Naomba ushauri juu ya namna nzuri ya kujenga nyumba kwa ajili ya kupangisha tu

Naomba ushauri juu ya namna nzuri ya kujenga nyumba kwa ajili ya kupangisha tu

Kwa hesabu za haraka fanya hivi at the minimum na kuassume apartment zimeungana; (m=meter, sqm=square meters)
1. Master bedroom 3.5x4m=14sqm (upate room 3x3m na washroom 1x2m na kabati 0.5x2m)
2. Sitting room 3.5x4m=14sqm
3. Jiko 2.5x2m=5sqm
4. Entry porch/balcony/baraza/upenuni 1.5x2m=3sqm
5. Walls thickness (0.23m) not considered; most of other things are kept constant (plot size, landscape, location, availability of materials etc)

So roughly hapo jumla kwa apartment moja=36sqm

36x6=216sqm

Approx ujenzi per sqm ni 500k

216x500,000=108,000,000
Daaah sawa hizi hesabu, ila watu wote wangepigiwa hesabu hizi wasingejenga.
Hivi mnajua ni watu wanagapi tumejenga na milioni 10-30 nyumba za kupanga, tena tukiwa hatuna hela.
Mtu ana milioni 60 ashindwe kufanya project ya nyumba za kupanga acheni bwana basi.
 
Kweli kabisa. Biashara ya kupangangish nyumba unafanya investment kubwa ila Return yake ndogo. Let's hapo hata kiwanja bado.

So ku invest 60M kwa return ya 900K, Ambayo ni 9M kwa mwaka, means hadi ifike miaka 7 ndipo uanze kupata faida.

Kuna biashara zenye majina makubwa na faida kidgo.

Hiyo hela si bora utupie Utt au ununue Bonds, fedha yako inabaki na unapata gawio?

Kama bado una akili ya kutaka kujenga sikushauri, Secure viwanja, vifuge, hela ingine invest passively.

Otherwise jenga A frame houses, ziweke Airbnb. Hapo utacheza na 20M kwa each, ukitumia materials kama Interlocking bricks, plastic woods au Mega panel.. ukiwa navyo viwili unaendelea kujitafuta.

Jilipue fanya tafiti ya biashara zingine, usiweke zaidi ya 5M after kuijua hiyo biashara. Anzia mwisho kuja mwanzo, anzia ku network na masoko.
Mkuu hii biashara ya Air bnb ni nzuri?
 
Hivi investment yoyoye lengo ni kuwa tajili ,? Uwekezaji wka nyumba faida yake siyo ya haraka lakini Ina matokeo chanya kwa watoto ,ardhi inapaa thamani Kila siku,siyo ili uuze upate pesa,ni ili kizazi/watoto wako waje kuwa na pakuanzia pazuri

Wazungu wanatoa misaada ya barabara zinazoenda kwenye rasilimali Fulani Kisha wanapeleka ramani kwao kutunza kwenye maktaba za familia/nchi, baada ya miaka 100 watoto wanarudi kusambaza injili eneo lilelile ambalo mababu walichora ramani, sisi waafrika Huwa tunapenda kuishi Hadi maisha ya vitukuuu, tukifa tunakufa na Kila kitu,

Uwekezaji wa ardhi nauunga mkono kwa asilimia mia Moja,yes fanya na mengine ,ila kwa jinsi tunavozaana ,kuboreka kwa huduma za afya ya uzazi na Akina mama,vifo vinakuja kuwa vichache sana, population ikikuwa hitaji la kwanza ni aridhi, Sasa kama ukiwa na hekima ya kuwekeza katika ardhi ,naamini wajukuu watakutangaza kuwa mwenyeheri💯
 
Kweli kabisa. Biashara ya kupangangish nyumba unafanya investment kubwa ila Return yake ndogo. Let's hapo hata kiwanja bado.

So ku invest 60M kwa return ya 900K, Ambayo ni 9M kwa mwaka, means hadi ifike miaka 7 ndipo uanze kupata faida.

Kuna biashara zenye majina makubwa na faida kidgo.

