Naomba kuwaaga rasmi Wana JF, nikipona tutakuwa pamoja tena

Chochote unachopitia sasa kitaisha salama na kila kitu kitakuwa sawa. Kila kitu kitarudi kama kilivyokuwa awali.
 
Daah pole sana mpendwa una tatizo gani unaloumwa au nini kimekupata mkuu tuambie halafu nakuomba kama unasoma hapa mwombe Mungu akusamehe kila jambo ulilotenda na elewa Mungu ni mponyaji
 
Lo bibie Beaty una uthbutu wa imani na nguvu ya nafsi.
Mungu akuponye, maana Yeye kwake hakuna lililo kubwa asiloliweza.
Upone haraka na usikate tamaa.
Naamini Mama Samia huwa anapita humu , naomba aione hii.
 
Mkuu usikate tamaa Kama Ni 19 inazungumzika."HAKUNA DHAMBI MBAYA KAMA KIKATA TAMAA.KWA UWEZO WA MUNGU UTAPONA NA KURUDI KWENYE HALI YA KAWAIDA AMINI HIVYO MKUU
 
Nakutakia heri urudi. Nakumbuka mwaka jana ushimen alibananishwa na homa akatuaga ila hadi leo yupo anadunda.
 
Katiba iliyopo haipewi heshima ....hiyo mpya unafikiri ndio itaheshimika..?

Ila poa... Wewe nenda tu...
Katiba mpya itapatikana tu... Sijui lini lakini.
Ila tutapambana kuidai katiba mpya tukiwa nyuma ya keyword, maana wengi wetu ni wanaharakati feki na ndiyo maana raia wengi wanatuponda na kuona bora wabaki na kijani yao.

Mambo ni mengi mno...

Katiba mpya tutaipata... Ila hakuna atakaye ifuata.. Itakuwa kama katiba iliyopita...hakuna aliyeifuata... JK alitaka kuifuta na kuweka mpya... Kumbe alikuwa anatuzuga tu... Hao ndio wanasiasa....JPM "katiba mpya sio kipaumbele changu kwa sasa"... Mama Samia... Sijui.. Labda anaweza kuanza mchakato sasa...
 
Ujumbe mzito huu!Pole sana kwa maumivu,Mungu ni mwema.
 
Ngoja niwasiliane na wadau waliopo regency kama ndo jina lake halisi ndo ilo nitawetea mrejesho nini kinamsibu wakuu
 
Pole sana, Mungu akuongezee siku za kuishi duniani ili siku moja uishuhudie katiba mpya!
 
Pole ila usiogope



Hakunaga kifo kwa wale wanaomwamini MUNGU Ambaye yu hai niamini mm
 
Mwenyezi Mungu,
Naomba ukaudhihirishe ukuu wako mtakatifu kwa Beatrice kwa Nguvu yako iliyo Kuu akapokee uponyaji na kuinuka tena!
 
Mungu ni waajabu sana!!
Utarudi humu ukiwa na Afya tele.
Endelea kumtumainia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…