Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Pengine ufahamu wangu una shida ya kuelewa polepole au kuna mambo yananipita kushoto. Naomba mfano wa taifa lililoshusha gharama ya maisha kwa kutumia Katiba?
Kwanza kwa kutambua tu kuwa ufahamu wako una shida ya kuelewa na mambo mengi yanakupita kushoto, jina tu The Phylosopher ni ishara ya ufinyu huo. Bila shaka hata hujui kwa nini taifa linahitaji kuwa na Katiba!
Kwa kukujuza tu The Phylosopher, neno sahihi ni philosopher na si phylosopher. Katiba ni maamuzi ya wananchi kuhusu watakavyoweza kuishi pamoja na kuboresha maisha yao kwa uhuru na haki sawa kwa wote.
Kwa katiba ya sasa ni wenye nguvu wanaokula kwa urefu wa kamba zao na kuvimbiwa huku wanyonge wakilala njaa. Tunasahau kuwa Katiba ndio msingi mkuu wa maendeleo kwa binadamu waliojaaliwa akili.
Kwa kutojaaliwa na akili mnyama wa mwituni hahitaji Katiba wala taratibu za kuishi pamoja. Kwa wenye uelewa wa shida kama wewe huwezi kuona umuhimu wa Katiba kwani dude CCM imekaba njia zote za haki na usawa.