Ms R
JF-Expert Member
- Jan 19, 2023
- 8,853
- 19,587
Kwa nadra sana aseeeeMbona kila mara huwa ninafanya hivyo ms r
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa nadra sana aseeeeMbona kila mara huwa ninafanya hivyo ms r
Naona maneno mengi yanayotajwa na wadau ni yale yanayoangukia katika sayansi na teknolojia. Haya kupata tafsiri ya moja kwa moja ni vigumu ndiyo maana mara nyingi inabidi yatoholewe kama yalivyo. Hata lugha zingine zimepitia shida hiyo na siyo Kiswahili pekee. Kiingereza, kwa mfano, kimechukua maneno mengi katika tanzu hizi kutoka katika Kilatini na Kigiriki (cha kale); na kuyakopa kama yalivyo. Ndiyo maana misamiati kama ya kwenye taaluma za udaktari na uhandisi, kwa mfano, ni migumu kweli kweli. Ingependeza kama mjadala ungejikita katika maneno ya kawaida; na yanayotumiwa na watu wa kawaida mtaani katika mazingira yasiyo rasmi (mf. Katika elimu)
Kwa hapa Tanzania BAKITA ndiyo wenye jukumu la kuunda hizi istilali za maneno mapya katika Kiswahili na huchapisha vitini au vikamusi mara kwa mara katika tanzu mbalimbali zikiwemo zile za sayansi na teknolojia. Tatizo hata hivyo ni kwamba lugha ni mali ya wanajamii; na jamii ndiyo huamua neno gani litumike. Ni kwa sababu hii misamiati mingi inayopendekezwa na BAKITA wamebaki nayo huko huko BAKITA makabatini kwao wakati mtaani jamii inatumia maneno inayotaka. Na hakuna juhudi zo zote za makusudi hata katika mazingira rasmi (mf. kwenye vyombo vya habari na mashuleni) kuhakikisha kuwa maneno rasmi yaliyopendekezwa na BAKITA yanatumika ili yazoeleke. BAKITA, kwa mfano, walipendekeza kompyuta iitwe tarakilishi (mashine yenye akili na yenye uwezo wa kukokotoa tarakimu) lakini mtaani neno kompyuta limeshika na BAKITA hawana la kufanya maana lugha ni mali ya jamii. Baobonye - keyboard, ugiligili - liquid...n.k.
Kuhusu utohoaji wa maneno BAKITA huzingatia misingi kadhaa; na hawatafsiri tu kiholela.
1. Huangalia katika lahaja zingine za Kiswahili kama wanaweza kupata neno linaloshabihiana kimaana/kidhana na neno jipya. Lipo dai kwamba Kiswahili ni lugha tajiri sana na hakukuwa na sababu ya kukopa maneno mengi kutoka katika Kiarabu (na Kiingereza) kwa sababu karibu kila neno la mkopo linaweza kupatiwa tafsiri yenye asili ya Kibantu kama tungechimbua kwenye lahaja zingine za Kiswahili hasa zile za muda mrefu mf. Kimvita. Hawa huwa wanahoji ni kwa nini lahaja ya Kiunguja iliteuliwa kuwa lahaja teule wakati ni lahaja ambayo tayari ilikuwa "imeshaharibiwa" sana na Kiarabu. Kama lahaja za kale kama Kimvita zingeteuliwa kuwa msingi wa usanifishaji, Kiswahili cha sasa kisingekuwa na maneno mengi ya Kiarabu, maneno ambayo mengi yamekopwa na kusanifishwa bila sababu za msingi maana kuna maneno shabihi katika lahaja zingine za Kiswahili. Pengine kulikuwa na njama za makusudi "kukiharibu" Kiswahili kwa "kukiarabisha" na "kukiingerezesha". Kumbuka kwamba mchakato wa kukisanifisha Kiswahili ulisimamiwa na Waingereza!😳
2. Tukikosa neno katika lahaja za Kiswahili basi tuangalie katika lugha zingine za Kibantu. Hapa ndiyo tunapata maneno kama ikulu (Kinyamwezi), shiganga (Boulder-Kisukuma) n.k.
3. Tukikosa katika lugha za Kibantu basi tuangalie katika lugha zingine za Kiafrika ambazo si za Kibantu
4. Wakati mwingine inabidi kuangalia dhana ya kitu tunachojaribu kutohoa (mfano wa kompyuta hapo juu - tarakilishi - mashine yenye akili inayokokotoa tarakimu).
5. Kutohoa maneno kama yalivyo. Hii ndiyo njia inayopendwa na jamii na tayari maneno mengi yameshazoeleka kama yalivyo (bicycle - baisikeli, radio - redio, helicopter-helikopita). BAKITA hujaribu kupendekeza maneno mapya lakini jamii inakuwa imeshatohoa moja kwa moja maneno na mapendekezo yao mengi huwa hayashiki.
Pia kuna hatua zingine za kuzingatia katika utohoaji wa maneno mbali na huu mwongozo wa jumla wa ukopaji wa maneno.
Kiswahili ni lugha inayokua na itaendelea kukopa hasa katika hii misamiati ya kisayansi na kiteknolojia. Hili ni jambo la kawaida maana lugha zote zimepita huko. Japo tuna BAKITA lakini mwamuzi hasa wa lugha ni jamii yenyewe.
