Naomba Nijuzwe kama ni kweli kuna Wamarekani weusi wanahamia TZ kwa wingi

Naomba Nijuzwe kama ni kweli kuna Wamarekani weusi wanahamia TZ kwa wingi

Yes I agree with you, nigga msikie tu , hutaweza kumwelewa mpaka uishi nae sio watu hao
Exactly we are so rude,naught in nature but all that shits caused by cruelty which has been done for black community,at Tanzania we could say we feel safe guarded well.
 
Baada ya kuona post yako Duksi , imebidi niangalie baadhi ya video mbalimbali youtube kuhusiana na mada tajwa hapo. Nami nikaamua kusumaraizi na kuongezea kidogo.
Hao wamarekani weusi wamejaa wengi sana tena wengine wamepanga mpaka uswahilini. Nimeangalia na nimefanikiwa kujua sababu kadha wa kadha zinazowafanya wamiminike bongo ikiwemo;
i). Ubaguzi ama police brutality huko Marekani kama ulivyosema.
Hapa kuna mzee anasimulia jinsi yeye na mtoto wake (kijana). Alikuwa anahadithia jinsi walivyokamatwa na polisi wa usalama barabarani na kuamriwa kwenda kituoni maana kuna msala walifanya kuwaudhi askari wetu wa usalama (hakutaja ni nini). Walichoshangaa ni pale waliporuhusiwa kuendesha gari wenyewe mpaka kituoni wakati huko kwao wangeoneshewa bastola na pingu juu huku ukiwa na hofu ya kuawa.

ii) Uponyaji wa kiimani (spiritual healing). hapa wengi ni wale wanaopenda mazingira ama nature.
iii) Bongo hamna mambo ya lock down
iv) Urahisi wa maisha. Mtu anapanga mansion kwa dola mpaka 800 wanaona ajabu sana wakati kwao kwa dola 2000 kupata tu nyumba ya kawaida ngumu sana labda upate kachumba tu wenyewe wanaita studio yaani ka ghetto ka kizushi.
v) Bongo kuna beach nzuri sana clear water haswa Zanzibar
vi) Kuna machaguo mengi ya sehemu za kukaa kwa kuzingatia hali ya hewa unayopenda mfano; wanaopenda baridi wanakaa Arusha na wanaopenda mjini wanakaa Dar kwa sababu ya malls ni nyingi na urahisi wa kupata kila unachohitaji
vii) Hii nchi ina amani sana na imetulia
viii) Vivutio vya kitalii ni vingi sana kuanzia Serengeti, mlima Kilimanjaro n.k

Licha ya kufurahi maisha yao hapa bongo na kusema sisi bongo ni wakarimu sana kwa kila mtu, baadhi wamekutana na tamaduni ambazo hawajazoea (culture shock) kwa mfano;
i) Suala la mavazi, waliozoea kuvaa vimini wanapata tabu sana
ii) Too much stare. Hahahaha... imenibidi nicheke kidogo. wabongo tunakodolea sana macho watu, ukipita mtu anakushangaa kama kaona sanamu, wanaona sio kawaida shangaa yetu ya kiajabu.
iii) Bongo ni ngumu sana kupata rafiki wa uhakika sababu wengi wanakuwa rafiki kwa sababu wanaona kama sehemu ya kitonga kupiga pesa za hapa na pale.
iv) wabongo tuko slow sana kwenye suala customer care, kila kitu ni pole pole tu

Pia matamanio yao makubwa kwa bongo ni wao kuweza kupata ardhi na kumiliki kama mzawa bila kupitia TIC (shirika la uwekezaji TZ). wao wanaamini wamerudi motherland sasa kitu kama hiki wanahisi hakijakaa sawa kinawabagua kimtindo. Wengine mpaka wameamua kuolewa na wabongo na sasa wameamua na kujenga nyumba za ndoto zao.
Hawa wamarekani weusi wanazidi kujaa si tu bongo bali Afrika haswa nchi ya Ghana, Gambia, Tanzania, Rwanda n.k na nchi ambayo ina mazingira mazuri sana kwao ni Ghana kwa sababu kule ilianzishwa kampeni mwaka 2019 inaitwa "A year of return" ilikuwa kwamba raisi Akufo Ado(serikali) inawapatia pasipoti ya Ghana, ardhi yako binafsi kwa ajili ya kujenga makazi yako n.k cha kushangaza bongo sio rahisi kama huko Ghana lakini wanajaa na wanaitana wengi sana.
Binafsi ningependa wajichanganye zaidi na wazawa na wawekeze katika maeneo mbalimbali kwani naamini kuishi kwao dunia ya kwanza watakuwa na exposure na ujuzi wa hali ya juu katika kuongezea uthamani kwa kuboresha uwekezaji wa kisasa nchini wasiishie kuwa youtubers tu, labda serikali ikiona mchango chanya toka kwao itaweza kuwapa kastatus fulani.
Iwapo wangepata opportunity kama waliyoipata ghana,Tanzania ingejaa aise,maana pamoja na changamoto ya visa na umilikaji wa ardhi lakini bado wametokea kupapenda Tanzania,nilisikia wameunda community yao na wanafanya vikao na serikali ili waruhusiwe baadhi ya vitu
 