Hiyo hela si bora utupie Utt au ununue Bonds, fedha yako inabaki na unapata gawio?

Kama bado una akili ya kutaka kujenga sikushauri, Secure viwanja, vifuge, hela ingine invest passively.

Otherwise jenga A frame houses, ziweke Airbnb. Hapo utacheza na 20M kwa each, ukitumia materials kama Interlocking bricks, plastic woods au Mega panel.. ukiwa navyo viwili unaendelea kujitafuta.

Jilipue fanya tafiti ya biashara zingine, usiweke zaidi ya 5M after kuijua hiyo biashara. Anzia mwisho kuja mwanzo, anzia ku network na masoko.
Umenena vyema aisee mimi nakuunga hapo kwenye viwanja .... nataman sana kuwa na shamba kubwa haijalishi umbali,

Just imagine 50M uwekeze kwenye ufugaji mbuzi/ng'ombe kisasa then io miaka mitano utakua wapi?

NB hela nyingi sio ya ununuzi wa ng'ombe ila ni uandaaji wa ranch ya kisasa... etc

yaani wewe acha tu.
 
Exactly hapo umeongea point, I wish ningekuwa nazo mimi 60M ningetanua sana mradi wangu wa dairy cattle, banda kuuubwa ng'ombe wachache.
 
Hii Biashara hua naona ni Kwa matajiri ambao tayari wanapesa na kwamba hapa ni mahala pa kuhifadhi pesa na sio "kutafutia" pesa.... Yaani uwekeze 108m upate return ya 900k ambapo ni around 10.8m kwa mwezi... Kwamba inahitajika zaidi ya miaka kumi kurejesha tu fedha yako.... Noway!!

108m Ina alternative nyingi Sana ya quick return!
Unatania wewe. 10.8 kwa mwezi? Au umekosea ulitaka kusema kwa mwaka?
 
Complicate??
Yaani unataka kujijenga apartments na hujui lolote kuhusu hiyo location?
Mkuu kama haupo tayari kujifynza na kufanya utafiti achana na biashara hizi mbili.
1. Real estate.
2. Transportation
Ila unaweza kubahatisha.
Siyo hizo tu ni biashara yoyote. Hakuna kitu kibaya kama huna plan na correct info yako kichwani kwenye kuanzisha biashara yoyote. Haya mambo unauliza halafu watu wanaanza kukuyumbisha eti bora ufanye hili, eti hapa kurudisha fedha itachukuwa muda na kila aina ya bla bla halafu wewe unayumbayumba ni hatari hasa. Wengi wanafeli kwa sababu ya hili. Sikatai kuulizia lakini uliza ili kupanua mawazo na siyo kuuliza kutaka kufanya kitu ambacho hujawahi fanya na unayumbishwa yumbishwa kwa moto wa kibatali kwenye upepo.
 
Exactly hapo umeongea point, I wish ningekuwa nazo mimi 60M ningetanua sana mradi wangu wa dairy cattle, banda kuuubwa ng'ombe wachache.
Unajua boss vijana tuna kimbilia kujenga kwenye 20 kwa 20 tunaacha mambo ya msingi

Imagine Mungu kakupa neema umepata hela umejenga nyumba yako unakaa mwenyewe haikulipi chochote .... ila hela io io ungeweza zama nayo porini huko msata chalinze mbeya morogoro anywhere....

Ukafanya project moja matata sana mfano kama ni maziwa unayaongezea thamani kabisa, nyama ivyo ivyo etc...
 
Mimi nategemea kuwa na seti ya chumba - master, sebule, jiko, six times na return ya 150k kwa kila combination ya chumba, sebule, jiko. How much nataka kuinvest ndio bado sijapiga hesabu.

Hebu nipe uzoefu Mkuu, how much hii inaweza kunicost?
Eneo/mkoa gani?
 
Unajua boss vijana tuna kimbilia kujenga kwenye 20 kwa 20 tunaacha mambo ya msingi

Imagine Mungu kakupa neema umepata hela umejenga nyumba yako unakaa mwenyewe haikulipi chochote .... ila hela io io ungeweza zama nayo porini huko msata chalinze mbeya morogoro anywhere....

