ONTARIO
JF-Expert Member
- Oct 16, 2013
- 1,884
- 17,096
- Thread starter
- #161
Aisee, sasa kwa kijana ambaye ni mgeni kwenye ishu za ujasiliamali, namaanisha hajakomaa vizuri,
wewe kama wewe unamshauri atumie njia ipi kati ya hizi tatu kwa kuanzia(yenye afadhali)
Forex, kilimo, ufugaji(natambua unauzoefu nayo thats why nimekuuliza kuhusu hayo)
Hahaa hahaa - swali hili liko tricky sana.
Mimi napenda Kilimo kwasababu kinaonekana, kina make sense hata ukimwambia mtu na pia usimuone mtu kama rais mstaafu Dr. J. Kikwete anatoka nyumbani kwake anaenda mashambani kupiga picha na mahindi afu anapost Twitter, kuna raha yake aisee. Yani there's that feeling you get, kwamba ili watu wale inabidi wewe ulime, yani kuna kitu fulani sijui kama unanifeel.
Kuhusu poultry nafanya kwasababu ni passion, kifaranga unakibreed kutoka Day Old chick hadi anakua mkubwa. Afu watu wote wanajua Ontario ni mtu wa poultry, na network yangu kubwa nimeshaijenga upande huo so lazima nikomae.
Lkn ukija kwenye Forex, kama leo nikifilisika kila kitu nikabaki na laki 3, yotr naingia nayo kwenye forex. Nina uhakika baada ya mwezi nina mil 2 mkononi, kitu ambacho si kuku wala shamba vinaweza kunipa hiyo reward. So naeza kusema, if I were to start again from zero I'd go for forex.