Naomba Mkopo wa TSh 20,000 – Nimekwama kwa Sasa

Naomba Mkopo wa TSh 20,000 – Nimekwama kwa Sasa

Status
Not open for further replies.
Mkuu Mawazo255 pole kwa unayoyapitia siko sehemu nzuri kuweza kutuma hiko kiasi cha hela ila ikiwa hautajali tafuta kituo chochote cha polisi ,omba kuonana na askari anayehusika na mahusiano ya jamii ,ukionana naye nakutumia namba PM ,unipigie nizungumze naye nimuombe akupe elfu thelathini kutoka kwenye mfuko wa jeshi la polisi upande wa mahusiano mema na jamii .

Ni haki yako mkuu wangu kusaidiwa nao na pia na mimi ni haki yangu kukuombea wakupe hela .

Ikiwa uko tayari tafadhali nijibu natuma nikupe namba yangu sasa .

Pole sana rafiki .
 
Naomba Mkopo wa TSh 20,000 – Nimekwama kwa Sasa

Habari wakuu wa JamiiForums.

Naomba kwa heshima kama kuna mdau mwenye uwezo wa kunikopesha TSh 20,000. Kwa sasa nimejikuta kwenye kipindi kigumu kifedha, na kiasi hicho kitanisaidia kuvuka changamoto ya dharura niliyonayo.

Ninaelewa si rahisi kumwamini mtu usiyemfahamu, ndiyo maana siombi kwa kulazimisha wala kwa kutunga hadithi za kuonea huruma. Naomba kwa uaminifu. Nikipata msaada, nitawasiliana vizuri na tutakubaliana namna na muda wa kurejesha fedha hizo.

Kama hutaweza kunikopesha, hakuna shida. Ushauri, kazi ya kufanya, au fursa yoyote ya kunisaidia kujikwamua pia nitapokea kwa shukrani.

Asanteni kwa kunisoma. Mungu awabariki na awazidishie pale mnapotoa kwa ajili ya wengine.
Njoo makunganya upige hela
 
Pole sana ndugu 20K fedha ndogo deni lake ni himilivu. Nina imani watu wema watakufuata PM kwa msaada.
Wengine wanatamani kukusaidia ila wanahofia usalama wao maana watekaji wa ccm wapo kazini.
si unaenda kwa wakala mtaa D unaacha pesa na number wakala asiekujua
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom