Naomba kuongea na wadogo zangu wa kiume walio kwenye ndoa na wanaotarajia kuingia kwenye ndoa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
NB: Talaka zimekuwa nyingi kwakuwa ndoa nyingi hazina maandalizi ya kutosha

Hii mada ilikuwa ije weekend lakini naona nakumbushwa Sana hivyo sina budi kuileta usiku huu. Maana mchuzi wa umbwa hunywewa wa moto Nitajitahidi kufupisha ili isichoshe kusoma

Ndoa za leo zinatakiwa kwenda nazo kwa tahadhari kubwa kwakuwa vijana wa sasa wanadhani wanajua zaidi kuliko wazazi. Na huko tuendako kile kiapo cha "Nitakupenda hadi kifo kitakapotutenganisha" kitabadilika na kuwa "nitakupenda hadi talaka itakapotutenganisha"

Ndoa za zamani zilidumu kwakuwa wanandoa waliandaliwa vizuri na wazazi na infact hata wachumba walitafutwa na wazazi

Zile ndoa hazikuwa kwa ajili ya waoaji tu bali kuunganisha familia ama koo mbili baada ya urafiki ama ukaribu wa muda mrefu wa wazazi wa pande zote mbili... Ndoa hizo zilichukua hadi miaka 10 mpaka kuja kuoana.. Maana wachumba walikuwa spotted tangu shule za msingi

Vigezo vilivyoangaliwa kwa msichana wakati huo pamoja na vingine hivi ndio vilikuwa vya msingi
1. Usichana wake(bikira)
2. Heshima
3. Uchapakazi
4. Vipawa/vipaji
5. Uzao wake
6. Ukaribu wa familia
7. Magonjwa ya kimwili ya kurithi na yale ya kiroho
Hayo mambo Saba yalizingatiwa Sana.. Lakini baadae yakaanza kukengeukwa.. Masharti na vigezo vikawa vinapungua kila uchao

Tukatoka kwenye hitaji la bikira mpaka mtoto. Kwamba hata kama hana usichana wake basi asiwe kazalishwa..

Tukatoka hapo tukaingia hapa! hata kama kazaa lakini kama afya iko sawa AIDS negative sawa
Tukatoka huko tukaingia kwenye elimu kipato na ajira.. Kwakuwa sasa ukimwi sio ishu tena, MTO to ndio kabisa.. Bikira sahau, elimu pia na sasa ni ajira na kipato

Kwahiyo sasa tembeeni na biti hiyo lakini lazima kwenye vile vigezo Saba bado vingi vinahitaji uzingativu
1. Bikira si sana kwakuwa siku hizi zinatoka kwa njia nyingi.. Lakini vilevile ukimpata mwenye nayo mchunguze vema.. Mabinti wengi siku hizi hulinda mlango mkubwa na kuuacha mdogo wazi.. Ni heri umpate aliyelinda mdogo akaacha wazi mkubwa! Zingatieni sana hilo

2. Mwenye maono na ndoto za kujenga familia bora... Baadhi huja kwenye ndoa si kwa mapenzi bali kutafuta ahueni ya maisha na kuchuma

3. Mchapakazi, mwenye kujituma, msafi na mwenye kujali

4. Mwenye kutoka kwenye familia iliyo elimika(achana na utajiri au umaskini), familia inayojitambua, wasio na vimelea vya ushirikina, laana za ukoo, magonjwa ya kurithi na magonjwa ya kiroho
Hii point number nne ni muhimu sana kwakuwa imevunja ndoa nyingi sana!

5. Mchunguze mtarajiwa wako kama sio sex maniac ama kama hana dalili za ukhanithi wa kike.. Ni muhimu awe moderate.. Na ni muhimu kumchunguza anapenda nini mnapokuwa faraghani.. Style nk.. Utajifunza mengi hapo.. Ngono ni sehemu ya ibada kwenye kiapo cha ndoa.. Hivyo pamoja na kusemwa mapenzi ni uchafu.. Lakini kuna usafi wa kimwili na kiroho pia.. Pa mtumba sawa lakini at least use grade one au two.. Lisiwe lonya..