Nimesikia kuna Wamarekani weusi wanahamia TZ kwa wingi kwa sababu wanakimbia kuchanjwa kinga ya corona.

Pia sababu nyingine ni kuipenda TZ kwa sababu ya JPM walivyokuwa wanamhusudu.
Na ubaguzi wote wanaofanyiwa Huko USA,hakuna Negro yoyote ambaye anaweza kukubali kurudi Afrika achukue uraia wa nchi kama Taz,Kenya,nk,wengi wao wanakuja kama utalii tu kama wezao weupe,lakini hakuna anayeweza kuitupa passport ya USA achukue ya kibongo,
 
Iwapo wangepata opportunity kama waliyoipata ghana,Tanzania ingejaa aise,maana pamoja na changamoto ya visa na umilikaji wa ardhi lakini bado wametokea kupapenda Tanzania,nilisikia wameunda community yao na wanafanya vikao na serikali ili waruhusiwe baadhi ya vitu
TZ ni kama nguvu ya sumaku, wengine wanakuja kwa ajili ya kutembea tu lakini wakishafika wanapapenda na kulowea kabisa.

Nimeona kweli wana community zao hapa bongo ila sifahamu kama wanamazungumzo na serikali. Ila ni kitu poa kama wanafanya hivyo.

Kuhusu suala la ardhi, ingekuwa favours kama za Ghana kweli wangejaa sana. Ila sisi tuko so protective kwenye suala la rasilimali ardhi na urai pacha, kwa hiyo kwa hapa, sidhani kama watapata kitu zaidi ya kuendelea na utaratibu uliopo wa kukodi ardhi kupitia shirika la uwekezaji.
 
Kwanza huna adabu, tatizo watanzania tunataka kupata utajiri kwa haraka. Tunataka tuwaibie ndio maana tunawapenda wazungu. Na hao wazanzibar unawasema wewe wanawapenda wazungu hasa wakike ili wapate vitonga.

Black Americans hapa ni kwao ni muda sasa wa kuwawekea mazingira ya kurejea na kuja tujenge uchumi wa nchi.
Vipi wakenya hapa sio kwao? Wote si weusi? Au weusi wakutola Marekank tu ndo hapa ni kwao?
 
TZ ni kama nguvu ya sumaku, wengine wanakuja kwa ajili ya kutembea tu lakini wakishafika wanapapenda na kulowea kabisa.

Nimeona kweli wana community zao hapa bongo ila sifahamu kama wanamazungumzo na serikali. Ila ni kitu poa kama wanafanya hivyo.

Kuhusu suala la ardhi, ingekuwa favours kama za Ghana kweli wangejaa sana. Ila sisi tuko so protective kwenye suala la rasilimali ardhi na urai pacha, kwa hiyo kwa hapa, sidhani kama watapata kitu zaidi ya kuendelea na utaratibu uliopo wa kukodi ardhi kupitia shirika la uwekezaji.

watu hawaamini ila ndio ukweli unashangaza sana.

juzi naongea na jamaa mmoja anafanya kazi ubarozi,anakwambia hakuna kitu kigumu kama afisa wa ubarozi humo kuambiwa anatakiwa aondoke nyumbani muda umekwisha,huwa wanalia sana.
miaka ya nyuma alidhani ni sababu ya mazoea,ila hali imeanza kuwa inamshangaza maana hata wale walioinyesha kupakataa baada ya kuingia tu,hali hugeuka hivi siku ikifika.
 
TZ ni kama nguvu ya sumaku, wengine wanakuja kwa ajili ya kutembea tu lakini wakishafika wanapapenda na kulowea kabisa.

