Naomba mfano wa Taifa lililoshusha gharama ya maisha kwa kutumia Katiba?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Pengine ufahamu wangu una shida ya kuelewa polepole au kuna mambo yananipita kushoto. Kwa jinsi ninavyowasikiliza wanasiasa wanavyoizungumzia katiba mpya ni kana kwamba katiba mpya ikipatikana leo kesho changamoto zote zitakwisha, au chini ya katiba iliyopo hatuna uwezo wa kuivisha chochote.

Katiba mpya haitamaliza wizi, uzembe, majungu, ujinga, uvivu, nk

Mambo yanayolalamikiwa sana kwenye katiba iliyopo ni
Madaraka ya rais
Tume huru
Muungano
Nk

Hayo yoote sioni ni vipi yatashusha gharama ya maisha.

Labda wajuvi mje na taifa lililowahi kufanikiwa kushusha gharama ya maisha kwa kutumia KATIBA.
 
1. Ukubwa wa madaraka ya Rais. tamko au matakwa ya Rais ni amri hii kwa sababu ya ukubwa wa madaraka yake ivyo akitoa tamko ambalo lipo kinyume na kanuni za kiuchumi inaweza ikapelekea kuongezeka sana au kupanda kwa bei ya bidhaa mfano kipindi cha magufuri aliingilia kati suala la korosho matokeo yake soko lilivurugika na kupelekea wakulima kupata hasara, alitumia approach za kibabe sana kushughulika na wawekezaji tukaona watu walifunga biashara, pia mwanzoni mwa uongozi wake alitoa tamko kuhusu sukari tuliona bei ya sukari ilipanda sana, mambo kama hayo yanasababisha ugumu wa maisha kwa mwananchi kama kungekua na namna ya kumpiga break Rais asiingilie kila kitu uenda hali ingekua nzuri

2. Tume huru ya uchaguzi. Inapokosena tume huru maana yake kuna uwezekano wa kupata viongozi wasiokua na uwezo ilmradi tu wawe na connection na mamlaka, hii itapelekea viongozi kubweteka wakijua hata wakiboronga uchaguzi ukija watapita tu hata kwa bao la mkono matokeo yake wanafanya maamuzi bila kujari hali za wananchi mfano kuongeza tozo, kodi kandamizi n.k. Kungekua na tume huru wangeumiza vichwa kuja namna nzuri ya kushughulikia matatizo bila kuumiza wananchi maana wangejua wakialibu baada ya miaka mitano watahukumiwa kwenye sanduku la kura
 
Libya ambayo kila siku mnaisifia humu ilifika pale sababu ya mabadiliko ya uongozi wa nchi ambayo Gadaffi aliyaita "Revolution"

Gadaffi alibadili katiba kwa kuja na The green book
Kwa hiyo unakusudia kusema hata katiba ya libiya ya gadafi ni ya kupigiwa mfano iliyomuweka madarakani Kwa miaka 40?
 
Pengine ufahamu wangu una shida ya kuelewa polepole au kuna mambo yananipita kushoto. Kwa jinsi ninavyowasikiliza wanasiasa wanavyoizungumzia katiba...
Mfano serikali imeleta tozo kama chanzo Cha Mapato kwenye bajeti.

Wananchi mtapiga kelele na kuwaambia wabunge wakatae bajeti Ile.

Kwa katiba ya sasa wabunge wakipinga hiyo bajeti eti kisa Ina tozo kibao, basi inampa mamlaka Rais kuvunja bunge!!! Mbunge Gani Yuko tayari kurisk cheo chake kisa kupinga bajeti??

Ila kupitia katiba mpya wabunge watakua na haki ya kuisimamia serikali na Hawa risk kupoteza nafasi zao kisa kupinga bajeti mbovu.

Hilo ni Moja tu mifano ni mingi sana
 
Pengine ufahamu wangu una shida ya kuelewa polepole au kuna mambo yananipita kushoto. Kwa jinsi ninavyowasikiliza wanasiasa wanavyoizungumzia katiba mpya ni kana kwamba katiba mpya ikipatikana leo kesho changamoto zote zitakwisha, au chini ya katiba iliyopo hatuna uwezo wa kuivisha chochote.

