrejesho, inatusaidia kujipima kwa sisi tunaojipanga kujenga
 
 
MREJESHO

Hatimaye sasa nimekuja kureta mrejesho hapa,kaa kitako na ujiandae kujenga ghorofa.

1. Msingi nimetumia 8,528,200
2.Shimo la choo ni 1,237,500
3.Boma ni 5,029,200
4.Kumwaga slab ni 16,537,000
5. Kulaza Bomba za umeme kwenye slab ni 220,000
 
MREJESHO

Hatimaye sasa nimekuja kureta mrejesho hapa,kaa kitako na ujiandae kujenga ghorofa.

1. Msingi nimetumia 8,528,200
2.Shimo la choo ni 1,237,500
3.Boma ni 5,029,200
4.Kumwaga slab ni 16,537,000
5. Kulaza Bomba za umeme kwenye slab ni 220,000
Asante kwa mrejesho mkuu.
1. Slab ni mita ngapi za mraba?
2. Vipi nguzo ni ngapi na umetumia kiasi gani.
3. Boma ni full kwa floor 2 au ni ya floor ya kwanza tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…