Naomba ushauri jinsi ya kumuapproach aliyenitafutia kazi, nataka kuacha kazi

Naomba ushauri jinsi ya kumuapproach aliyenitafutia kazi, nataka kuacha kazi

Nifanye Nini

Member
Joined
Sep 5, 2022
Posts
61
Reaction score
147
Salamu Kwenu Greatthinker(Akili kubwa).

Ushauri wako muhimu sana. Two weeks ago nilipewa connection Kwa Mzee wa makamu kidogo nikampigia simu kumuomba kazi the way nilivyoongea naye kupitia simu nilijionyesha kuwa Nina uhitaji sana na kazi hatimaye nikaitwa Kwenye interview japo Kwenye usaili palikuwa na graduates wengine ila kupitia ile connection nikafanikiwa kupata kazi nikapangiwa kituo changu.

Honestly Kwa nature ya kazi na nilivyojitathmini siwezi kufanya Kazi Na sio Kwa ubaya bali Kwa lengo la kutoharibu kazi za watu siku za mbeleni. Sasa nataka kuwasiliana na aliyenipa connection kuwa sipo tayari kuendelea kazi naombeni WanaJamiiforums ambao walishakutana na situation kama hii mnisaidie approach sahihi ya namna navyoweza kuacha kazi kubwa zaidi ni kumpa taarifa Mzee aliyenitafutia kazi in humble way asione kuwa nilikuwa namsumbua
 
Mpigie umwambie unahitaji kuonana nae kisha mkisha onana umueleze sababu za kutaka kuacha kazi!

Kimsingi lazima ujiande kujibu maswali magumu sana maana inakera sana nakuumiza sana kumtafutia mtu kazi halafu anaikataa wakati mwanzo alikulilia sana...

Kwakweli utamvunja moyo sana huyo mzee lakini usimwambie kwenye simu bali mfate mwenye umuone muongee ana kwa ana
 
Tell us first, umepata kazi nyingine? Ni kazi Gani hiyo usiyoiweza?
Tudadafulie nature ya kazi yako Ili tukushauri
Nature ya Kazi ni Kudeal na mikopo Sasa nimejitahidi kuendana na mfumo lakini najikuta nafsi inakataa ni kazi ambayo inataka roho mbaya afu usiwe msikilizaji na pressure kutoka juu ni kubwa sasa Mimi ni good listener inshort sipo tayari kuifanya
 
Mpigie umwambie unahitaji kuonana nae kisha mkisha onana umueleze sababu za kutaka kuacha kazi!

Kimsingi lazima ujiande kujibu maswali magumu sana maana inakera sana nakuumiza sana kumtafutia mtu kazi halafu anaikataa wakati mwanzo alikulilia sana...

Kwakweli utamvunja moyo sana huyo mzee lakini usimwambie kwenye simu bali mfate mwenye umuone muongee ana kwa ana
Tupo mazingira tofauti na kumpigia simu ndio the only means of communication.
 
Credit officer
Mkuu kwa uzoefu wangu hakuna kazi ngumu hapa duniani, ukiweka akili yako ikawa tayari kupambana unaweza na utafanikiwa, punguza presha na woga fanya kazi, jiweke low, fanya kazi kwa utaratibu huku ukiendelea kujifunza na kujijengea kujiamini... Usiache kazi, bora kupata changamoto kazini kuliko kuacha mana utampa mzee disappointment kubwa sana na utakuja kujutia.

Punguza uoga pambana, mtaani ni kugumu sana mzee.
 
Nature ya Kazi ni Kudeal na mikopo Sasa nimejitahidi kuendana na mfumo lakini najikuta nafsi inakataa ni kazi ambayo inataka roho mbaya afu usiwe msikilizaji na pressure kutoka juu ni kubwa sasa Mimi ni good listener inshort sipo tayari kuifanya
You want to go back in your comfort zone where there is relaxation.
Sina ushauri wa ulichoomba ila ninachoweza kusema vumilia utengeneze CV kipindi unatafuta kwingine, usikubali kukaa nyumbani.
 
Wakati unaikubali mwanzo mkuu ulijua nature yake?

Nakushauri sana kama kaka yako, USIIACHE HIYO KAZI! Fanya hiyo kazi angalau miezi 6 au mwaka alafu acha. Nakwambia hivi kwa sababu zifuatazo

1. Unless useme kama umepata kazi nyingine sasa hivi ambayo unahisi ni nzuri zaidi na kwa nature yako usivyochunguza mwanzo nayo ukiianza utaiona mbaya, kumbuka hakuna kazi rahisi duniani, ukishakuwa nayo itaanza kukuboa

2. Utamsikitisha sana mtu aliyekuunga na mzee na mzee mwenyewe. Hapa maana yake unakata network yako yote na kumbuka maisha sio tu kutafutiana kazi kuna na mengine ya kusaidiana

3. Mtaani ni pagumu sana jamaa. Aheri ukomae kukusanya madeni kuliko kutengeneza madeni wewe kudaiwa
 
Tupo mazingira tofauti na kumpigia simu ndio the only means of communication.
Hutokaa ufanikiwe endekeza ujinga mara mimi ni good listener sijui Godfearing,,,, baghdad blali lebanon mother Teresa.
Siku utapewa mgodi usimamie utaanza mara siwezi kusimamia wavuta bangi, mazingira machafu, dhuluma, tanganyika jeki wewe, ......Kuwa uyaone.... Mwenzako Majaliwa kajitoa muhanga kuokoa majeruhi wa ndege wewe unashindwa ata kumuheshimisha aliekutafutia kazi ...balimi baridi sana wewe
 
You want to go back in your comfort zone where there is relaxation.
Sina ushauri wa ulichoomba ila ninachoweza kusema vumilia utengeneze CV kipindi unatafuta kwingine, usikubali kukaa nyumbani.
Nashukuru sana Kwa ushauri wako. Ila kabla ya kuomba Kazi nilikuwa Nina harakati ambazo nafanya ndio hizohizo nataka kuziendelezea pale zilipoishia.
 
Back
Top Bottom