Naomba mfano wa Taifa lililoshusha gharama ya maisha kwa kutumia Katiba?

Katiba nzuri ndio inayotupatia viongozi wazuri na katiba ya hovyo hutupatia viongozi wa hovyo

Viongozi ndio wanatakiwa kutatua changamoto zetu kama maji,uchumi, biashara, chakula, miundombinu n.k.

wakipatikana viongozi wa hovyo hayo yote yatakuwa ndoto kama ilivyo Sasa miaka 60 ya uhuru bado maji,elimu na chakula ni tatizo sana kwa nchi yenye ardhi kubwa na heti kilimo ndio UTI wa mgongo

Katiba nzuri ni Ile inatoa usawa kwa watu wote inawajibisha kwa usawa na hakuna aliye juu ya sheria.

Viongozi ndio wanapanga hatima ya mwananchi katika Kila jambo.
 
Inategemea unaposema miaka 60 unajilinganisha na nani maana nchi sio binadamu hata hivyo ukiangalia takwimu bila macho ya makengeza utajua Kuna hutua kubwa imepigwa japo htujafikia ubora tunaoutaka.

Katiba ni jambo moja na utendaji wa katiba ni jambo lingine kabisa najifunza sana Kwa jirani zetu Kenya pamoja na katiba nzuri sana lkn nadhani wanaongoza Kwa kuwa na viongozi wapigaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…