Naomba ushauri juu ya namna nzuri ya kujenga nyumba kwa ajili ya kupangisha tu

TensorFlow

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2020
Posts
993
Reaction score
1,286
Ndugu wajumbe,

Naombeni ushauri wa namna nzuri (economically optimal) ya kujenga nyumba kwa ajili ya kupangisha tu. Nalenga kupangisha wanafunzi wa chuo/shule, mabachelors, na watu wanaoanza maisha - mfano, mke na mme au mke mme na mtoto mmoja.

Je, naweza kujenga nyumba ya kupangisha kulenga hayo makundi ambayo baadaye naweza kuibadili na kuwa nyumba yangu ya kuishi?
 
Mkuu, ukitaka uenjoy, jenga nyumba ya kupangisha bachelors wenye pesa,
Jenga chumba jiko choo,
Chumba sebule jiko choo,

Hizo hapo juu zina pesa, pia soko lake ni zuri na wateja wake wana kipato hivyo hawasumbui sana kulipa,
Kama upo Dar,

Chumba jiko choo, utaweza kudai 80-100 inategemeana na eneo

Chumba choo sebule jiko utadai 100-150 kulingana na eneo
 
Kama upo dar,

Chumba jiko choo, utaweza kudai 80-100 inategemeana na eneo

Chumba choo sebule jiko utadai 100-150 kulingana na eneo
Ahsante Mkuu. Nadhani hii ya chumba - master, sebule na jiko ni nzuri zaidi.

Hii ujenzi wake unakuwaje, suppose nataka kuwa na nyumba za hivi sita (chumba - master, sebule na jiko), je, ni vizuri ziwe separate au kuna namna zinaunganika ?
 
Ina tegemea na kiwanja,
Ila vya kuzingatia,
Inabid ziungane, ila make sure wapangaji hawaonani, yan zisikae kama frame 😂😂😂
Ukiweza kuweka maget mawili au matatu inakuwa fresh, ili wapangaji wasionane 😂😂 wapangaji wana maneno 😂😂 so unaweza weka vyumba viwili viangalie mbele, viwili kulia viwili kushoto,

Epuka kuweka shared mita kwa watumiaji wengi, ukiweza weka wawili wawili, itakupa advantage kwenye kupata wateja wenye hela,
 
Ahsante Mkuu. Nadhani hii ya chumba - master, sebule na jiko ni nzuri zaidi.

Hii ujenzi wake unakuwaje, suppose nataka kuwa na nyumba za hivi sita (chumba - master, sebule na jiko), je, ni vizuri ziwe separate au kuna namna zinaunganika ?
vyumba vikishea ukuta unaokoa gharama,ila ushauri wangu mkuu,tuambie kwanza bajeti yako uliyopanga ni kiasi gani,na tuambie unategemea kupata kodi kiasi gani,ili tuone return itakuwaje.
 
Mimi nategemea kuwa na seti ya chumba - master, sebule, jiko, six times na return ya 150k kwa kila combination ya chumba, sebule, jiko. How much nataka kuinvest ndio bado sijapiga hesabu.

Hebu nipe uzoefu Mkuu, how much hii inaweza kunicost?
 
hapo unaongelea return ya 900k kwa mwezi...kuhusu ni kiasi gani inabidi uwekeweze ngoja injinia waje,je hela yako inafika milion 100?
 
Around mil 60.
Daaa kaka,milion 60 ndio ikupe return ya laki 9 kwa mwezi? hizo apartment sita unazotaka kujenga kwa hiyo hela zina ubora gani? Una uzoefu na ujenzi wowote? Anyway ngoja tupeane uzoefu,nilikuwa na pesa nilitaka kuiwekeza kama wewe,hiyo option ya kujenga nyumba ya wapangaji niliiwaza,lakini kiukweli nikaja kuona hailipi...unaweka hela nyingi kwenye ujenzi lakini return ni ndogo sana. Ngoja mainjinia waje lakini hiyo hela ukijenga nyumba standard unaweza kupata apartment mbili au tatu tu. Kwahiyo tegemea kuingiza 300k mpaka 450k kwa mwezi. Ujenzi ni gharama sana sa hivi.
 
