Naomba tuungane kuanzisha Vitabu vya Dini ya Waafrika

Naomba tuungane kuanzisha Vitabu vya Dini ya Waafrika

of what use? Nilidhani tuungane tutengeneze magari, ndege , baiskeli , tugundue dawa za magonjwa yanayotukabiri, etc etc za african brand/flavour, bado tu mko kwenye dini!
Hayo utafanya wewe,huyu kaja na hili,mwingine atakuja na lingine
 
Ndio Mungu ni mmoja lakini hata ndani ya waafrika wa kale kuna waliompatia na wengine wengi waliishia kuabudu viumbe tu kama majini nk. Mungu hujifunua kwa wanadamu polepole na inweza kuchukua mamilioni ya miaka kufunuliwa kuhusu Mungu. Wazungu walishaupata ufunuo ulio wa juu zaidi yetu kuhusu Mungu. Na ujue sio wazungu wote. Sasa kwanini kurudi nyuma?
Majini asili yake ni warabu ambayo sisi Waafrika tunaiita mizimu, hao waarabu hawakutawaliwa na wazungu na kuoandikizwa ujinga wa wazungu ndiyo maana waliweza kujisimamia baada ya kuzitetea mila na desturi zao,pia wachina,wazungu,n.k waliweza kisimamia mila na desturi zao.

Huwezi kufanikiwa iwapo hujaweza kuzilinda mila na desturi zako i.e. dini/imani ndiyo maana Afrika ni maskini kulinganisha na wazungu na warabu waliosimamia mila zao.
 
Kipi kilichoanzishwa na Mwafrika kikafaulu, pan africanism imefeli, imani ya rastafari imefeli. Kabla ya kuanzisha jambo angalia asili ya watu hao ipoje
Muda ndiyo unaoamua waliotupoteza ni waliotutangulia i.e. educated elites baada ya waasisi wetu wa awali i.e. mababu zetu lakini sasa tumekuja zao jipya tutaweza kabisaaaa labda wewe msaliti ndiyo utashindwa kwa kuendelea kuisaliti imani yako
 
Yani kitu pekee kingetuletea dini ni Kinjekitile kushinda ile vita ya maji maji

Mussa (as) na Muhammad (saw) wenzake walishinda vita zao yeye alifeli
Tatizo unaamini ulichoaminishwa na waliokutawala hivyo siyo rahisi kutafuta ukweli juu ya uliotawaliwa nao hasa kujua nini sababu ya kinjekitile kufeli kama siyo kusalitiwa kitu ambacho watu kama wewe mnakiendeleza kwa kusaliti kila wazo la Mwafrika.
 
Can you be spiritual person without bealiving in God?
Who is God to you? Concept ya Mungu ni tofauti kwa kila jamii/mtu............we una namna yako ya kumtambua mungu unaemuamini wengine wanaabudu ng'ombe............wengine mungu ni ile nguvu ya juu kabisa katika kile wanachokiamini
 
Dini ni sehemu ya mila na tamaduni zako ambazo zitakutambulisha kwa kuamini Mungu yupo.Ulaya mila na tamaduni zao zimeweza kuwatambulisha Wajerumani kupotia dini yao ya kilutheli,uk kupitia dini yao ya anglikana,na nchi nyingine zenye dini za usabato,rc,nk.

Kama waingereza wanaiita dini yao angilican kutoka na utashi wao kwani Waafrika tukiamua kuiita dini yetu AFRICANISM kuna tatizo?

Wakati ni huu dini ya Waafrika itarejeshwa kwa kuunganisha mila na tamaduni zetu na siyo ujinga wako,kwanini wakorea,wachina,wahindi,nk wawe na dini zao kutokana na mila na destuli zao WAAFRIKA tushindwe?

Sasa huo siyo ujinga ni nini?
 
Hii tafasiri unayoitoa hapa ni euroncentric view na ndivyo ulivyoamini kwa kuwa tu umetafasriwa na mabwana zako wazungu.

Kama tayari tuna spiritual basi sasa tuwe na taasisi yetu ya Kiafrika itakayosimamia spiritual za Waafrika.
 
Kama ni mambo ya kufikirika why una dini ya kigeni usiwe na dini yako?

Huwezi ukapata kitu bila kukifikiria hata kidogo
 
Hakuna haja ya kuvumbua gurudumu kwani lishavumbuliwa tayari. Wazungu walipokuja kuvamia Africa Babu zetu walikuwa na miungu yao. Walitumia miungu na mizimu yao kutaka kuwaondoa wazungu lakini ilishindikana. Kwanini? Kwa sababu miungu ya wazungu ina nguvu zaidi ya miungu ya waafrika! Tuifuate miungu na maarifa ya wazungu tutafanikiwa kama wao.
Yesu Kristo ana nguvu kuliko miungu yote ya Kiafrika.
 