Katiba mpya haitamaliza wizi, uzembe, majungu, ujinga, uvivu, nk

Mambo yanayolalamikiwa sana kwenye katiba iliyopo ni
Madaraka ya rais
Tume huru
Muungano
Nk
Hayo yoote sioni ni vipi yatashusha gharama ya maisha.

Labda wajuvi mje na taifa lililowahi kufanikiwa kushusha gharama ya maisha kwa kutumia KATIBA.
Acheni upotoshaji, katiba mpya haija contain ubora wa maisha kwa wananchi tu bali inajenga mustakabali mpya wa Taifa na muongozo thabiti kwa maendeleo ya nchi. Acheni ujinga wa kusema katiba mpya haikuletei chakula nyumban shubaamit!
 
Huyu alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kutumia akili zake vizuri.
Anasema lengo lake huo mfumo wake ungefikia hatua ya juu kabisa basi binadamu wasingekuwa interested na material things na hivo pesa isingekuwa inatumika na hivo watu wasingehitaji pesa

Lengo lake kila mtu awe na nyumba nzuri nk hivo ukiwa na kila kitu hutohitaji pesa au kumake profit
 
Kwa hiyo unakusudia kusema hata katiba ya libiya ya gadafi ni ya kupigiwa mfano iliyomuweka madarakani Kwa miaka 40?
Katika hili sitaki kutoa maoni yangu,nimeweka hapo link ya Green book,isome alafu linganisha na maendeleo waliyofikia Libya wakati wa Gadaffi utapata opinion yako mwenyewe

Nataka kila mtu awe na opinion yake
 
Pengine ufahamu wangu una shida ya kuelewa polepole au kuna mambo yananipita kushoto. Kwa jinsi ninavyowasikiliza wanasiasa wanavyoizungumzia katiba mpya ni kana kwamba katiba mpya ikipatikana leo kesho changamoto zote zitakwisha, au chini ya katiba iliyopo hatuna uwezo wa kuivisha chochote.

Katiba mpya haitamaliza wizi, uzembe, majungu, ujinga, uvivu, nk

Mambo yanayolalamikiwa sana kwenye katiba iliyopo ni
Madaraka ya rais
Tume huru
Muungano
Nk
Hayo yoote sioni ni vipi yatashusha gharama ya maisha.

Labda wajuvi mje na taifa lililowahi kufanikiwa kushusha gharama ya maisha kwa kutumia KATIBA.

Mkuu wayajua haya kwenye katiba yetu:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe?
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe?
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu?
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi?
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe?
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi?
7. Kuna rundo kubwa la vigogo wasio na tija na wasiolipa kodi wanaopata uhalali tokea katika katiba yenyewe?
8. Nk, nk.

Kimsingi ndiyo maana Hata pesa zetu zaishia China Kwa mujibu wa katiba.

Huoni tukiwa na mpya mapungufu kama haya tukayaziba tutaweza kupiga hatua?
 
Libya ambayo kila siku mnaisifia humu ilifika pale sababu ya mabadiliko ya uongozi wa nchi ambayo Gadaffi aliyaita "Revolution"

Gadaffi alibadili katiba kwa kuja na The green book
Hili ni jibu tosha !
 
Mkuu wayajua haya kwenye katiba yetu:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe?
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe?
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu?
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi?
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe?
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi?
7. Kuna rundo kubwa la vigogo wasio na tija na wasiolipa kodi wanaopata uhalali tokea katika katiba yenyewe?
8. Nk, nk.

Kimsingi ndiyo maana Hata pesa zetu zaishia China Kwa mujibu wa katiba.

Huoni tukiwa na mpya mapungufu kama haya tukayaziba tutaweza kupiga hatua?
Mkuu unaweza kutusaidia kutuwekea hapa hivyo vifungu na namna vinavyosababisha gharama kupanda kuliko hivi unavyotaja jumlajumla.
 
Kwamba wewe hujui:

1. Kuwa kwa mujibu wa katiba hii kuna watu hawawezi kushtakiwa?
2. Kama hawawezi kushtakiwa kumbe kipi kinawasimamisha kufanya nini?
3. Kama hawawezi kushtakiwa ila sisi, pana usawa gani mbele ya sheria?
4. Wewe hujui kuwa kuna vigogo wasiolipa kodi kwenye malipo yao lukuki wanayopata?
5. Wewe hujui kuwa wilayani Kuna DC, DAS, DED na hali kadhalika mikoani ambayo duplication ya vyeo tu kimsingi?
6. Nk, nk.

