Naomba msaada wa mawazo

Naomba msaada wa mawazo

Apo umatakiwa unadownload salary slip au ukaombe bank statement utajua tu pesa zilipo kwenda ndio utaenda kuuliza huko
 
Kufungwa hakupo hata siku moja midhali kithibitisho cha mkataba kwa njia ya kujaza fomu za kuomba mkopo kipo.

Kibubwa nenda Bank, hasa uliyoanza kuomba mkopo na wakamissbehave wenyewe na kukuletea kiwango cha chini ambacho haujaomba!

Ninadhani hao ndiyo chanzo cha tatizo hili.

Ukienda wataangalia mfumo mzima wapi kulipotokea tatizo na watarekebisha.

Mkopo wa aina yoyote hauwezi kukomba mshahara mzima bila kubakisha 2/3 ya take home kama masharti ya mikataba ya mikopo ya wafanyakazi inavyotaka.

Kama itaonekana ulizidisha kiwango cha kukopa kwa kujua ama kutokujua basi mtabagain nao ili ngapi wakuachie ya kurudi nayo nyubani kuhemelea watoto.

Lazima watakurekebishia makato, hawawezi ng'ang'ania kukata mshahara mzima, sheria haiwaruhusu kufanya hivyo.

Majibu unayohitaji mleta mada yapo katika post hii...
 
Mkuu, wewe ni mwalimu? Mimi pia ni mwalimu na sina nia mbaya kuuliza hili swali.

➡️➡️➡️ Yaani ulipokuta hela zimeingia, japo kidogo kuliko mkopo ulioomba, we ukaanza kuzitwanga ulifikiri zimetoka wapi? Na ukaenda tena kukopa benki ya pili dah! Nenda kwenye benki zote mbili ukawaambie ukweli. Naamini watakusaidia.

Elimu ya pesa, japo kwa yale mambo ya msingi, inahitajika sana. Pole!
Walimu wameingiaje hapo msukuma lakini!!

Sema Aalitakiwa asitumie hizo pesa tofauti na kiwango alichoomba yani kakuta tofauti ye nae bila kuhoji kazifakamia tu !

Ile bank ya mwanzo watakua wanakata hizo pesa zao ndogo walizomuingizia kabla hawajacancel

Na hio benki ya pili nayo wanakata chao hapo lazima aisome namba!

Pole yake sana asee

Cc Smart911
 
Mimi ni mtumishi wa umma mwandamizi lakini jambo hili limenipita pembeni na nahisi nimeingia kwenye tatizo kuubwa.

Niliomba mkopo bank kwa kutumia mfumo wa utumishi. Kabla mfumo haujapitisha mkopo bank wakawa wameshaniwekea kiasi Fulani Cha pesa. Sikujua kama ndo ulikua mkopo wangu au la. Nilikuja kushituka baada ya kufanya withdrawal na balance kuwa ndogo kuliko mkopo nilioomba.

Nikawapigia bank hawakunipa ushirikiano. Nikarudi kwenye mfumo wa utumishi nikakuta mkopo umekuwa cancelled. Nikajaribu kuomba tena kwa bank nyingine ikakubali mpaka hatua ya mwisho na pesa nikazitumia. Zote za bank ya kwanza na ya pili.

Tatizo limekuja sasa. Kila mshara ukiingia nakuta balance ni 0. Na bank ile ya mwanzo wanataka niende kuboresha taarifa za akaunti yangu

Nahisi watanifunga. Ila pia sina mshara mwezi wa pili sasa..Hali ngumu. NIENDE AU NIJIKAZE MPAKA PESA YAO WAIRUDISHE KWA KUNIKATALIA MSHAHARA
MREJESHO: Nimeenda bank ya kwanza..wameniomba radhi kwa kuzuia mshahara wangu. Wamekubali kuwa mfumo ndio ulileta tatizo kitaifa. Wamenionba twende kwa HR ili tukubaliane makato nje ya mfumo. Pia wamekubali kuniekea kiasi cha mkopo walichonipunja

Nawashukuru wanajamii kwa msaada wenu. Nimegundua kuwa jukwaa hili ni muhimu sana. Nilikuwa positive kwa Kila maoni na mawazo na kusema kweli yamenisaidia. Walionibeza pia nawashukuru. Nawaombea wasije kupata changamoto. Hela nilikula ndio but bank wameelewa na kukili kuwa hawakufanyia kazi taarifa niliyowapa kwa wakati na isingewezekana kurudia maombi ya mkopo kwenye bank Yao.

AKSANTENI JAMANI
 
Salary slip iko poa kivipi?

Kinachosoma kwenye salary slip unamaanisha ni tofauti na kinachotakiwa benki?
Nimeenda na nimeandika MREJESHO hapo juu.. nashukuru mkuu kwa mawazo yako muhim
Walimu wameingiaje hapo msukuma lakini!!

Sema Aalitakiwa asitumie hizo pesa tofauti na kiwango alichoomba yani kakuta tofauti ye nae bila kuhoji kazifakamia tu !

Ile bank ya mwanzo watakua wanakata hizo pesa zao ndogo walizomuingizia kabla hawajacancel

Na hio benki ya pili nayo wanakata chao hapo lazima aisome namba!

Pole yake sana asee

Cc Smart911
Bank wameelewa. Kwanza wao ndo wamekubali makosa kwa maana niliwataarifu ila hawakuzingatia.. Asante kwa mawazo mazur hata hivyo
 
Kawashitaki maan wamekukata zaid ya 1/3 ya mshahara wako , wew huna makosa , makosa either ni ya mfumo
 
Mkuu, wewe ni mwalimu? Mimi pia ni mwalimu na sina nia mbaya kuuliza hili swali.

➡️➡️➡️ Yaani ulipokuta hela zimeingia, japo kidogo kuliko mkopo ulioomba, we ukaanza kuzitwanga ulifikiri zimetoka wapi? Na ukaenda tena kukopa benki ya pili dah! Nenda kwenye benki zote mbili ukawaambie ukweli. Naamini watakusaidia.

Elimu ya pesa, japo kwa yale mambo ya msingi, inahitajika sana. Pole!
Alidhani mkopo ni sadaka.

Mkopo siyo sadaka kamwe. Mkopo ni Deni.
 
Kawashitaki maan wamekukata zaid ya 1/3 ya mshahara wako , wew huna makosa , makosa either ni ya mfumo
Kesi tena mkuu..wamenirudishia mshahara wangu wa miez miwili tayari.. hakuna haja ya kesi tena
 
Back
Top Bottom