Naomba kuuliza kwa wote wanaomuamini Yesu

halafu usafiri alitumia punda, hakupanda toyo
 
Hiyo ni imani yako,na inaweza ikawa ni kishamba tu hata MUNGU haitambui, eti ikitungwa mimba kuna dua inasomwa, aliyekwambia watu wengine hawaombei mimba zao nani?watu wengi kwenye hizi imani mmevaa ujinga mwingi sana wa kidharau imani ya mwingine ilihali yamkini ninyi ndo mko wrong kuliko hata mpagani
 

Unajua kabla ya kuzaliwa Mariam Yesu alikuwepo?
 
Elewa nachozungumza mkuu hili jambo hata sio la kuhitaji ubishi, nakwambia anayekusudiwa hapo ni mmoja pamoja ingawa kuna hizo tofauti kutoka kwenye vyanzo tofauti. Sasa ukisema hao ni watu wawili tofauti vp hayo mengine wanayofanana?


Mfano waislamu huwa wanazungumzia viumbe majini kwamba ni viumbe vilivyoumbwa kwa moto na kwamba kuna wema na waovu ila wakristo wanasema majini ndio wale malaika waovu na ukiangalia sifa za majini zinazoelezwa ni tofauti na hao malaika, je tuseme Mungu kaumba malaika ambao ndio kuna wengine ni wale malaika waovu na pia kaumba viumbe majini?
 
Ni Upuuzi mkubwa sana kumuamini Mtu aliyejitokea tu Pangoni mwaka 600AD kisha akaanza kusema yaliyotokea mwaka 33AD Ni uongo....
Na kwamba yeye ndiye mkweli Wakati hata kusoma na Kuandika Tu Hufahamu.

Ni hudhuni kwa kweli.
Lakini ukisoma kitabu chake hakina makandokando kinaeleza ukweli mtupu
 
Ni Upuuzi mkubwa sana kumuamini Mtu aliyejitokea tu Pangoni mwaka 600AD kisha akaanza kusema yaliyotokea mwaka 33AD Ni uongo....
Na kwamba yeye ndiye mkweli Wakati hata kusoma na Kuandika Tu Hufahamu.

Ni hudhuni kwa kweli.
Kwahiyo point ni kutangulia kusema ndio huhesabika kuwa ni yaliyosemwa ni ya ukweli?
 
Pole sana ndugu yangu na mimi mwenywe nilikuwa kama wewe nilikuwa nafuata ya wanadamu baadala ya mwenyezi Mungu
 
Elewa nachozungumza mkuu hili jambo hata sio la kuhitaji ubishi, nakwambia anayekusudiwa hapo ni mmoja pamoja ingawa kuna hizo tofauti kutoka kwenye vyanzo tofauti. Sasa ukisema hao ni watu wawili tofauti vp hayo mengine wanayofanana?
Dah! Isa mama yake ni Mariam mtoto wa Amrani.
Mariam mtoto wa Imrani katika Biblia ni dada wa Musa na Haruni. Kwa mujibu wa Biblia waliishi miaka yapata 900+ kabla ya Yesu.

Sasa kama kwenye Biblia angetajwa mtoto wa Mariamu dada wa Musa tjen akaja mtu akasema huyu ndio Isa wa Qurani, kichaa pekee angekataa. Kwa sababu kimsingi angekuwa mi mtu yule yule.

Ika kusema Mariam aliyeishi karne ya 1000BC somehow ndiye Mariamu aliyeishi karne ya 1AD haina mantiki kabisa
Hii ndii similarity ambayo tunaweza sasa kuijadili kwa sababu Biblia pia inasema Malaika wana asili ya moto na kuwa kuna malaika waasi na Malaika wema. At least hiki ni kitu ambacho kina mantiki ya kujadili bila kulazimishia
 
common sense isn't common.
hao wengine wanaoniona sina maarifa ni akina nani?hao wengine ndiyo wamekutuma uje uniambie kuwa na mimi sina maarifa ama umejituma mwenyewe?.
unaponikot make sure unajadiliana na mimi kama mimi si kuingiza {WENGINE}.
unaponikot na kuingiza wengine ambao hawajanikot hata kuona Comment yangu huo ni usingiziaji .
ulipaswa useme tu hata wewe(mimi) huna maarifa na uwe tayari kuonyesha maarifa nisiyonayo kama mimi nilivyoonyesha uputu wa maarifa ya Charles.

furthermore sijasema nina maarifa yote kwasababu hakuna anae jua kila kitu. ,nimesema:, Mungu anasema(si mimi) "WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA". uenda ningelikuwa na sehemu ya maarifa anayokusudia Mungu niwe nayo nisingelikujibu hata hii Comment yako, ningelikuupuza tu.

na kuhusu dini kuwa false ilo halinihusu since mi si muumin wa dini watag wenye dini zao waje wakujibu dai lako. Mungu ninaemjua mimi hana Dini. ukianzisha mjadala kuhusu huyo Mungu ni tag.
 
Kuna dini za hovyo sana hata ukitumia akili za kuvukia barabara huwezi kuwa muumini wa dini hizo.
Imagine kuna dini ukivaa kama alivyovaa mtume unapata thawabu, ukila kitimoto ni dhambi kubwa kuliko kufuga majini
 
Mambizi, hili jibu linamtosha
 

Wanaume kuvaa kanzu au baibui kwa wanawake ni utamaduni, kuna wakristo kibao wanavaa kanzu au baibui ingawa sio utamaduni asili wa africa.. wakristo wanasujudu pia
 
Mababu zetu walivaa magome ya miti wewe unavaa?
 
Sifa za majini ni tofauti na malaika, kwanza waislamu wanawazungumzia majini kama viumbe ambao wameumbwa na Mungu na si kwamba ni kundi fulani la malaika ila wakristo hawasemi kwamba Mungu aliwahi kuumba majini bali kundi fulani la malaika ndio huwaita majini na ukiangalia sifa za hao majini ni tofauti na malaika.

Ila cha kushangaza mkristo hukataa Yesu kuwa ndio Isa ila wanalazimisha majini ndio kuwa ndio malaika waliyoasi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…