Naomba neno moja tu la Kingereza ambalo halina tafsiri rasmi ya Kiswahili

Nashukuru kwa mchango wako. Je unaweza kusema "Orodha nyeusi" ndio tafsiri rasmi ya "Blacklist?" katika muktadha wa "Mwenye/wenye sifa mbaya iliyopitiliza?"
Hapana! Orodha nyeusi Si tafsiri sahihi ya neno blacklist. Tafsiri sahihi inapaswa kuwa ' orodha ya nchi korofi/ kaidi'.
 
Kwanini iwe "waya janja" na isiwe "waya hewa"?

Mchango mzuri.

Nimejibu jinsi nilivyofikia pendekezo langu. Naomba na wewe utuambie umefikiaje kwenye pendekezo lako la "waya hewa."

Mjadala unazidi kunoga. Tuendelee.
 
Hapana! Orodha nyeusi Si tafsiri sahihi ya neno blacklist. Tafsiri sahihi inapaswa kuwa ' orodha ya nchi korofi/ kaidi'.

"Blacklist" ni general word. Mtumiaji ndio anaweka muktadha au context. Kwa hiyo tafsiri rasmi ni ipi?
 
Phisics, kemia😂😂, geo, cjauvinism, cocastic, bambustic, fantastic, radio, bulb, bamboo, dance floor, lip sync, melanin, platelets, madamu, skimming, scanning, saini, gonolea, overloading, siesta, /, ni mengi aisee🥱
 
Mkuu unafanya utafiti hapo time ya Kiswahili, ?

Hapana ndugu. Kama nilivyosema mwanzo, nafikiri kuna haja ya kuwashirikisha wananchi au watumiaji wa lugha ya Kiswahili katika kutafuta au kuikuza lugha yetu. Sehemu yangu mimi baada ya kuona hii changamoto, nimeamua kuja na platform ambayo itatoa fursa hiyo kwa jamii. Kwa hiyo nataka kujua kama hiyo changamoto ipo kweli au ni mimi binafsi ndio nimepitwa na wakati.
 
Napendekeza bluetooth iitwe jongeohewa. Mfano wa sentensi Nirushie huu wimbo kwa jongeohewa

Umefikiaje hilo pendekezo lako la "Jongeohewa?" Je kuna kilugha hapo? Hebu tupe ufafanuzi kidogo ili umma uelimike.

Lina uhalisia wa Kibantu.

Asante.
 
Kiswahili hakikutakiwa kitumike kabisa

Moja ya utambulisho wa jamii fulani ni lugha yao. Kwasababu tuna msingi tayari, tuanzie hapo kukikuza zaidi.

Usikate tamaa
 
Serendipity
"Serendipity" ni neno la Kiingereza linalomaanisha ugunduzi wa mambo mazuri kwa bahati au kwa nasibu, hasa mambo ambayo hayakutarajiwa au kutafutwa. Hali hii inapotokea, mtu anapata kitu kizuri bila kuwa amekikusudia au kukitafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…