Poa 2
JF-Expert Member
- Jul 7, 2019
- 1,317
- 1,320
Katiba nzuri ndio inayotupatia viongozi wazuri na katiba ya hovyo hutupatia viongozi wa hovyoPengine ufahamu wangu una shida ya kuelewa polepole au kuna mambo yananipita kushoto. Kwa jinsi ninavyowasikiliza wanasiasa wanavyoizungumzia katiba mpya ni kana kwamba katiba mpya ikipatikana leo kesho changamoto zote zitakwisha, au chini ya katiba iliyopo hatuna uwezo wa kuivisha chochote.
Katiba mpya haitamaliza wizi, uzembe, majungu, ujinga, uvivu, nk
Mambo yanayolalamikiwa sana kwenye katiba iliyopo ni
Madaraka ya rais
Tume huru
Muungano
Nk
Hayo yoote sioni ni vipi yatashusha gharama ya maisha.
Labda wajuvi mje na taifa lililowahi kufanikiwa kushusha gharama ya maisha kwa kutumia KATIBA.
Viongozi ndio wanatakiwa kutatua changamoto zetu kama maji,uchumi, biashara, chakula, miundombinu n.k.
wakipatikana viongozi wa hovyo hayo yote yatakuwa ndoto kama ilivyo Sasa miaka 60 ya uhuru bado maji,elimu na chakula ni tatizo sana kwa nchi yenye ardhi kubwa na heti kilimo ndio UTI wa mgongo
Katiba nzuri ni Ile inatoa usawa kwa watu wote inawajibisha kwa usawa na hakuna aliye juu ya sheria.
Viongozi ndio wanapanga hatima ya mwananchi katika Kila jambo.