Naomba uniulize chochote kuhusu kufanikiwa katika Biashara na Ujasiriamali

Naomba uniulize chochote kuhusu kufanikiwa katika Biashara na Ujasiriamali

1. Kupanua uzalishaji wa Bidhaa maana yake ni kua bidhaa unazozalisha ni chache kuliko mahitaji ya clients wako. Kama bado unastruggle kupata clients, njia 1 na rahisi ni kuadd new features kwenye product yako ambayo wengine hawana, hata aina ya packaging pekee inaweza kukutofautisha, pia kuangeza quantity kwa bei ile ile.

Unajua kwenye biashara kitu cha kwanza kbs ni kuWin people's hearts, then ukitoka hapo ndio uanze kufikiria kutengeneza faida. Kama hauna consistent clients hauwezi kutoa products zako hivyo hauwezi kutengeneza faida. Kwahiyo uwe tayari kuingia gharama za kuwavutia wateja ambayo wazungu wanaita 'client acquisition'.

2. Mimi nahisi kwa products zako soko la ndani lenyewe ni kubwa sana, nahisi bado haujafanya utafiti wa kutosha. Lkn again sio mbaya kuingia kwenye soko la nje kama upo tayari.

Mimi mwaka jana nilivuna vitunguu November, lkn soko la bongo lilikuwa ovyo mno mno. Ukienda Kkoo na Buguruni bei ni elfu 70-80 wakati kipindi kama hiko mwaka 2015 bei ilikua 180k. So nilichokifanya ni kuuza Kenya, nilienda kwa bus hadi Nairobi, nikakutana na madalali wakanipa dira na kila kitu. Baadae nilivuna na kuuza mzigo wangu Garissa krb na mpaka wa Somalia kusini mwa kenya mbapo niliuze kwa bei mara 3 ya iliyokuepo bongo.

Nice one.
How do you win the master card prize?!
You have seen my products. All I need are funds to take off. You have links for grants and sort?!
Thanks for your time.
 
Ni maeneo gani mkuu yanafaa kwa makazi ya kudumu na kilimo.

Yasiyo na wafugaji kuepuka( VURUGU ZA WAKULIMA NA WAFUGAJI)

Na reli ya TAZARA imepita hapo?
Hapo msowero panafaa mana hakuna mvutano na wafugaji harafu kijiji kina huduma zote za jamii kuanzia umeme, barabara ya rami nk
 
Kaka Ongera Sana Mungu aendelee kukupigania kila nikisoma thread zako uwa naumia Sana najiona nimechelewa mno natamani ata nisimame Sasa hivi nifanye hiki na kile lkn too late, mbaya Zaid umekuwa mtu WA kutu-inspire tu kwa maneno nikikufata PM ata unielekeze wapi pa kuanzi unakua mgum.
All in all kaka kubali kubeba watu wachache ili huwe mwalimu watu tujisifu kufanikiwa kupitia mgongo wako.
 
Samahani mkuu Mimi Nina banda tayari Lakini mtaji wangu Ni laki tatu

Je ?? Naweza Kuanza Kwa huo mtaji ?? Nakama naweza kuanza

Waweza Nishauri lolote ??
 
Hapo msowero panafaa mana hakuna mvutano na wafugaji harafu kijiji kina huduma zote za jamii kuanzia umeme, barabara ya rami nk
asante mkuu ila msowero imepitiwa na reli ya Tazara?

Maana nilikuwa napenda mji wa Moro wenye treni Dar to Zambia.

Ulio karibu na Njombe au Songea pia.
 
