Naomba ushauri: Hati ya kiwanja ni ya mke wangu pekee au naweza kubadilisha majina?

Haya mambo ni zaidi ya vile tumeyasoma Mkuu, amini nakwambia inawezekana kabisa. Nimefanya kesi 2 mwaka jana za mtindo huo huo tena baada ya mwanamke kudanganywa na kugoma kuhamisha umiliki uwe wa wawili.

Natamani yule mwanamama akate rufaa HC ili itoke precedence. 😂
 

"........akasema tuchange hela tununue........."

☝️☝️ kosa la kwanza kubwa sana.

".........huko alipoenda alikuwa na mama ake mzazi wakanunua mimi kipind chote hicho sikuwahi kuulizia hati ya kiwanja lakini kwenye kiwanja nimefika mara tatu........."

☝️☝️ kosa la pili .

Ila subiri ushauri wa wadau wenye uzoefu na kesi kama hizo.
 
Huyo mkeo remote ni mama yake,
Kabla ujajenga nyumba pamoja, jenga yako kimyakimya.
Nina uhakika alinunua viwanja viwili, wewe kakuonyesha kimoja, deed ya pili ipo kwa mama yake. Shtuka
wewe ni dhaifu sana
 
Yale yale ya Mwandishi wa ITV na Radio One Ufoo Saro, Marehemu Mpenzi wake Mushi na Mama Mtu kumwagwa Ubongo na kuwa Historia sasa.
 
Huyo mkeo remote ni mama yake,
Kabla ujajenga nyumba pamoja, jenga yako kimyakimya.
Nina uhakika alinunua viwanja viwili, wewe kakuonyesha kimoja, deed ya pili ipo kwa mama yake. Shtuka
wewe ni dhaifu sana
Sawa
 
Nashukuru kwa ushauri
 
Kwanza hati ya kiwanja haina mashahidi, sijui hapa unamaanisha mkataba wa mauziano au nini. Pili hati inabadilishwa majina kwa maana ya umiliki kwa makubaliano ya pande zote mbili. Tatu wewe ni bwege na huhudhurii vikao. Tulishasema don’t trust a woman. Wanawake wengi hutumia wanaume ili kuvushwa kwenye mambo yao. Kwenye hili bado nafasi ipo, nenda nae taratibu mbadili umiliki, tumia sana akili asihisi tofauti, vinginevyo ndio utaharibu kila kitu. All the very best
 
Yeye kakubali na ameshanipa hiyo hati
Kama amekubali mkuu ni sawa, ila kukupa hio hati haimaanishi ndio unakiliki bado anamiliki yeye. Anatakiwa akubali kubadili umiliki kutoka kuwa yeye hadi kuwa ninyi.
 
Hebu eleza vizuri mkuu,ni hati ya kiwanja au karatasi ya mauziano?
 
Kwa kilatini tunasema "Quod licet Iovi, non licet bovi"
Haya kisheria nenda kwa mkeo muombe ubadili jina la kiwanja , akikataa basi huna haki nacho!
😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…