Naomba kupata taarifa kuhusu kisiwa cha Mafia

Daah hii dunia ngumu Sana kweli ajikwezaye hushushwa yaani ulichoandika kinakutafsiri Kama mshamba
Hiyo ni tafsiri yako.

Mimi sikubaliani na maoni yako na nayaacha kama alivyo.

Maswali ya kitoto kauliza, na huo ndio utakuwa msimamo wangu.

Swali la msingi ni 1 tu hapo, upatikanaji wa huduma za kijamii.

Mengine yote ni rubbish.
 
Hiyo ni tafsiri yako. Mimi sikubaliani na maoni yako na nayaacha kama alivyo. Maswali ya kitoto kauliza, na huo ndio utakuwa msimamo wangu.
Swali la msingi ni 1 tu hapo, upatikanaji wa huduma za kijamii. Mengine yote ni rubbish.
Hivi hakuna watu wanaokaa utende halaf ofisi zao za kazi zipo chole juani au jibondo?? Je wanatumia usafiri gani kwenda makazini kwao
 
Asilimia kubwa ya wakazi wa kule hawajasoma zaidi ya kwenda madrasat tu, hivyo kama una watoto ama huyo mdogo wako ana Watoto na anataka wasome basi awaache huko huko anakosihi aende Mafia yeye tu peke yake.
 
Hivi hakuna watu wanaokaa utende halaf ofisi zao za kazi zipo chole juani au jibondo?? Je wanatumia usafiri gani kwenda makazini kwao
Okay, tunaizungumzia mafia as kisiwa per se au Mafia as wilaya?

Twende pole pole. Ntakujibu swali lako ukinijibu hilo hapo.
 
Kimtindo Mafia ni pagumu kwa mtumishi wa umma ambaye ni mgeni.

Huduma zote muhimu za kijamii zipo kwa maeneo ya katikati ya mji wa Mafia.

Changamoto za Mafia.

1. Usafiri wa kwenda au kutoka Mafia. (Sio wa uhakika sana)

2. Mgeni kuweza kujichanganya na wenyeji.

3. Magonjwa ya kuambukiza (kama Malaria, kuharisha).

4. Imani na vitisho vya kishirikina.

Eneo lolote ukiona watumishi wengi wa umma wanaogopa kupangiwa au wanajitahidi kuhama kila wakipangiwa, basi ujue lina shida kubwa.
 
K
Mafia kuzuri sana dada yangu,
  1. Watu wa Mafia nzima wanafahamiana
  2. Dhuruma hakuna
  3. Dereva wa gari la serikali asipokupa lift, kamsemee kwa diwani, kesi itafika baraza la madiwani hatua zitachukuliwa dhidi yake
  4. Watu wa Mafia hawana makuu, ukikosea omba msamaha yanakwisha hawana malipizi
  5. Mambo ya kupigana fimbo ati umekula mchana hayapo
  6. Watu wa mafia wanaishi kwa uaminifu sana, ukiwa huna pesa watakukopesha tu ila uwe mwaminifu kurudisha kwa wakati
  7. Ukiishiwa ukaenda kwa jirani atakusaidia na hakuna masimango siyo kama Kwamtogole Dar
  8. Hakuna polution, hewa ni clean
  9. Ukitaka kwenda airport huna haja ya taxi, ni bajaj tu au miguu yako maana haiko mbali
  10. Kwa ndege Mafia to Dar ni 30 minutes umefika
  11. Upana wa kisiwa ni takribani Km 19 na urefu Km 70
  12. Kiukweli kile ni kisiwa cha amani
 
Ina maana unaenda jioni mpaka asubuhi ndo mnafika?
Mwambie usafiri siku hzi kutoka nyamisati hadi mafia wanatoaka alasiri huko mafia watafika saa 12 au saa moja asisahau kitambulisho kitakachomtambulisha yeye ni mtanzania
 
Kumbe ni kisiwa kikubwa tu.
Km 70 ni Sawa na kutoka mwenge Hadi bagamoyo
 
MAFIA HAINA BUDI KUINULIWA KWANI NDICHO KISIWA CHETU KILICHOPO BAHARINI KIINULIWE KWA HALI ZOTE,KIWE MAPED UPYA KISASA BANDARI ZA WASTANI ZIJENGWE HUKO MADUKA YA KISASA (FREE PORT ACCESS) ISLAND. AT LEAST KIFIKIE HADHI YA NUSU DUBAI.
 
Ngombe kabisa Sasa Google map ingenipa details nilizopata hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…