Naomba tuungane kuanzisha Vitabu vya Dini ya Waafrika

Naomba tuungane kuanzisha Vitabu vya Dini ya Waafrika

Habarini,

Baada ya kupitia mijadala mingi humu JF na mitandao mbalimbali nimeona sasa kunaumuhimu wa kuungana sisi wenyewe Waafrika na kuanzisha dini/kanisa la Imani ya Waafrika/Washindi wa Afrika/Africa Catholic nk.

Hii ni kutokana na uwazi kuwa sasa Waafrika tumeanza kujitambua hivyo inatubidi kuweka maandiko yetu ya kiimani na kuabudu yatakayofundisha mambo mazuri na kuyaendeleza na pia mambo mabaya na kuyaacha kwa kufuata mfumo uleule wa kuzikataa dini na imani tulizoletewa na wakokoni wote kwani siyo rahisi kuzikataa pasipo kuanzisha ya kwetu.

Naomba mapendekezo yenu wote wenye nia njema na Afrika kwa kuanza na jina lipi litumike kuiwakilisha dini/imani yetu ingawa naona kabisa madhebu yetu yanaweza kuegemea koo au makabila yenye mila na desturi zilizosawa na vitabu vyetu pia vinaweza kuwa hivyohivyo i.e. kitabu cha Wasukuma, kitabu cha Wachanga, n.k

Naomba kuwasilisha.
umasikini ulio kuwa nao umesababishwa na dini?
 
Kabla ya yote chimbua kabla ya ujio wa weupe je Mwafrika aliabudu dini ipo?.
Chunguza kuhusu asili ya mwafrika then ndipo uje kwenye ideology ya kuanzisha dini.
Hivyo walivyoabudu Waafrika kabla ya ujio wa watu weupe ndiyo dini
 
Mimi simuamini huyo yesu wa mohamed kama wewe bwana na hata hao mambo yao yaliandikwa na jamii yao siyo mwafrika kwani wapi umeelezwa kuwa yesu,musa au mohamed walikuwa ni Waafrika?

Siongelei na htutaandika habari za wazungu wala warabu katika kitabu chetu kama wao ambavyo hawakutuandika Waafrika kwenye biblia au quruan zao.

Jiongeze
Sikulaumu

Swali lako la uafrika ungesoma Hadith wala usingeuliza

Ndugu zangu Waafrika tusitafute mchawi wa kumshushia lawama za umasikini wetu tusome tusome tusome

Tusikimbie wajibu kuwa mababu zetu walitufelisha big time

Vasco da gama aligota cape of good hope for yeaars

Mababu zetu wa pwani ya Afrika mashariki walikuwa na muda wa kutosha kujiandaa kuwakabili lakini walikuwa busy na nini sijui

TUSOME TUSOME TUSOME!!
 
of what ue? Nilidhani tuungn e tutengeneze magari, ndege , baiskeli , tugundue dawa za magonjwa yanayotukabiri, etc etcza african brand, bado tu mko kwenye dini!
Lazima tuwe na belief yetu kwanza ndipo tuweze kuwa na vyakwetu huwezi kuwa na gari la mzungu lugha ya mwarabu imani ya muhindi
 
Hakuna haja ya kuvumbua gurudumu kwani lishavumbuliwa tayari. Wazungu walipokuja kuvamia Africa Babu zetu walikuwa na miungu yao. Walitumia miungu na mizimu yao kutaka kuwaondoa wazungu lakini ilishindikana. Kwanini? Kwa sababu miungu ya wazungu ina nguvu zaidi ya miungu ya waafrika! Tuifuate miungu na maarifa ya wazungu tutafanikiwa kama wao.
Tatizo niuelewa mdogo kama wako siku ukijua kuwa uliongopewa juu ya Mungu wa wazungu na Miungu ya Waafrika basi utatambua kuwa kutokuwa na umoja na kusaritiana baina ya Waafrika ndiyo sababu ya wao kushindwa na wazungu,Mungu ni mmoja hakuna wa wazungu wala wa Waafrika bali mila na desturi ambazo ni silaha muhimu au njia za kuwasiliana na Mungu za Waafrika ndizo zilibezwa na kupotoshwa.