Huku mbezi kuna nyumb imejengwa kw bajeti ya milion 40 ila inatoa return ya 600k kwa milango mnne
Ni kwamba kajenga nyumba moja kubwa ila ndan yake kuna chumba sebur choo na jiko na kila mtu anatumia mlango wake na anaingilia upande wake wanachowez kushare ni uwanja wa kuanikia nguo
Unawez kujenga self servant kota ya chumba sebure choo na jiko weka bajeti ya milion kum kila kimoja ambapo utapata nyumba 6 kam upo location nzuri unavuta 150k alaf shega
 
Mimi nategemea kuwa na seti ya chumba - master, sebule, jiko, six times na return ya 150k kwa kila combination ya chumba, sebule, jiko. How much nataka kuinvest ndio bado sijapiga hesabu.

Hebu nipe uzoefu Mkuu, how much hii inaweza kunicost?
Kwa hesabu za haraka fanya hivi at the minimum na kuassume apartment zimeungana; (m=meter, sqm=square meters)
1. Master bedroom 3.5x4m=14sqm (upate room 3x3m na washroom 1x2m na kabati 0.5x2m)
2. Sitting room 3.5x4m=14sqm
3. Jiko 2.5x2m=5sqm
4. Entry porch/balcony/baraza/upenuni 1.5x2m=3sqm
5. Walls thickness (0.23m) not considered; most of other things are kept constant (plot size, landscape, location, availability of materials etc)

So roughly hapo jumla kwa apartment moja=36sqm

36x6=216sqm

Approx ujenzi per sqm ni 500k

216x500,000=108,000,000
 
Hii Biashara hua naona ni Kwa matajiri ambao tayari wanapesa na kwamba hapa ni mahala pa kuhifadhi pesa na sio "kutafutia" pesa.... Yaani uwekeze 108m upate return ya 900k ambapo ni around 10.8m kwa mwezi... Kwamba inahitajika zaidi ya miaka kumi kurejesha tu fedha yako.... Noway!!

108m Ina alternative nyingi Sana ya quick return!
 
Kwa ukubwa wa eneo nadhani haitakuwa issue, ni kama sqm 1500.
 
Hii Biashara hua naona ni Kwa matajiri ambao tayari wanapesa na kwamba hapa ni mahala pa kuhifadhi pesa na sio "kutafutia" pesa.... Yaani uwekeze 108m upate return ya 900k ambapo ni around 10.8m kwa mwezi... Kwamba inahitajika zaidi ya miaka kumi kurejesha tu fedha yako.... Noway!!

108m Ina alternative nyingi Sana ya quick return!
Kusema ukweli ni msala. Miaka 10+, bado gharama za matengenezo. Kuna muda nawaza ukumbi wa sherehe. Sijui hilo nalo likoje!
 
Mimi nategemea kuwa na seti ya chumba - master, sebule, jiko, six times na return ya 150k kwa kila combination ya chumba, sebule, jiko. How much nataka kuinvest ndio bado sijapiga hesabu.

Hebu nipe uzoefu Mkuu, how much hii inaweza kunicost?
Mtu yeyote atakayekupa ushauri bila kujua location ya hiyo project, usimtilie maanani sana.
 
Kigamboni, maeneo ya Mwembe Mdogo.
Bado hayo maelezo hayatoshi kupewa ushauri nzuri. Kuna apartments nyingi mitandaoni zinauzwa.
Tatizo ni location.

Aina ya watu wanaokaa mwembe Mdogo.
Idadi Yao.
Umbali kutoka barabara kuu, umeme na maji upatikanaji wake pamoja na huduma za jamii.
Wastani wa kipato na source ya kipato Chao.
 
Back
Top Bottom