Naomba tumsaidie Joyce Kiria wa wanawake live. Anabomoa msingi wa taifa Bora

We ndo unapenda unyanyasaji, na point zinakuchoma Kama pasi,
Nimnyanyase mume ninayempenda neverrr,
nakushauri achaaa na uwe na upendo yote hayo hayatakuwepo.
Hapo mwenyewe mbona nahubiri upendo sana, soma in a positive way. Mtu unayempenda huwez kumpiga Wala kunyanyasa.
 
Naungana na wewe. Mimi ni mwanamme lakini kusema ukweli mambo ya vipigo nayaona ni kitu kilichopitwa na wakati. Siyo kipigo kwa mke tu bali hata watoto. Japokuwa mtu unaweza kukasirika sana na kujikuta umefikia hatua ya kupiga lakini siku zote tujitahidi kutumia njia za maongezi kufikia suluhisho. Kama mnashindwa kufikia suluhisho basi njia iwe ni kuachana kwa usalama japo hili nalo linaleta matatizo kwa watoto.
 
What a gentleman, thank you for understanding.
Tunatamani Sana kusiwe na vifo au familia kufarakana sababu ya kipigo.
Let love lead🙏
 
Hivi mtu amepigwa hadi ametolewa meno au jicho tunahitaji kumsikiliza eti ilikuwaje hadi akamtoa mwenzie jicho??? Vipi visivyozingatia taaluma ya habari vinafungiwa kila siku kwani huoni? Hadi kimeachwa maana yake kipo sawa
Kwamba mwanamme timamu na akili zake timilifu amponde mkewe hadi kumnyofoa meno bila sababu sio, ndo unataka tuamini hivyo sio?
Halafu hilo ni shambulio in terms of criminal case na sio unyanyasaji kama inavyosadikishwa.
 
Tatizo lake yuko biased! Kwani wanaume pia hawanyanyasiki au sababu tumekaa kimya?
Hivyo vipigo ni shauri la kuchoka kuvumilia kero zao.
Jitokeze na madhira yako unayopata paza sauti, nitakusaidia kupinga kelele [emoji23]
 
Mume kwenda kwa mchepuko ni dalili kwamba wewe kama mke hutoshi katika nafasi yako iwe kwa makusudi au bahati mbaya.

Kama mke unasimama katika nafasi yako vizuri mume hata kama atachepuka anakuwa na nidhamu bado!
Hiyo yakuchepuka iache kabisa, uzinzi ni tabia ya mtu hata afanyiwe nini, kuna tabia nikama ngozi mkuu!
 
Poleee ila tenda Wema tu na umuombee sanaa. Ujue viseversa pia it's true wanaume wengi tu wanadharau wake zao wakipata
So we tenda Wema tuu na mjitahid kuwa Makin wakati wa kuoa upate mtu mtakayeelewana pia.
Tena wanadharau sana, mnaanza chini Mungu akishawabariki tu shida inaanzia hapo, acha waseme tu ila ukweli wanawake wanavumilia sana
 
Swala la kupiga halikubaliki. Sheria zipo lakini post zake kwanini zijikite kwenye kuachana!? Hakuna hatua mbadala. Wanaoachana waachane kwa Amani ilausitokee kwa ushawishi wa mtu
Naona yeye amechagua cases zenye mwelekeo wa kuachana. Nia ikiwa ni kuwaelimisha wanawake wanaoteseka kwenye ndoa wasione aibu kuachana na mateso kwa kuhofia ndoa.
Ni sawasawa kuwa na wanahabari wa michezo, uchumi, mazingira etc
 
Jitokeze na madhira yako unayopata paza sauti, nitakusaidia kupinga kelele [emoji23]
Over my deadbody! Tutayamaliza mjengoni tu iwe kwa siasa au makofi ila sipeleki tatizo langu na wife kwenye media.
 
Sasa nyie wanaume hamtoi ya moyoni mnagugumia moyoni wanawake wanasema wasikike huko nje, Ila mwisho wa siku tunapata one side of the story kwingine hatujui before judging
 
Hii imekaa vzr...
 
Tunatakiwa tuandamane kwenye mitandao ili TCRA wamuweke bench, kile kipindi hakimfai yule hafai kuwa mwalimu wa wanawake yule ni victim wa ndoa, wala hana experiance zaidi ya simulizi anazoambulia kushuri kuachana, anatakiwa asifanye hiyo kazi kabisa[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Hee una utani na watuu...yaani midume mizima inategemea wadhungu!!?
 
Mwisho wake sasa atakuwa amezalisha kundi kubwa sana la wanawake walioachika kwa ushawishi wake na kufanya taifa liwe na mpasuko mkubwa sana
 
Maskini dada wa watu lbda amepata pa kutolea nyongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…