6.. Zingatia sana hii point hapa! Chumbia/oa binti wa imani yako ama inayokaribiana na yako... Chumbia/oa wa kabila lako ama anayekaribiana na kabila lako.. Hapa muingiliano wa imani na tamaduni umevunja ndoa nyingi sana!
7.. Chumbia mwanamke wa kawaida, mwenye vigezo vya kawaida.. Wanawake wazuri sana hawafai/hawawezi ndoa.. Ni pambo la wengi litakutesa.. Chumbia mwenye tabia zinazorekebishika.. Aliyeshindikana kwa tabia fulani jitenge naye atakutesa. Kwa mfano, hasira, uchoyo, wivu majungu rohombaya nk

8. Unachumbia/kuoa mtu utakayeishi naye miaka yote mpaka kifo... Hivyo una mengi ya kufanya.. Epuka uchumba wa miezi sita mwaka mmoja.. Kumfahamu walau nusu inakuhitaji si chini ya miaka mitatu
Vilevile si kwamba unaoa supermarket kwamba utakuta kila kitu humo.. Vingine utapaswa kuongeza taratibu.. Unaoa mtu ambaya hamkuwa wote tangu udogoni hivyo kuna kipindi cha mpito cha kurekebishana ili mfiti.. Sometimes ni kipindi chenye changamoto zake.. Stay focused.. Show your support, love and caring
Mfahamu January yake mpaka December kila mwezi.. Wiki yake Monday to Sunday.. Siku yake kukicha mpaka kukichwa
Nitaendelea
 
Sehemu ya pili
Sisi tulipelekwa jando na kupata masomo ya ukakamavu. Nyie hamna hiyo bahati... Jitahidini sana kumudu majukumu ya faraghani.. Fanya yote kwa ukamilifu wake lakini hilo lipe umuhimu no 1. Vijana wengi wamefeli hapo. Tendo la ndoa ni sadaka na zawadi ya upendo...usilipuuze. Hutatoboa..😀 Jali sana hisia zake kwenye hilo..Tendo la ndoa ni ukamilifu wa kiapo cha uwili katika mwili mmoja...
Simama kama baba
Simama kama kiongozi na mhimili wa familia
Simama kama mbeba maono, mfariji..
Na sometimes simama kama kaka ama rafiki kwake
Ni muhimu kulinda urijali wako kwa wivu mkubwa kwa maana hiyo ndio maana ya kuitwa mwanaume.. Jilindeni na nyeto na X movies. Zingatieni vyakula na mazoezi
LA mwisho na muhimu sana tambueni mipaka ya familia na marafiki.. Muda wa familia na marafiki
Ishini kwa ibada na usafi wa kiroho.. Kataeni maroho ya ushoga, kulelewa...
Je kuna nilichobakisha!? Nikumbusheni🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
1000043819.jpg
 
NB: Talaka zimekuwa nyingi kwakuwa ndoa nyingi hazina maandalizi ya kutosha

Hii mada ilikuwa ije weekend lakini naona nakumbushwa Sana hivyo sina budi kuileta usiku huu. Maana mchuzi wa umbwa hunywewa wa moto Nitajitahidi kufupisha ili isichoshe kusoma

Ndoa za leo zinatakiwa kwenda nazo kwa tahadhari kubwa kwakuwa vijana wa sasa wanadhani wanajua zaidi kuliko wazazi. Na huko tuendako kile kiapo cha "Nitakupenda hadi kifo kitakapotutenganisha" kitabadilika na kuwa "nitakupenda hadi talaka itakapotutenganisha"

Ndoa za zamani zilidumu kwakuwa wanandoa waliandaliwa vizuri na wazazi na infact hata wachumba walitafutwa na wazazi

Zile ndoa hazikuwa kwa ajili ya waoaji tu bali kuunganisha familia ama koo mbili baada ya urafiki ama ukaribu wa muda mrefu wa wazazi wa pande zote mbili... Ndoa hizo zilichukua hadi miaka 10 mpaka kuja kuoana.. Maana wachumba walikuwa spotted tangu shule za msingi

Vigezo vilivyoangaliwa kwa msichana wakati huo pamoja na vingine hivi ndio vilikuwa vya msingi
1. Usichana wake(bikira)
2. Heshima
3. Uchapakazi
4. Vipawa/vipaji
5. Uzao wake
6. Ukaribu wa familia
7. Magonjwa ya kimwili ya kurithi na yale ya kiroho
Hayo mambo Saba yalizingatiwa Sana.. Lakini baadae yakaanza kukengeukwa.. Masharti na vigezo vikawa vinapungua kila uchao

Tukatoka kwenye hitaji la bikira mpaka mtoto. Kwamba hata kama hana usichana wake basi asiwe kazalishwa..

