Naomba kujuzwa hali ya maisha na fursa kati ya bumbuli (mombo) na kondoa dc

Naomba kujuzwa hali ya maisha na fursa kati ya bumbuli (mombo) na kondoa dc

Mtu kauliza Kuhusu sehemu bora, Mnaleta ujuaji na Familia za watu, Vijana mda wote wanawaza kupigiwa ndio maana stress zinawaua, kama mtu hajatulia unapigiwa mpka chumbani kwako...

Twende kwenye Mada.

Bumbuli haipo Mombo,
Mombo ni korogwe, ni njiani kuelekea bumbuli ambayo ni halmashauri nyingine ndani ya Wilaya ya Lushoto.

Kwahio Rout yako inakua

Mombo - Soni - Mbelei - Bumbuli.

Kama Shule Ni mbelei una uhakika, basi ni shule nzuri, ina mpaka advance, kwa ufupi ndio kama shule kubwa kwa halmashauri

Unaweza ukaishi hata Soni Central, ukitaka kwenda Dar miezi ya Nyuma ilikua hata 15k unaenda asaivi 18k unatoka mbelei saa 12 : 30 dar Unaingia Saa tano asubuhi, arusha nako 15k, Dom 30k, Moro 15k,.

NOTE : Kama Ni shule tofauti na Mbelei uliyoitaja..
Labda iwe Soni Day(hii ndio ipo njiani unatoka shuleni ndani ya Dk moja upo main road ya Dar) au angalau Bumbuli sec yenyewe ipo Central ila ni mbali, kinyume na hapo ACHA KABISA. Kuna shule huko unaenda kwa kutambaa..

Kuhusu Kilimo kipo Hasa mboga mboga, ufugaji n.k
Vyakula, Matunda na Mboga Ni CHEAP MNOOOOO, hasa ukiishi soni,
Hali ya hewa ni ya Ubaridi kiasi, Ila kwa ufupi ni rafiki.

Biashara Ni Changamoto kiasi kwa mgeni, kuna ile kujuana.

Singida Kalime Arizeti, Babati vitunguu,
Kondoa kafuge...., huku kote jiandae kwa jua la utosi.
Kama hutojali Taja Shule na huku nikupe Taarifa.

Call me Journey Man.
Wewe ndio umemaliza kila kituu,

Humu watu wanajitia wajanja, kumbe mda wote wanaendeshwa na Tension ya Kuchapiwa, Rubish kabisa, Mwanamke halindwi mtakufa na Pressure.
 
Mkuu mtu huishi na mkewe elewa vizuri. Kwa nini unataka kumweka mtoto wa watu mnadani wajanja wamgombanie, bint mwenyewe bado mdogo kwa hesabu za haraka hazidi 20yrs!
Ni kweli, nimeshachukua maamuzi ya kuhamia Hapo kondoa, nadhani itakua ni njia ya kufungua fursa kuliko huku kigoma nilipo.
 
Ni kweli, nimeshachukua maamuzi ya kuhamia Hapo kondoa, nadhani itakua ni njia ya kufungua fursa kuliko huku kigoma nilipo.
Kondoa ni best option...
-hali ya hewa ipo moderate sio joto wala sio baridi
-Kilimo wanalima kwa wingi mazao kama Mahindi,Alizeti,Mbaazi,Rosella n.k
-geographical advantage ipo katikati ya nchi unaweza kusafiri popote pale Tanzania hii na ukafika siku hiyohiyo
-Kibiashara unaweza kufanya biasharazako na miji ya karibu kama Dodoma ,Tanga,Singida,Kiteto,Babati,Katesh,Arusha n.k
 
Nenda Kondoa na familia yako. Bumbuli Wana umwinyi mwingi.
 
Back
Top Bottom