Huyajui hayo ndugu kuwa ni kwa mujibu wa katiba hiyo?
 
Katiba inakuletea aina ya viongozi mbalimbali na namna ya kutumia rasilimali zilizopo kumaliza changamoto zilizopo; na hao viongozi walioletwa na katiba ndio wanatakiwa kutatua changamoto zilizopo; kama changamoto bado zipo, ina maana katiba haijafanya kazi vizuri; ndio maana jamii inataka katiba mpya itakayotatua changamoto zilizopo.​
 
Kama tungekuwa na Katiba itakayotamka wazi idadi ya wizara unadhani leo hii tungekuwa mzigo wa kulipa mishahara na posho za msururu wa mawaziri wengine hata kazi zao zinaingiliana?

Kama mawaziri wetu wangepatikana kwa njia ya kutuma maombi na kuangaliwa nani ana vigezo unadhani tungekuwa na hawa akina Mwigulu?

Yapo mambo meengi sana, Katiba ndio inayokupa viongozi sahihi.
 
Pengine ufahamu wangu una shida ya kuelewa polepole au kuna mambo yananipita kushoto. Kwa jinsi ninavyowasikiliza wanasiasa wanavyoizungumzia katiba mpya ni kana kwamba katiba mpya ikipatikana leo kesho changamoto zote zitakwisha, au chini ya katiba iliyopo hatuna uwezo wa kuivisha chochote.

Katiba mpya haitamaliza wizi, uzembe, majungu, ujinga, uvivu, nk

Mambo yanayolalamikiwa sana kwenye katiba iliyopo ni
Madaraka ya rais
Tume huru
Muungano
Nk
Hayo yoote sioni ni vipi yatashusha gharama ya maisha.

Labda wajuvi mje na taifa lililowahi kufanikiwa kushusha gharama ya maisha kwa kutumia KATIBA.
Ujinga wa baadhi ya watanzania ni mkubwa sana na wewe ukiwemo! Katiba ni mwongozo wenye taratibu na kanuni za kutenda yote katika nchi. Kama hakuna miongozo na sheria nzuri hatuwezi kuendelea. Mfano katiba iliyopo inamruhusu rais kuamua yeye mwenyewe kupeleka fedha pale apendapo na ndiye mwamuzi wa mwisho. Tumeona jinsi jambo hili lilivyotutia hasara kwa rais kutumia mwanya huu kufanya maamuzi mabaya.
 
Hawa hawa siku Rais Samia akisema sasa tunaandika katiba mpya...wata mpongeza mama, na kuja kusema eti wametoa machozi ya furaha.

Ni hawa hawa watamsifia na kuimba kila aina ya mapambio pale katiba mpya itakapo kuwa mezani.

Hawa si watu wanaofikiria..si watu wenye agenda..ni watu ambao wanajua kusifia tu kulingana na upepo wa boss.
 
Pengine ufahamu wangu una shida ya kuelewa polepole au kuna mambo yananipita kushoto. Kwa jinsi ninavyowasikiliza wanasiasa wanavyoizungumzia katiba mpya ni kana kwamba katiba mpya ikipatikana leo kesho changamoto zote zitakwisha, au chini ya katiba iliyopo hatuna uwezo wa kuivisha chochote.

Katiba mpya haitamaliza wizi, uzembe, majungu, ujinga, uvivu, nk

Mambo yanayolalamikiwa sana kwenye katiba iliyopo ni
Madaraka ya rais
Tume huru
Muungano
Nk
Hayo yoote sioni ni vipi yatashusha gharama ya maisha.

Labda wajuvi mje na taifa lililowahi kufanikiwa kushusha gharama ya maisha kwa kutumia KATIBA.

..Canada inatoa kifuta machozi kwa wananchi wake wasiokuwa na ajira. Je, huko sio kushusha gharama za maisha?

..Pia kwenye nchi za wenzetu [ ulaya + marekani] BUNGE huweka ukomo wa serikali kukopa. Deni la serikali linaathiri hali maisha ya wananchi ikiwa halitadhibitiwa.
 
Back
Top Bottom