Tafakari
 
Mfumo wa nature chenye nguvu umeza kinyonge.
Kama miungu ya kiafrica ilishindwa kumlinda mwafrika asichukuliwe utumwani plus kutawaliwa je kwa sisi kizazi cha SAsa tuna haja ipi kuabudu miungu dhaifu iliyoshindwa.
Tatizo ni kutokuelewa kuwa Waafrika walisalitiana na mzungu alitumia divide anda rule.

Kwenye biashara ya watumwa mzungu alikuwa ni soko na pia waliofanya biashara hii ni machifu wa kiafrika ambao walisalitiana kwa tamaa na kutoa siri zao kwa wazungu kitu ambacho walipokibadilisha wazungu waliondoka kwa kisingizio cha kutoa uhuru
 
Ndiyo hapo mkuu najiuliza kila siku

Hiyo miungu ilikuwepo wapi wakati wale washenzi wanakuja kutupeleka utumwani
Mzungu hakuja na miungu bali waliivunja kupitia Waafrika wenyewe walioisaliti sasa kama ulivyolishwa ujinga uliolishwa na ukaamini ndivyo ndivyo Machifu walivyolishwa uongo juu yao wakagombana na kupoteza asili yao.

Mungu na miungu ilishindanishwa wapi na akatokea mshindi?Waliokuja Afrika ni wafanyabiashara,missioneries,wasafiri na wachunguzi siyo mungu wa wazungu au wazungu wote kuhamia Afrika na mungu wao au mizimu yao
 
Huenda walituzidi hakili kwa kujiaminisha Sana kwa miungu yetu kwamba wao niwa tiifu kuliko sisi kupitia mabarozi wake ambao niwaganga na machifu lakini baada ya kuaminika na miungu wakaamua kutudhuru
Hicho ndicho kilichofanyika waliwagombanisha machief na kuwafarakanisha kisha wakakaa katikati yao baada ya kupigana machifu na kujidhoofisha
 
Mzungu hakuja na miungu bali waliivunja kupitia Waafrika wenyewe walioisaliti sasa kama ulivyolishwa ujinga uliolishwa na ukaamini ndivyo ndivyo Machifu walivyolishwa uongo juu yao wakagombana na kupoteza asili yao.

Mungu na miungu ilishindanishwa wapi na akatokea mshindi?Waliokuja Afrika ni wafanyabiashara,missioneries,wasafiri na wachunguzi siyo mungu wa wazungu au wazungu wote kuhamia Afrika na mungu wao au mizimu yao
Mkuu twende taratibu

Mbona hakuna mahali nimesema Miungu ilishindanishwa😂

Kwahiyo unalalamikia Miungu ya Afrika imesalitiwa?

Unajua nini kuihusu mkuu?
 
Hakuna haja ya kuvumbua gurudumu kwani lishavumbuliwa tayari. Wazungu walipokuja kuvamia Africa Babu zetu walikuwa na miungu yao. Walitumia miungu na mizimu yao kutaka kuwaondoa wazungu lakini ilishindikana. Kwanini? Kwa sababu miungu ya wazungu ina nguvu zaidi ya miungu ya waafrika! Tuifuate miungu na maarifa ya wazungu tutafanikiwa kama wao.
[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Kabla ya ujio wa hizi dini waafrika walikuwa gizani wakimtafuta Mungu kupitia kuabudu vitu wasivyovijua in deep yaani nature kupitia matambiko kwa kuabudu milima, misitu, nk.
Sababu ya kuwa gizani wakimtafuta Mungu, shetani akatumia fursa hio akawamiliki kiimani akajifunua kwao kupitia mizimu , wao waliamini wanamuabudu Mungu. Kwa sababu shetani ndie mkuu wa ulimwengu, mwanadamu baada ya kutenda dhambi akatupwa duniani ambapo tayari shetani alikuwa ashatupwa duniani toka mbinguni,hali mwanadamu alitupwa toka bustani ya Eden.
Mwanadamu na shetani wote wapo duniani kwa mda mfupi sababu Dunia si makazi y kudumu kwa shetani na mwanadamu.Makazi ya kudumu ni paradiso na jehanamu.
Dunia si milele, ni temporary place, thus tunakufa mda ukifika.
Siyo kosa lako ndivyo ulivyokalilishwa na wazungu kuwa kuna paradiso nyingine zaidi ya Afrika kwako Mwafrika,je wahindi,wachina,nk nao wataingia paradiso kwa kupitia wazungu?

