Naomba mnisaidie jinsi ya kupata mtaji, nimekwama sana

Naomba mnisaidie jinsi ya kupata mtaji, nimekwama sana

Tumia mbinu za kibepari ku acquare capital mkuu
(Fraud,robbery,Ponzi scheme et Al) Lasivyo utachakaa
Nipe mbinu kaka nimeangaika sana na haya maisha ni story ndefu mengi yapo moyoni nipe hata mbinu moja ya kutumia nitashukuru
 
Tengeneza business plan ya hiyo biashara yako kisha anza kutafuta wadau ili waweze kuwekeza kwenye hilo wazo lako. Nadhani hii ndio njia nzuri ya kurise capital.

Kama ukionesha clear path to profit katika pitch deck yako nadhani utapata watu wa kuwekeza kwenye hilo wazo lako, thou haitokua rahisi ila kwa nionavyo Mimi nadhani hiyo ndio sehemu nzuri ya kuanzia kwenye muktadha huo wa kurise capital.
Sawa shukrani, business plan nnayo ishu ni namuona mdau gani maana nimepigwa kama giza fulani sielewi elewi
 
Ndio maana nasisitiza sana vijana tununue ardhi, hasa hivi plot za miradi. Leo hii halmashauri na manispaa nyingi zina viwanja vya mradi ambavyo vipo hadi vya SQM 1 Tsh. 500, vijana tununue asset hizi udogoni.

Mambo hupinduka
Niliwai kuwa na kiwanja nilikiuza nifanye biashara, nikapata mitihani ikabidi nipambanie afya kwanza so hela yote iliisha japo umeongea ushauri mzuri sana sikupingi.
 
Kama mda unakutosha utatakiwa uwe na kazi ya ziada nyingne ama ukiwa unapga kibarua hapo tafta kibarua cha juu zaidi.

  • Au jibanebane kwa mda pesa ikae, na ufanye mradi au genge la mboga
  • au tembeza chai/alkasusu.

Onyo usipende kubadiri badili kazi mara kwa mara kwan na malengo hubadilika ama kufa.
Kuhusu muda ni hautoshi nafanya kazi ya shifts na ukifika kazini ni kazi mwanzo mwisho ukitoka hapo lazima upate muda wa kupumzika ili kesho yake uweze kufanya tena kazi.
 
Pole mkuu una familia?? Biashara unayoitaka ni lazima ianze na kiasi hicho tu?? Haiwezi kuanza na kiasi kidogo ukawa unakuza kidogo kidogo?
Ni biashara inayohusu mashine fulani ya kuinunua ndio pesa nyingi inaenda huko na ninaamini ni biashara inayoweza kuwa sustainable nikaifanya for the rest of my life
 
Ungefanya hivi ikiwa umesoma weka Elimu yako hapa .

Uanze na kubadilisha Kazi .

Na pia njia ya pili kwa sasa uandike wazo na kuonesha mchakato wa upatikanaji wa Faida na hasara upoje .

Then baada ya hapo MTU aweke hiyo 5M muwe mnagawana faida kwa kupitia asilimia .

Mfano kwakuwa wewe hauna mtaji unaweza kuwa unachukua 30% then mwenye mtaji 70%
 
Kwanza pole Kwa changamoto za kimaisha, lakini ongera Kwa mawazo chaja. Habari njema ni kwamba bado uja chelewa wewe bado kijana.

Kwenye maelezo yako unaitaji m5 za mtaji jibu ni ngumu sana kupata pesa hiyo Kwa haraka ukizingatia hauna asset, connection, Wala ujuzi wowote lakini unaweza kupata zaidi ya hiyo kama utaweka strategy na kuzisimamia ipasavyo.

Kwa Sasa tafuta angalau laki tatu au Tano inategemea na uwezo wako then tafuta biashara yoyote yenye mzunguko mkubwa kulingana na eneo ulipo(usifanye biashara ya msimu au inayo weka sana pesa). Zingatia hata bakharesa alianzia chini kijana.
Sawa nimekuelewa shukrani kwa ushauri wako.
 
Ungefanya hivi ikiwa umesoma weka Elimu yako hapa .

Uanze na kubadilisha Kazi .

Na pia njia ya pili kwa sasa uandike wazo na kuonesha mchakato wa upatikanaji wa Faida na hasara upoje .

Then baada ya hapo MTU aweke hiyo 5M muwe mnagawana faida kwa kupitia asilimia .

Mfano kwakuwa wewe hauna mtaji unaweza kuwa unachukua 30% then mwenye mtaji 70%
Sawa Dr nimekuelewa, andiko nnalo tayari ishu labda iliyobakia ni nalipeleka kwa nani hapo napo sijui pakuanzia
 
Sawa Dr nimekuelewa, andiko nnalo tayari ishu labda iliyobakia ni nalipeleka kwa nani hapo napo sijui pakuanzia
Mkuu Andiko lako lipandishe hapa JF na uelezee mchakato kwa style hii

SWOT
Strength
Weakens
Opportunity
Threat

Ili MTU ajue endapo akiweka hiyo 5M usalama wa pesa yake upoje na faida ipoje .

Then ni muhimu kuwa na permanent Address
 
Pole Mkuu, usikate tamaa na uko hai. Kwa Imani yako, Mungu hufanya njia pasipo na njia. Kama wengine walivyotangulia na ushauti mzuri, unaweza ukafatilia na ikasaidia.

Mimi naungana nao kwa yote, labda niongeze tu. Pale ambapo mtu unaona ndugu, marafiki hawapo au si wa kutoa msaada. Ni vizuri pia kuwa karibu na watu unapoabudia kwa Imani yako.

Hawa watu, kiongozi unaweza kumwambia na wakakuelewa wakakufanyia harambee. Pia naona watu wanakuwa kwenye vikundi vya aina tofauti. Mwenyezi Mungu akakutimizie yote uyaombayo.
 
Sasa kwanini huyo Mungu asimtimizie sasa hivi jamaa anakula msoto?
Ni Imani, kila kitu kina wakati wake. Hujawahi ona mtu anapitia shida kubwa sana, anakuja kuzivuka na inabaki historia? Mimi nimewaona wengi kwa macho yangu. Ukumbuke hachelewi wala hawai.
 
Back
Top Bottom