View attachment 3028238
Halafu ufaidike nini sasa kwa kutajiwa hayo maneno?Kwa muda mrefu sana nimekuwa napata wakati mgumu ninapoona baadhi ya maneno ya Kingereza haswa katika Technology au professional fulani kukosa tafsiri rasmi. Hapa neno "tafsiri" nina maana ya translation. Mfano maneno kama, excavator katika context ya machinery au equipment; hearse katika context ya vehicle; au digital katika context ya technology.
Kwa maneno yenye tafsiri rasmi, nimekuwa najiuliza zinapatikanaje na mchango wa jamii ni kiasi gani. Mfano mdogo tu, dunia ilipoanza kutumia email kama njia ya mawasiliano, ilinichukua muda mrefu kujua tafsiri yake ni barua pepe. Pia nafikiri tafsiri rasmi ya Artificial Intelligence au AI, ni "Akili Mnemba." Kwa mara nyingine tena swali langu ni je, hizo tafsiri rasmi zimepatikanaje? Wananchi walihusishwa kwa kiasi gani?
Mfano mwingine ambao umenipa maswali mengi hivi karibuni ni wakati nasikiliza taarifa ya Habari ya saa mbili usiku kutoka redio moja maarufu, (bila kuitaja jina) hapa nchini. Katika kuwasilisha Habari kuhusu taifa fulani kugomea mkutano wa UN kwasababu nchi hiyo imewekwa kwenye "Blacklist", mtangazaiji alisema, (sio nukuu ya moja kwa moja), "Nchi X ilitoka nje ya mkutano kwasababu imewekwa kwenye listi nyeusi." Baada ya kusikia hivyo nikajiuliza, Je katika muktadha huo, kusema "Listi nyeusi" ndio tafsiri rasmi ya "Blacklist?"
Baada ya kusikia hivyo, ikaamsha tena chachu yangu ya kujua tunapataje tafsiri rasmi ya maneno magumu ya Kingereza na, ni jinsi gani wananchi wanaweza kujumuika katika kutatua changamoto hiyo.
Baada ya kusema hayo machache, swali langu kwako ni, je, unafikiri lugha yetu ya Kiswahili ina changamoto hiyo? Au wewe binafsi umeshawahi kukumbana nayo katika masomo yako, au kazi zako za kila siku? Kama jibu ni ndiyo, naomba neno moja tu la Kingereza ambalo unafikiri halina tafsiri rasmi. Kwa kufurahisha mjadala huu, ukiweza, pendekeza tafsiri ambayo wewe unafikiri itafaa kwa neno ulilopendekeza.
Kwanini nimeleta ombi hili kwenu? Nia kubwa iliyonifanya nilete ombi hili kwenu ni kwasababu, kwanza binafsi nafikiri hii changamoto ipo. Pili, nafikiri ingekuwa vema kama wananchi nao wangejumuishwa katika utafutaji wa tafsiri rasmi ya menono magumu au mapya ya Kingereza. Tatu, kwa kushirikisha jamii, watajiona nao ni sehemu katika kukuza Kiswahili.
Kwa kumalizia, nimepata muarobaini wa changamoto hii. Muda si mrefu, nataka niweke platform ambayo itakuwa rafiki kwa jamii nzima. Itajumuisha jamii yote ndani na nje ya nchi kwa ujumla katika kukabiliana na changamoto hii. Itasaidia kufanya watu wafikiri na kupanua mawazo.
Ndani ya siku 7, nitawajulisha jina la platform.
Nashukuru sana. Karibuni sote tujiunge kukuza Kiswahili.
Powa powaHii itakuwa kali. Sina uhakika kama kuna tafsiri rasmi lakini natamani kuona mapendekezo ya jamii yatakuwaje.
It will be fun!
FreshNashukuru sana kwa mchango wako. Nafurahi kwasababu naona umeelewa nini nataka jamii ishiriki.
Bluetooth= meno ya udhurungi.Mmh! Umeandika parefu sana mkuu!
Anza na hili BLUETOOTH.
Bluetooth= meno ya udhurungi.
XS§ABkA¿SOCATbhrT¿bTrrF¡VoCAZSW§a§AtCSISÑ@ÆIkOkAZiKUCY¡?SMkekgQSAFQCW§AFQCARÑiCÑKiSAVSÄKWoSgQCC¡?SEkAD2Ø'E¡VoKÑsKA&Ubaradhulishaji majumui au ubaradhulishaji wa kimajumui
Hii inayo kiswahili ni "Asante kwa huu uzi"Thanks for this thread.
Lugha iliyoanzishwa kwa kukopa misamiati na lugha nyingineKiswahili ni lugha ya kuunga unga sana sijui kwanini tunaikumbatia
TechnologyKwa muda mrefu sana nimekuwa napata wakati mgumu ninapoona baadhi ya maneno ya Kingereza haswa katika Technology au professional fulani kukosa tafsiri rasmi. Hapa neno "tafsiri" nina maana ya translation. Mfano maneno kama, excavator katika context ya machinery au equipment; hearse katika context ya vehicle; au digital katika context ya technology.