Naomba mnisaidie niweze kula vizuri🙏🏼🙏🏼

Naomba mnisaidie niweze kula vizuri🙏🏼🙏🏼

Valhalla

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2024
Posts
279
Reaction score
430
Habari wakuu.

Baada ya kugundua kuwa sina uwezo wa kujenga,kununua gari au kwenda mavacation nimeona nifurahie maisha kwa japo kula vizuri kama matajiri.Starehe na anasa yangu iwe kula vizuri.

Uwezo wa kula vizuri ninao ila siridhiki na vitu ninavyokula.Najikuta kila siku nakula vitu vile vile na sasa vimenikinai sivifurahii.Nisipokula ugali samaki au kuku nitakula ubwabwa samaki au nyama nazi njegere ni ndizi za kupika,chipsi,au viazi roast main roast,chapati supu au mchuzi na vingine vingine tu kama hivi vya kawaida.

Naomba nyie mnaojua mapishi/mnaokula vizuri mnipe menu ya vyakula viziuri vizuri vya kitanzania.Hata vya kikabila kama vinanoga nitajie.

Niko serious nishachoshwa na vitu ninavyokula na mara nyingi jioni nakula ubwabwa na mboga tofauti tofauti ila zote zishanikinai.Hapa ubwabwa na mchuzi wa sangara na njegere nazi unanisibiri ila sina hamu nao kabisa ila nina njaa na roho yangu inatamani kula kitu kingine mbali ya hivi🙏🏼🙏🏼

NB:Wapi kwa Tz naweza kupata Egusi seeds.
 
Back
Top Bottom