Mbona wana dini zao na imani zao na wamefanikiwa sana tu bila dini za wazungu?
 
Habarini,

Baada ya kupitia mijadala mingi humu JF na mitandao mbalimbali nimeona sasa kunaumuhimu wa kuungana sisi wenyewe Waafrika na kuanzisha dini/kanisa la Imani ya Waafrika/Washindi wa Afrika/Africa Catholic nk.

Hii ni kutokana na uwazi kuwa sasa Waafrika tumeanza kujitambua hivyo inatubidi kuweka maandiko yetu ya kiimani na kuabudu yatakayofundisha mambo mazuri na kuyaendeleza na pia mambo mabaya na kuyaacha kwa kufuata mfumo uleule wa kuzikataa dini na imani tulizoletewa na wakokoni wote kwani siyo rahisi kuzikataa pasipo kuanzisha ya kwetu.

Naomba mapendekezo yenu wote wenye nia njema na Afrika kwa kuanza na jina lipi litumike kuiwakilisha dini/imani yetu ingawa naona kabisa madhebu yetu yanaweza kuegemea koo au makabila yenye mila na desturi zilizosawa na vitabu vyetu pia vinaweza kuwa hivyohivyo i.e. kitabu cha Wasukuma, kitabu cha Wachanga, n.k

Naomba kuwasilisha.
Ila tu isiwe ya zile imani za vilingeni🤔
 
Mkuu
KAMWE, narudia KAMWE haitatokea anytime soon

Jamani dini sio jambo dogo hasa hasa kuianzisha

Mnavyowaona akina mwamposa wanatreza sababu kuna mtu alitundikwa msalabani, watu waliuwawa, watu walitengwa na jamii zao

Kwahiyo hizi sio story za kijiweni

Msipoteze muda na hili
Sema siyo jambo dogo kwako wachina,wahindi,wakorea,warusi,wahindink waliwezaje?

We kaa pembeni Waafrika tufufue dini zetu kwani wewe ni mzungu au mwarabu na dini yako.
 
Mfumo wa nature chenye nguvu umeza kinyonge.
Kama miungu ya kiafrica ilishindwa kumlinda mwafrika asichukuliwe utumwani plus kutawaliwa je kwa sisi kizazi cha SAsa tuna haja ipi kuabudu miungu dhaifu iliyoshindwa.
Muafrika na mzungu wali "interact kwa kipindi gani hadi wakafikia kutawaliwa??haohao unaosema wana miungu yenye nguvu walishaanza kufanyiana hayo mambo ya utumwa na kutawaliwa na wengine miaka maelfu huko sembuse afrika juzi tu..........shida waafrika wengi wanadhani historia yao ilianzia pale mzungu alipokuja ndo maana wengi hata uzao wao unakuta anavijua vizazi vi 3 a u 4 tu vya nyuma na ambavyo aidha vilifata ya mwarabu au ya mzungu, nyuma ya hapo kapa
Hao mnaowaita taifa teule walikua utumwani kwa miaka ya kutosha na leo ndo mnaamini vitabu vyao na kusema miungu yao ndo ina nguvu
Screenshot_20230224-180610_Samsung Internet.jpg
Screenshot_20230224-180556_Samsung Internet.jpg
 
Nazungumzia reality nimestudy pote
Hakuna ulipostudy sema umefundishwa na wazungu na wazazi wako maisha ya wazungu na hujawahi kutafakari iwapo wazungu au warabu walikuwa sahihi kwa wao kueneza dini zao Afrika na kuua dini za Kiafrika
 
Back
Top Bottom