Naomba msaada mume wangu amekamatwa na polisi nyumbani saa nane usiku kwa tuhuma za kununua simu ya wizi. Vituo vyote wanadai hayupo na tusimtafute

KUNA MTU NINGEKUPA ILA NAITAJI KUMJUA HUYO ALIYEKAMATWA YUPOJE NA KAZI YAKE NO KUFICHA
 
Dah braza mm unanichanganya kwa kweli ila Mimi naamini nchi yangu bado ni Safi haijafikiwa huko kwenye mambo ya ushetani mkubwa hivyo ndio màana nasema huenda kuna watu pemben Wana mabifu Yao na mwangosi wakamtwanga risasi kisha wanasakizia serikali ili ionekane mbaya,sasa Kama akwilina alikuwa kwenye gari Nani atampiga risasi yeye aache wale WA kwenye maandamano yaani amlenge haswa target mtu aliyetulia kwenye gar aache wanaopiga kelele,unaweza kuwa alitaka apige juu kutuliza ghasia chuma ikaponyoka ikapita siko watu eeeeh kamuua akwilina hapo sasa mchaka mchaka WA maneno ndio unaanza kizazi na kizaz kurithishana roho mbaya za chuki.hivi bro wewe unakubal mtu aache kundi amlenge akwilina..aliyetulia kweli?

Kuna kundi linachafua linatumia vibaya mamlaka Yao na wanayoyafanya yanarudi kwa serikali kutupiwa lawama Kama hawa Askari wawili wamemteka Bwana Omary na sasa unasema serikali nzima.

Sema serikali tatzo haishughlikii IPASAVYO hawa watu wapuuzi ili isiwachafue yaani ingekuwa inawashughlikia isingekuwa na doa ingekuwa myeupe Kama tishu
 
Siku hizi Polisi.hawafati PGO?

Kwa nini.ubinadamu unawatoka?

Yaani simu tu ndio hivyo?

Mbona mafisadi wanatamba?
 
Taarifa pia zimechelewa.....mwizi anatakiwa Apigiwe mayowee muda huo huo anakosa ujasiri.

Huenda wasiojulikana wamerudi tena.
 
Kama serikali haihusiki na mauaji ya watu holela mpaka leo tungeshawafahamu waliompiga risasi Tundu Lisu. Pia hata Ben Saanane tungeshajua hatima yake.

Ndugu yangu, tunaposema serikali hatumaanishi vitengo vyote. bali ushiriki wa wenye mamlaka na wenye uwezo wa kukomesha haya matukio.
 
kwahiyo una maanisha polisi wanaruhusiwa kuchukua sheria mkononi? au basi na hao ndugu wakaloge aliempoteza ndugu yao waridhike au tumia medula mkuu.
 
nchi hii huyo binti amtafute baba keagan hao wengine wote wanaogopana bashite ana vinasaba vya magufuli.
 
KILE KITUO UNAWEZA KUWEKWA NA UKATAFUTWA KOTE USIJULIKANE WAANZIE HAPO TENA KWA BUSARA
Busara unamaanisha waanze vipi kaka,..wameambiwa HAPA HAKUNA KESI KAMA HIYO NA MSIJE TENA KUULIZIA...wanashindwa hata waende wakaanze vipi na wanajua hapa ndio ndugu Yao yupo...ila mbona Kama hawa wenzetu wanatunyanyasa sana aisee kwani si wanyooshe tu maelezo na watu wamuone ndugu Yao akipandishwq mahakamani? Si ndio sheria itakavyo au wanatengeneza njia za kupata kupga pesa huku nyumban mtoto na mke wanateseka sana.HAKI IKO WAPI?
 
MUONE MALISA GJ YULE WA CHADEMA FACEBOOK KESHO SIO MBALI TU MTAPATA MAJIBU
 
MUONE MALISA GJ YULE WA CHADEMA FACEBOOK KESHO SIO MBALI TU MTAPATA MAJIBU
Atatoa msaada mkuu kama unavyosema au ataleta mambo ya uchama kwenye matatizo halisi ya Mtanzania huyu aliyemuacha mke na mtoto wanateseka kwenye nyumba ya kupanga?hapa sina kitu na Nina familia lakini nawawazia wao

Imagine ni ndugu yako ndio amefanyiwa hivyo ungejisikiaje mkuu?
 
HUYU ANA NGUVU KUBWA YA KUSIKILIZWA KUPAZA SAUTI .KUNA WATU HATA NENO MOJA KWAO NI TISHIO KWA SERIKALI
 

Ndio unajidanganya?? Kuwa mpole mkuu Watu wanapotezwa na katiba ni karatasi.
 
Jumanne Sajin, naibu waziri wa mambo ya ndani ameshasoma ujumbe huu.
Kuwa mvumilivu, linafanyiwa kazi
 
Sawa hata kama ni mwizi sheria zipo wazi , ijulikane yupo kituo gani na apewe haki zake za msingi kama dhamana au kama dhamana haitolewi kwa sababu za kiuchunguzi pia liwekwe wazi , kumficha mtu na kutowajulisha ndugu hapo ni uvunjifu wa haki na sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…