Mbowe huwa anasema tatizo ni mfumo nafikiri tumejionea, tudai katiba mpya🤣
Tukirudi kwenye maada, huo mfumo utakuwa unatatizo kwenye sehemu inayotuma email (mailing system) inawezekana wametuma email nyingi na quota (bando) walilokuwa nalo limeshakwisha, au email zao zinaingia kwenye spam folder kutokana na sababu mbali mbali za kiufundi.
Jaribu kuangalia kwanza kwenye spam mail uone kama kuna email yoyote umetumiwa, kama ipo fuata maelekezo yake, ikigoma itakuwa ime-expire.
Jaribu kwenda kwenye sehemu inasema forgot password, weka email uliyojisajilia uone kama watakutumia link yoyote.
Yote yakishindikana fungua akaunti mpya tu kwa email nyingine uone kama itafanya kazi.