Una muda gani tangu umefuata dini,elimu,mavazi,lugha,nk kutoka kwao je umeendelea nini kama siyo kuwa mtumwa na tevemezi?

Jitawale kupitia fikira zako ndiyo utafanikiwa,hao wazungu baada ya kukupa elimu yao kupitia kukufundisha mambo yao wamekuwezesha kujiendeleza au wamezidi kukufanya kuwa tegemezi kwao?

Tulichostahili kupata kutoka kwa wazungu ni kujua kusoma na kuandika basi siyo dini,mila na tamaduni zao kwa kulitia kusoma na kuandika tungeweza kubadilishana mawazo yetu na mwishowe kuvumbua vitu mbalimbali kama wachina,wahindi,nk

Tafakari na ujiongeze je wengine wote wasioamini ktk ukristo na uislam hawajaendelea?kama wameendelea basi uislam na ukristo SIYO issue ktk maendeleo.
 
Muhindi na mchina je?? Ishu ni kufata kama zombi,,,hizo teknolojia na maarifa mengine pia mzungu alichukua kwa wengine sio vyote vya kwake,,,kakopi ila kabaki na asili yake kama walivyo wahindi na hata hao wachina na wenzao, we mtu mweusi unataka kukopi na ku paste kila kitu hadi asili yako unaisahau ,huo sasa ndo utumwa na ndo maana pamoja na kukopi kote huko bado afrika na mtu mweusi amebaki kua masikini na mtu wa mwisho karibia kwenye kila kitu duniani tofauti na wenzie waliokopi ya wazungu na wakafika mbali kama wahindi, wachina na hata waarabu.........watu wanakopi ila hawazifuti asili zao kama mtu mweusi anavyofanya kwa upumbavu wake
Hapa umewasaidia,asante!
 
Who is God to you? Concept ya Mungu ni tofauti kwa kila jamii/mtu............we una namna yako ya kumtambua mungu unaemuamini wengine wanaabudu ng'ombe............wengine mungu ni ile nguvu ya juu kabisa katika kile wanachokiamini
Siyo kweli umeongopa pale ngombe anatumika kama kiunganishi chao na Mungu kama wewe unavyomtumia yesu au muhamadimaria,nk.

Hata Afrika wanatumia viumbe mbalimbali kuwaunganisha na Munguhata USA wanamimini tai ananguvu ya kuwaunganisha na nguvu ya Mungu
 
Tunarudi palepale huyo unaesema mungu ndani yako unaielewaje/kuitambuaje hio nguvu......kama wote tungekua tunaitambua hio nguvu moja basi dunia ingekua paradiso
 
Yesu Kristo ana nguvu kuliko miungu yote ya Kiafrika.
Ana nguvu kwako usiyejitambua na siyo kwa Waafrika,Wahindi,Wakorea,nk wanaojitambua je Waafrika wasiowamwani yesu hawafanikiwi na nyie mnaomuamini mmefanikiwa wote?
 
Tunarudi palepale huyo unaesema mungu ndani yako unaielewaje/kuitambuaje hio nguvu......kama wote tungekua tunaitambua hio nguvu moja basi dunia ingekua paradiso
Hakuna kitu paradiso ondoa ujinga huu kichwani kwako na uache kukariri na kuamini kila ulichofundishwa au kulishwa na mzungu,nguvu ya Mungu iko ndani ya kila kiumbe na ndiyo maana kila kiumbe kina hisia
 
Ana nguvu kwako usiyejitambua na siyo kwa Waafrika,Wahindi,Wakorea,nk wanaojitambua je Waafrika wasiowamwani yesu hawafanikiwi na nyie mnaomuamini mmefanikiwa wote?
Ishu sio mafanikio, ishu ni je miungu ya Kiafrika ipo na inafanya kazi?
Mbona watu wanarogwa licha ya kwenda kwa waganga kibao?
Haya njoo waulize watu wanaomtii Yesu kwa moyo wao wote, hawapindishi kitu, Yesu anawapigania katika maisha Yao yote.
 
Hakuna kitu paradiso ondoa ujinga huu kichwani kwako na uache kukariri na kuamini kila ulichofundishwa au kulishwa na mzungu,nguvu ya Mungu iko ndani ya kila kiumbe na ndiyo maana kila kiumbe kina hisia
Naona hatuelewani.........kwani nimeongelea paradiso ya hizo imani za wazungu?? Nilichomaanisha ni kwamba hii dunia watu wasingekua na mitifuano isioekeweka. . .unaelewa nini ukisikia paradisio, nirvana na utopia???
 
Back
Top Bottom