Naomba ushauri kuhusu biashara Spare za Pikipiki

Naomba ushauri kuhusu biashara Spare za Pikipiki

Kaka habari
Shukran kwa ushauri nimefanikiwa kuanza biashara na mtaji wa 5m ingawa kwa spare huu ni mtaji mdogo sana
Nimejaribu kwa msaada wa fundi kununua vifaa vichache vichache vya muhim sana
Na pia nimefanikiwa kupata fundi mzuri wa pikipiki Mungu ni mwema
Safari ndio inaanza Mungu atusaidie kufika malengo
Nitaleta mrejesho wa biashara so far inaonekana ni biashara nzuri ukipata location nzuri na fundi mzuri wa kuaminika na bodaboda
Shukran
Hongera kwa UTHUBUTU... Nadhani mpaka sasa utakua na uzoefu walau wa yule mtu anaetaka kuanza biashara hiyo, naomba ushare kwenye haya:

1: Ulianza kudeal na Uuzaji wa vipuri vya Kampuni zipi za pikipiki?(zitaje kwa majina)

2: Je, Ulianza kuuza spea na oil kwa pamoja hapo mwanzo? Ni spare zipi na/au oil zipi ulianza nazo?(zitaje kwa majina)

3: Chimbo ulilokuaunatoa/unalotoa spea na/au oil? Ni lipi

4: Gharama TRA zimekaaje?
AHSANTE...
Naomba kuwasilisha.
 
Personal nilianza na duka kubwa la urembo wa magari kwa mtaji wa 15M.

Mungu akisaidia by feb-march 2023, ntaongeza duka la spare na urembo wa Bodaboda/bajaji.

Mungu ni mwema business hizi hazimtupi mtu.
Nitaomba mawasiliano ya mahali unapochukua urembo wa pikipiki
 
Kiongozi samahani kwani spare kwa kuanzia huwezi kuanza bila kuweka fundi?

Bila fundi uongo kama unauza rejareja, mana boda hawez nunua spea akapeleka kwa fundi ambaye yuko kijiwe kingine ambako nako kunauza spare
Muhim kwa reja kuwa na fundi ili kurahisisha mzunguko,
 
Naendelea Vyema kaka nilianza mapema February na mtaji wa 5m na maendeleo ni makubwa sana namshukuru Mungu,,,ingawa hapo kati changamoto kubwa nimekumbana nayo ni mafundi tu ila nimejifunza sana na kuadvance
Pia muda huo nimejifunza kukisoma na kuelewa kila spea kwenye pikipiki zote kuanzia boxer,tvs,haoujue,gn za kawaida n.k spea zake, inavyofanya kazi na mahali inapofungwa.

Kiufupi biashara ni nzuri sana ila inahitaji umakini sana na eneo zuri lenye mzunguko wa kutosha faida lazima uione.

Natumai biashara yako imetimiza mwaka mmoja sasa hongera sana.

Vipi maendeleo kiongozi...?
 
Safi sana mkuu na mimi nitakutafuta unipe maarifa zaidi nina mpango wa kufanya hii biashara ingawa lengo langu ni kufikia kuuza vipuri, urembo na matengenezo kwa magari lkn kutokana na mtaji pia na mazingira nimeona nianze kwa pikipik na bajaji nikiwa na weka spare za magari kidogo kidogo maana kwa sasa nimehamia mkoani tabora. Changamoto niliyokuwa nayo ni kupata location nzuri lkn namshkru mungu nimepata eneo ambalo tumelewana na mwenye kiwanja nijenge then niweke biashara yangu alafu tutakatana kwenye kodi . Tathimin ya fundi wangu leo kwa ujenzi wa chumba cha biashara (frame ) pamoja na store yake ambayo itatumika pia kulala mtu kwajili ya ulinzi ni 3.5m inakamilika kila kitu. 🙏🙏🙏 Tuombeane uzima.

Mkishakatana kwenye Kodi kidogo kidogo baada ya hapo frame inakuwa yake ama...?
 
Bila fundi uongo kama unauza rejareja, mana boda hawez nunua spea akapeleka kwa fundi ambaye yuko kijiwe kingine ambako nako kunauza spare
Muhim kwa reja kuwa na fundi ili kurahisisha mzunguko,
But mm nataka niwe na ofisi kwanza nione inakuaje natumai sitochelewa kumpata fundi
 
Utajichelewesha hivyo ndugu! Jitahid uwe na fundi ili matatizo na hamu zao wateja wamalize hapo hapo!...
Nikitaka fundi nampataje maana wengi ni wapigaji akiona tena unashida nae sana anakua na kibri
 
Nikitaka fundi nampataje maana wengi ni wapigaji akiona tena unashida nae sana anakua na kibri
Unapotaka cha uvunguni sharti uiname!.. kwa maana wakat mwingine unaweza hata kumpa kiasi flani cha fedha kumtoa sehemu moja fundi kwenda nyingine. Na sio kuwa wanaringa ila eneo utakalomkuta kumbuka anakuwa na wateja wake hivyo basi unavyomuamisha atakuwa anakwenda kuanza maisha mapya kwahyo ndiyo maana wengi wao hiko wanakikwepa! Mfano mim fundi wangu kumtoa sehemu aliyokuwepo na kumleta mazingira yangu ilinibid nimpangie hadi chumba kwa miez 3 na posho kidogo nilimpa yote hiyo kujitengenezea mazingira!... Nadhan nimekujibu!...
 
Mkishakatana kwenye Kodi kidogo kidogo baada ya hapo frame inakuwa yake ama...?
Ndiyo kwa maana kiwanja ni chake . Kinachofanyika tu ni kwamba gharama ya kujenga frame inatoka kwangu kwa kuwa yeye kwa sasa hana pesa ya kujenga . Hivyo basi gharama inayotumika kujenga ni sawa na gharama ambayo nimelipia kodi kwa muda flan au miaka kadhaa lkn tumetengeneza mkataba wa makubaliano hayo kwa wanasheria maana huwezi jua Kwa badae mmoja wetu akaingia tamaa au mmoja wetu akatangulia mbele za haki basi familia zetu zibaki zikitambua hilo kupitia mkataba. Pia kwa kuwa itachukua muda mrefu pasipo kupokea yeye kodi basi tulikubaliana kodi ya frame nusu itakuwa inapunguza deni la kujenga alafu nusu anapokea.

Baada ya muda wa makubaliano ukishaisha nitaanza kulipa kodi kama kawaida na yawezekana pia ikapanda kulingana na thaman ya muda huo.
 
Tuchukulie umejenga kwa milioni moja hiko chumba kimoja, unatoa laki tano unampa yeye it means si ni milioni moja na nusu au sijakuelewa vizuri kiongozi...?
 
Back
Top Bottom