Na wewe kwanini ukakubali kupelekwa utumwani?? Kwanini usipambane?? Huoni kupelekwa utumwani ilikuwa ni ujinga na uoga na uzembe wako mwenyewe!!-- inakuaje mtu atoke atokake aje nyumbani kwako na anakukamata kama swala na anaondoka na wewe kiulaini !!, isitoshe utumwa ilikuwa ni biashara iliyochukua muda mrefu je mlishindwaje kushirikiana nyinyi wenyewe na kuitokomeza??, waafrika tulikuwa hovyo na hadi leo tunanyanyaswa na kubaguliwa na kuporwa maliasili zetu ni muendelezo wa ujinga uleule tuliorithi kutoka kwa mababu zetu hivyo huna haja ya kumlaumu Mungu bure juu ya ujinga wako.
Utumwa haujaisha,kama mababu zetu walivyochukuliwa namna ile,hata leo,tunapigwa sana,lakini sio kweli kwamba watu walichukuliwa kizembe,
Ushahidi ni vita ya majimaji,machifu kibao walinyongwa,jamii nyingi zilipambana kupinga utumwa,lakini kwa vile tulikuwa na dhana duni,tulishindwa vita,
Mfano mzuri,chukulia dikteta wa Libya Ghadafi alivyotandikwa na nchi za magharibi,kwa vile tu hakutaka wazungu waendelee kuvuna mafuta yake,nchi za ulaya,NATO,na USA,zilimtandika,zikamuua,na sasa hv wanavuna mafuta yake,
Umoja wa Afrika,ulikaa kimya,ukafyata mkia!hii imetokea Karne 21.
Tulipambana,ila wakatuzidi,baada ya uhuru,sisi tulidhani ubaya wa wazungu ni rangi yao,tukaweka weusi wenzetu,baada ya muda wakaonja utamu wa madaraka,ndio tukazaa majambazi ya ccm bongo,kanu Kenya,na Mengine Mengi,Uganda,Afrika magharibi,
Inabidi tuyaue haya Ili tukae vzr