Samahani mkuu Mimi Nina banda tayari Lakini mtaji wangu Ni laki tatu

Je ?? Naweza Kuanza Kwa huo mtaji ?? Nakama naweza kuanza

Waweza Nishauri lolote ??
Laki 3 kwa sasa haitakufikisha sehemu boss, kama ungekuwa na vifaa say feeders, drinkers nk ungeweza kuanza na japo broilers 50. Napo faida itakua kiduchu sana
 
Laki 3 kwa sasa haitakufikisha sehemu boss, kama ungekuwa na vifaa say feeders, drinkers nk ungeweza kuanza na japo broilers 50. Napo faida itakua kiduchu sana
Duh sawa mkuu Matumain yangu yamekata sababu

Vidole avilingani Uwezo wangu Ndio huo mkuu
 
Kaka Ongera Sana Mungu aendelee kukupigania kila nikisoma thread zako uwa naumia Sana najiona nimechelewa mno natamani ata nisimame Sasa hivi nifanye hiki na kile lkn too late, mbaya Zaid umekuwa mtu WA kutu-inspire tu kwa maneno nikikufata PM ata unielekeze wapi pa kuanzi unakua mgum.
All in all kaka kubali kubeba watu wachache ili huwe mwalimu watu tujisifu kufanikiwa kupitia mgongo wako.
Unataka kuniuliza nini PM mkuu ambacho ukiniuliza hapa hautaelewa. Boss, ni watu wachache sana watapoteza muda wao kuwatoa ushauri wa kibiashara bure, hiyo tu ni msaada tosha achilia mbali motivation ya bure.

Mimi nawalipa Awethu incubation $1800 kwaajili ya consultation pekee, na kila nikiwahitaji mimi ndio nawafata Afrika Kusini. Here am doing all this for free my boss.
 
Duh sawa mkuu Matumain yangu yamekata sababu

Vidole avilingani Uwezo wangu Ndio huo mkuu
Boss si lazima ufuge kuku, mpk sasa nimetumia karibia laki 2 kwa kila hekari ya mahindi (kutegemea mvua), na hesabu ni kuvuna kwa faida ya laki 4 kwa hekari - so nitarudisha laki 2 yangu na faida ya laki 4.

Jaribu kufikiria biashara gani unaweza kufanya kwa laki 3, mimi mtaji wangu wa awali haukuwa hata karibu na laki 3.
 
Mbegu gani unapanda ( kwa maana ya breed ya Mahindi & Mpunga ) au ni local/ ya wenyeji ?
 
Ni kwanini wafanya biashara wengi wanafeli kibiashara?
**Kutokuwa na taarifa sahihi - mtu anasikia biashara ya tikiti maji inalipa haswa, kesho anaingia shamba kulima tikiti, hajui chochote ye anawaza akivuna atapiga faida Milioni kadhaa.

**Mitaji ya kuunga unga - unakuta mtu ana mtaji mdogo lkn anataka afanye biashara kubwa ili apate faida kubwa, anaishia kuteketeza kile kdg alichonacho.

**Kutokujua principles za biashara kama uvumilivu - mtu anaanza biashara asubuhi anataka jioni aone faida. Au unakuta mtu kuyumbishwa kdg tu na upepo anaamua kuacha kabisa biashara.
 
Daaah kwenye biashara naona nicheza makidamakida nilijaribu kufuga kuku wa nyama niliishia kuwauza kwa mkopo hadi leo sijajua nilipokosea sasa nilipoona picha za kuku nimekumbuka mbali natamani kurudia biashara hiyo lakini soko imekuwa kikwazo sana kwa mkoa nilipo.........unakuta wapo walioshika soko kwa muda sasa wewe inakutia kwenye mahangaiko sana
 
**Kutokuwa na taarifa sahihi - mtu anasikia biashara ya tikiti maji inalipa haswa, kesho anaingia shamba kulima tikiti, hajui chochote ye anawaza akivuna atapiga faida Milioni kadhaa.

**Mitaji ya kuunga unga - unakuta mtu ana mtaji mdogo lkn anataka afanye biashara kubwa ili apate faida kubwa, anaishia kuteketeza kile kdg alichonacho.

**Kutokujua principles za biashara kama uvumilivu - mtu anaanza biashara asubuhi anataka jioni aone faida. Au unakuta mtu kuyumbishwa kdg tu na upepo anaamua kuacha kabisa biashara.
mashamba huko ruvu chini bado yapo mkuu? maana nikikuita dogo unamind
 
Back
Top Bottom