Ukafanya project moja matata sana mfano kama ni maziwa unayaongezea thamani kabisa, nyama ivyo ivyo etc...
Shida kubwa tuliyonayo watanzania ni Imani kwamba maendeleo ni lazima ujenge nyumba ya kuishi either uishi wewe mwenyewe au upangishe. Lakini hatuna mentality ya kusema ngoja niwe na stable business yenye return nzuri ili uweze kuishi vizuri na kufanya biashara nyingine.

Sasa uweke 60M kwenye apartments itarudi lini? Yani labda useme pesa hiyo hauna cha kufanyia utaitumia vibaya na biashara sio hobby basi ujenge tu.
 
Kweli kabisa mkuu,
 
Jenga ujengavyo ila make sure kuwa huko ndani unaweka hizi sections zifuatazo.

Chumba kimoja kikubwa kwa single bedroom kisipungue futi za mraba 12. Then make sure kama ni chumba single au chumba na sebule kisikose choo na jiko vyote viwe ndani ya chumba au nyumba.

Ujenzi wa sasa unatakiwa sana kuzingatia uwepo wa jiko la ndani, choo, mita ya kujitegemea na maji ya uhakika yaani kuwe na tenki la maji kuanzia lita 5,000 au lita 10,000.

Sasa shida wajenga nyumba huwa wanajenga bora liende ila wanasahau kuwa watu wanakuja kuishi hapo mahala na wanahitajika kupata privacy ya kutosha plus vyumba viweze kuaccomodate utulivu wa muda mrefu na kumpa mpangaji mazingira ya kujipanga kuwa na kwake na kujijemga kiuchumi.
 
Ahsante Mkuu. Nadhani hii ya chumba - master, sebule na jiko ni nzuri zaidi.

Hii ujenzi wake unakuwaje, suppose nataka kuwa na nyumba za hivi sita (chumba - master, sebule na jiko), je, ni vizuri ziwe separate au kuna namna zinaunganika ?
Weka ziwe separate. Mambo ya kuunganisha nyumba inakuwa na show ya hovyo. Kwanza hata miundo mbinu inakuwa haijakaa poa. Vema ukiseparate makazi.
 
Hii Biashara hua naona ni Kwa matajiri ambao tayari wanapesa na kwamba hapa ni mahala pa kuhifadhi pesa na sio "kutafutia" pesa.... Yaani uwekeze 108m upate return ya 900k ambapo ni around 10.8m kwa mwezi... Kwamba inahitajika zaidi ya miaka kumi kurejesha tu fedha yako.... Noway!!

108m Ina alternative nyingi Sana ya quick return!
Point. Ukitaka kujua ukweli ni uambiwe kaa hapo mezani tupange bajeti ya matumizi halafu tubashiri mapato. Ndipo utaelewa.
 
Mkuu, ukitaka uenjoy, jenga nyumba ya kupangisha bachelors wenye pesa,
Jenga chumba jiko choo,
Chumba sebule jiko choo,

Hizo hapo juu zina pesa, pia soko lake ni zuri na wateja wake wana kipato hivyo hawasumbui sana kulipa,
Kama upo Dar,

Chumba jiko choo, utaweza kudai 80-100 inategemeana na eneo

Chumba choo sebule jiko utadai 100-150 kulingana na eneo
Leta ramani
 
Ndugu wajumbe,

Naombeni ushauri wa namna nzuri (economically optimal) ya kujenga nyumba kwa ajili ya kupangisha tu. Nalenga kupangisha wanafunzi wa chuo/shule, mabachelors, na watu wanaoanza maisha - mfano, mke na mme au mke mme na mtoto mmoja.

Je, naweza kujenga nyumba ya kupangisha kulenga hayo makundi ambayo baadaye naweza kuibadili na kuwa nyumba yangu ya kuishi?
Nimekucheck kwa mawasiliano Zaidi
 
Back
Top Bottom