Naomba ushauri kuhusu biashara Spare za Pikipiki

Kaka habari
Shukran kwa ushauri nimefanikiwa kuanza biashara na mtaji wa 5m ingawa kwa spare huu ni mtaji mdogo sana
Nimejaribu kwa msaada wa fundi kununua vifaa vichache vichache vya muhim sana
Na pia nimefanikiwa kupata fundi mzuri wa pikipiki Mungu ni mwema
Safari ndio inaanza Mungu atusaidie kufika malengo
Nitaleta mrejesho wa biashara so far inaonekana ni biashara nzuri ukipata location nzuri na fundi mzuri wa kuaminika na bodaboda
Shukran
Kila lenye kheri kwako
 
Wauza mwenyewe au umeweka mtu
 
Hello lucy, me ndo nimeanza rasmi hii biashara, mtaji nimeanza na 10m duka ni kigamboni dar es salaam, mzigo nimechukua kariakoo duka linaitwa sayuni lipo cate hotel.. hili duka lauza spea kwa bei nzuri, na kwa mtaji wa m10 kwa duka la spea za pikipiki na bajaji duka linakua linapendeza na unakua na spea zote za muhimu... Pia dukan kuna kama gereji kwa ajili ya kutengenezea pikipiki(kumbuka hii biashara inabidi uwe na fundi mzuri unamuiba mahala anakua anafanyia ufundi wake dukani kwako.. fundi humlipi analipwa na wanaokuja kutengeneza vyombo vyao.. na kijiwe kikichangamka fundi anatakiwa akupe kiasi fulan kwakua gereji ni yako..

Nb; fundi wengi wanapenda duka lenye vitu vyote ili kuwe na uhakika wa kazi..

Pia inapendeza ukiweka na compressor ya kujazia upepo ili kazi za panja zifanyike.. mengine ntashare kadiri navo pata uzoefu..
Hii ndio spirit ambayo Watanzania tunatakiwa tuwe nayo. Hongera sana Mkuu na Mungu akubariki.
 
Mkuu maendeleo ya biashara yapoje?

Naendelea Vyema kaka nilianza mapema February na mtaji wa 5m na maendeleo ni makubwa sana namshukuru Mungu,,,ingawa hapo kati changamoto kubwa nimekumbana nayo ni mafundi tu ila nimejifunza sana na kuadvance
Pia muda huo nimejifunza kukisoma na kuelewa kila spea kwenye pikipiki zote kuanzia boxer,tvs,haoujue,gn za kawaida n.k spea zake, inavyofanya kazi na mahali inapofungwa.

Kiufupi biashara ni nzuri sana ila inahitaji umakini sana na eneo zuri lenye mzunguko wa kutosha faida lazima uione.
 
Pambana pambana
 
Back
Top Bottom