Nimeona kweli wana community zao hapa bongo ila sifahamu kama wanamazungumzo na serikali. Ila ni kitu poa kama wanafanya hivyo.

Kuhusu suala la ardhi, ingekuwa favours kama za Ghana kweli wangejaa sana. Ila sisi tuko so protective kwenye suala la rasilimali ardhi na urai pacha, kwa hiyo kwa hapa, sidhani kama watapata kitu zaidi ya kuendelea na utaratibu uliopo wa kukodi ardhi kupitia shirika la uwekezaji.
Wakipewa ardhi tumekwisha,tuilinde ardhi yetu kwa ajili ya akina junior wetu miaka ya mbele huko wasije kutawaliwa na mkoloni mweusi
 
Nimesikia kuna Wamarekani weusi wanahamia TZ kwa wingi kwa sababu wanakimbia kuchanjwa kinga ya corona.

Pia sababu nyingine ni kuipenda TZ kwa sababu ya JPM walivyokuwa wanamhusudu.
Ukiona hao mnaowaita black American wanakaa kuanzia mbezi beach mpaka uko Ununio jua kuna tatizo kubwa.
 
Ni kweli wapo wengi sana hapa bongo miaka mitatu nyuma naelekea bagamoyo nilipanda nao daladala walikua wanatokea Chi town{Chicago} tuliongea mengi wako poa kimtindo.
 
Nimesikia kuna Wamarekani weusi wanahamia TZ kwa wingi kwa sababu wanakimbia kuchanjwa kinga ya corona.

Pia sababu nyingine ni kuipenda TZ kwa sababu ya JPM walivyokuwa wanamhusudu.
Youtube wapo..na wanafanya vlogging..kuna mmoja aliliripoti vizuri sana msafara wa mazishi ya Magu
 
Wakipewa ardhi tumekwisha,tuilinde ardhi yetu kwa ajili ya akina junior wetu miaka ya mbele huko wasije kutawaliwa na mkoloni mweusi
Suala la ardhi bongo ni kama kitovu cha nchi kwa hiyo tunaulazima wa kuilinda. Binafsi sina neno tukiwanyima kumiliki kama wazawa. Hata hivyo, nashauri tuweke mbadala japo kwa wale ambao walikuwa watanzania lakini kutokana na shughuli za mihangaiko ya utafutaji wakajikuta wapo nchi za watu na kuchukua urai huko, japo hawa tuwape ardhi wawe huru kuwekeza watakavyo maana wengine inawabidi watumie ndugu wa karibu kujiwekeza.
 
Ukiona hao mnaowaita black American wanakaa kuanzia mbezi beach mpaka uko Ununio jua kuna tatizo kubwa.
Tatizo liko wapi boss? Kama sisi tumeshindwa kuweka mipango miji ya kueleweka kosa ni la kwetu, huwezi kulazimisha mtu akae uswazi ambapo jengo likishika moto hata zimamoto lishindwe kufika huko. Haiwezekani mtu alazimishwe kukaa sehemu ya hovyo kisa uzalendo.

Kiufupi hii Dar inatakiwa ipangwe upya ipangike, jiji limekaa kiwakiwaki sana.

Hapo suluhisho ni kuvunja uswazi zote jijini, unapandisha apartments wale waliovunjiwa unawapa kipaumbele cha kwanza kupewa vyumba.
Tukishindwa hilo basi tuipime ardhi ya nchi nzima kuzuia kilicho tokea huku Dar kusambaa nchi nzima miaka ijayo.
 
Unabidi ujiulize kwanini anaenda kuishi pembeni ya mji wengi wanakuwa Scammers kama sio mapopo sifa moja kubwa ya mpopo hakwambie origin yake ata siku moja and by the way wamepata fursa sana za kwenda state kwaiyo nirahisi kujifanya black American.Mbezi beach kuna nyumba mpaka leo iko isolated inamnara mmoja mkubwa balaa jamaa anapotea na kurudi ghafla anajifungia tu tusiwachukulie poa sana wengine wako kwenye special tasks. Talking from experience wachache sana wanakuja Tanzania wakijua wamefata nini wengi tunakutana nao hawajua wanachotaka mara akwambie nataka kuingia kwenye real estate mara mining na ndugu yangu anaweza invest ni kama wanakuja kutafuta fursa nao uku.
 
Umesikianwapi na tupatie records japo kwa mwezi wamekuja wangapi.
 
Kwenye huu uzi kila mtu nasikia ...nasikia, niliambiwa... YouTube....
 
Back
Top Bottom