Tukatoka hapo tukaingia hapa! hata kama kazaa lakini kama afya iko sawa AIDS negative sawa
Tukatoka huko tukaingia kwenye elimu kipato na ajira.. Kwakuwa sasa ukimwi sio ishu tena, MTO to ndio kabisa.. Bikira sahau, elimu pia na sasa ni ajira na kipato

Kwahiyo sasa tembeeni na biti hiyo lakini lazima kwenye vile vigezo Saba bado vingi vinahitaji uzingativu
1. Bikira si sana kwakuwa siku hizi zinatoka kwa njia nyingi.. Lakini vilevile ukimpata mwenye nayo mchunguze vema.. Mabinti wengi siku hizi hulinda mlango mkubwa na kuuacha mdogo wazi.. Ni heri umpate aliyelinda mdogo akaacha wazi mkubwa! Zingatieni sana hilo

2. Mwenye maono na ndoto za kujenga familia bora... Baadhi huja kwenye ndoa si kwa mapenzi bali kutafuta ahueni ya maisha na kuchuma

3. Mchapakazi, mwenye kujituma, msafi na mwenye kujali

4. Mwenye kutoka kwenye familia iliyo elimika(achana na utajiri au umaskini), familia inayojitambua, wasio na vimelea vya ushirikina, laana za ukoo, magonjwa ya kurithi na magonjwa ya kiroho
Hii point number nne ni muhimu sana kwakuwa imevunja ndoa nyingi sana!

5. Mchunguze mtarajiwa wako kama sio sex maniac ama kama hana dalili za ukhanithi wa kike.. Ni muhimu awe moderate.. Na ni muhimu kumchunguza anapenda nini mnapokuwa faraghani.. Style nk.. Utajifunza mengi hapo.. Ngono ni sehemu ya ibada kwenye kiapo cha ndoa.. Hivyo pamoja na kusemwa mapenzi ni uchafu.. Lakini kuna usafi wa kimwili na kiroho pia.. Pa mtumba sawa lakini at least use grade one au two.. Lisiwe lonya..

6.. Zingatia sana hii point hapa! Chumbia/oa binti wa imani yako ama inayokaribiana na yako... Chumbia/oa wa kabila lako ama anayekaribiana na kabila lako.. Hapa muingiliano wa imani na tamaduni umevunja ndoa nyingi sana!
7.. Chumbia mwanamke wa kawaida, mwenye vigezo vya kawaida.. Wanawake wazuri sana hawafai/hawawezi ndoa.. Ni pambo la wengi litakutesa.. Chumbia mwenye tabia zinazorekebishika.. Aliyeshindikana kwa tabia fulani jitenge naye atakutesa. Kwa mfano, hasira, uchoyo, wivu majungu rohombaya nk

8. Unachumbia/kuoa mtu utakayeishi naye miaka yote mpaka kifo... Hivyo una mengi ya kufanya.. Epuka uchumba wa miezi sita mwaka mmoja.. Kumfahamu walau nusu inakuhitaji si chini ya miaka mitatu
Vilevile si kwamba unaoa supermarket kwamba utakuta kila kitu humo.. Vingine utapaswa kuongeza taratibu.. Unaoa mtu ambaya hamkuwa wote tangu udogoni hivyo kuna kipindi cha mpito cha kurekebishana ili mfiti.. Sometimes ni kipindi chenye changamoto zake.. Stay focused.. Show your support, love and caring
Mfahamu January yake mpaka December kila mwezi.. Wiki yake Monday to Sunday.. Siku yake kukicha mpaka kukichwa
Nitaendelea
Umenena kweli Mshana, naongeza msisitizo kwa video hii👉
Ndoa sio kitu cha kujaribisha...
View: https://youtu.be/kGAWwqS9h-8?si=kL0BNYxLBBjE21vK
 
Mkuu hongera sana kwa bandiko hili lenye nondo Mungu,ila mimi nina maswali naomba niulize
Nina mahusiano na binti mmoja tukiwa pamoja mfano nimnunulie kitu eg hata kitu fulani cha kula ambacho mnaweza kushare yeye badala ya kunipa/kunikatia huwa ananiniuliza kwamba nikupe?na si kwamba anipe halafu mimi nikatae,
Pili,Tukiwa kwenye mazungumzo huwa nachomekea kwa kumuuliza uliongea lini na dada/kaka yako huwa ananijibu mimi mtu asiponipigia simu na mimi huwa sijihangaishi naye
Sasa mkuu,kwa akili zangu fupi nimeona huyu mtu kama ana tabia fulani ya uchoyo na roho mbaya nitakua sawa au nataka kumhukumu tu vibaya?nipe ushauri wako
 
Back
Top Bottom