Naomba tumsaidie Joyce Kiria wa wanawake live. Anabomoa msingi wa taifa Bora

Haya mambo haya, tunyamaze tu! Ndoa zetu zina mambo mengi sana, tuombe Neema ya Mungu mkuu itusimamie.

Joyce aendelee na vipindi vyake maana najua kuna roho anazisaidia kuendelea kuishi kwa Uhuru na amani.
 
By nature Mimi sio muumini wa vipigo. Sio kwa mke tu ata Watoto, Au vya wanafunzi. Kuna wanafunzi wa mpaka miaka 20 wa advance wanafundishwa kwa kuchapwa!?.
Swala la kupiga lilikuwa NI la hulka. Zipo jamii bado hutoa adhabu za viboko adi kwenye mikutano ya kijamii. Mfano sungusungu huko unyantuzuni NDANI au Ukulyani.

Tupinge kabisa vipigo Kama vipigo na jamii inahitaji elimu kubwa Sana kuacha kupiga.

Au mnawashauri vipi watoto wanaopigwa wakimbie makwao!?

Aache kuhamashisha uvunjwaji ndoa Lisa vipigo
 
Kwamba mwanamme timamu na akili zake timilifu amponde mkewe hadi kumnyofoa meno bila sababu sio, ndo unataka tuamini hivyo sio?
Halafu hilo ni shambulio in terms of criminal case na sio unyanyasaji kama inavyosadikishwa.
Kwa hiyo mtu kama amekukosea suluhisho ni kumbonda sio?
 
Wanaume wengi tuna nyanyaswa sana na wake zetu sema sisi hatuna makelele kama wanawake. Na sisi tukianzisha kampeni ya mwaume jikomboe tutafukuza wake zetu mwisho wataanza kulia mitaani. Waache waendelee sisi tuna waangalia kwa mbali tuna usoma mchezo. Tuki inuka watakiona cha mtema kini!
 
Kea
Kwa hiyo Bora kukaa tu hata Kama hamna furaha? Au Hadi ufe?
Anayevunja avunje lakini ifahamike tu mwanaume ana soko kuliko mwanamke

Mngekuwa na akili msingejishughulisha na harakati za hovyo badala yake mngejenga ndoa

Mlioshindwa mmekomalia kufa kwani mnakufa nyinyi tu? Wanaume wameshakufa sana kwa ndoa/mapenzi
 
Take time to know her history you won't be worried but utazilaumu mamlaka .....
 
Bibl Biblia ipi imekataza msitengane?
 
Sasa ndo ukute amevunja ndoa yake kwa mikono yake kisha anatoka faragha na mme wa mwanamke mwenzie
 
Alitakiwa ahubiri misingi ya ujenzi wa familia bora zenye upendo kabla ya kujenga hoja ya kuzivunja,anaangalia alipoangukia badala ya alipojikwaa.

Anatafuta cheap popularity bahati mbaya hana weledi wa kutosha wa kitaasisi zaidi ya kupiga umbeya.

Kuna watu wamesomea masuala ya jenda na ni wabobezi

Kila jinsia ina saikolojia yake, usipoijua basi utapata tabu sana, mwanaume usipomuheshimu, atakuvumilia, lakini ipo siku atakutwanga tu,kama huoni haja ya kumuheshimu,tembea kwenu,kwa nini ukae ili umvuruge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…