Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila LA kheri mkuuMi naitaji kuanzisha hi biashara ya spare za pikpki ila Nina mtaji wa milion3 natafta location na fundi alaf Bei ya compressor ikiwa poa naitaji niiweke nayenyewe
Safi sana mkuu na mimi nitakutafuta unipe maarifa zaidi nina mpango wa kufanya hii biashara ingawa lengo langu ni kufikia kuuza vipuri, urembo na matengenezo kwa magari lkn kutokana na mtaji pia na mazingira nimeona nianze kwa pikipik na bajaji nikiwa na weka spare za magari kidogo kidogo maana kwa sasa nimehamia mkoani tabora. Changamoto niliyokuwa nayo ni kupata location nzuri lkn namshkru mungu nimepata eneo ambalo tumelewana na mwenye kiwanja nijenge then niweke biashara yangu alafu tutakatana kwenye kodi . Tathimin ya fundi wangu leo kwa ujenzi wa chumba cha biashara (frame ) pamoja na store yake ambayo itatumika pia kulala mtu kwajili ya ulinzi ni 4.5m inakamilika kila kitu. 🙏🙏🙏 Tuombeane uzima.Hello lucy, me ndo nimeanza rasmi hii biashara, mtaji nimeanza na 10m duka ni kigamboni dar es salaam, mzigo nimechukua kariakoo duka linaitwa sayuni lipo cate hotel.. hili duka lauza spea kwa bei nzuri, na kwa mtaji wa m10 kwa duka la spea za pikipiki na bajaji duka linakua linapendeza na unakua na spea zote za muhimu.
Pia dukan kuna kama gereji kwa ajili ya kutengenezea pikipiki(kumbuka hii biashara inabidi uwe na fundi mzuri unamuiba mahala anakua anafanyia ufundi wake dukani kwako.. fundi humlipi analipwa na wanaokuja kutengeneza vyombo vyao na kijiwe kikichangamka fundi anatakiwa akupe kiasi fulan kwakua gereji ni yako.
Nb; fundi wengi wanapenda duka lenye vitu vyote ili kuwe na uhakika wa kazi.
Pia inapendeza ukiweka na compressor ya kujazia upepo ili kazi za panja zifanyike.. mengine ntashare kadiri navo pata uzoefu.
Hello lucy, me ndo nimeanza rasmi hii biashara, mtaji nimeanza na 10m duka ni kigamboni dar es salaam, mzigo nimechukua kariakoo duka linaitwa sayuni lipo cate hotel.. hili duka lauza spea kwa bei nzuri, na kwa mtaji wa m10 kwa duka la spea za pikipiki na bajaji duka linakua linapendeza na unakua na spea zote za muhimu.
Pia dukan kuna kama gereji kwa ajili ya kutengenezea pikipiki(kumbuka hii biashara inabidi uwe na fundi mzuri unamuiba mahala anakua anafanyia ufundi wake dukani kwako.. fundi humlipi analipwa na wanaokuja kutengeneza vyombo vyao na kijiwe kikichangamka fundi anatakiwa akupe kiasi fulan kwakua gereji ni yako.
Nb; fundi wengi wanapenda duka lenye vitu vyote ili kuwe na uhakika wa kazi.
Pia inapendeza ukiweka na compressor ya kujazia upepo ili kazi za panja zifanyike.. mengine ntashare kadiri navo pata uzoefu.
Hapana but hua naagiza bidhaa nyingine
Safi sana mkuu na mimi nitakutafuta unipe maarifa zaidi nina mpango wa kufanya hii biashara ingawa lengo langu ni kufikia kuuza vipuri, urembo na matengenezo kwa magari lkn kutokana na mtaji pia na mazingira nimeona nianze kwa pikipik na bajaji nikiwa na weka spare za magari kidogo kidogo maana kwa sasa nimehamia mkoani tabora. Changamoto niliyokuwa nayo ni kupata location nzuri lkn namshkru mungu nimepata eneo ambalo tumelewana na mwenye kiwanja nijenge then niweke biashara yangu alafu tutakatana kwenye kodi . Tathimin ya fundi wangu leo kwa ujenzi wa chumba cha biashara (frame ) pamoja na store yake ambayo itatumika pia kulala mtu kwajili ya ulinzi ni 3.5m inakamilika kila kitu. [emoji120][emoji120][emoji120] Tuombeane uzima.
Nina mwaka nimeanza biashara hii kiukweli ni nzuri faida unaiona japo changamoto zipo nyingi hasa kwa mafundi na bodaboda wenyewe, huwezi kukaa dukani siku zote so mda unatoka ukimuacha fundi kama sio muaminifu lazima akupige ukija kwa bodaboda ukimkopesha ndo umemfukuza ukimnyima pia ndo umempoteza. Wanaoanza hii biashara inabidi mtafute sehem wanayouza spare kwa bei rahisi kama hilo duka la sayuni alilolisema mchangiaji vifaa vyake ni bei rahisi kiukweli ndio duka langu ninalonunulia spare zangu kwa sasa.
Unaongelea kuagiza mzigo china au yeye mwenyewe aende chinaNa mimi niongezee
Mtaji ukikua ugawe nusu nunua kkoo nusu agiza China huu wa china ukiagiza round tatu tu wewe sio mwenzetu
Bado unaitaji kuagiza? ?tuwasilianeKaka unafahamu lolote kuhusu kuagiz mzigo china?? Mana huko nasikia kupigwa nje nje
Una connection yoyote??
KuagizaUnaongelea kuagiza mzigo china au yeye mwenyewe aende china
Mhhh sawaKuagiza
Safi sana kiongozi. Piga kaziMi biashara nafanyia huku kibaha maporini kwenye mikaa.Wateja wangu wengi Ni wabeba mikaa kwa pkpk(Busta) spea wanazonunua Sana Ni original za haojue,sinoray na fekon.Na Bei zake sio mbaya sn ukinunua direct kutoka kwao.
Unazichukulia wap ( dukani) chief hizo spare!Mi biashara nafanyia huku kibaha maporini kwenye mikaa.Wateja wangu wengi Ni wabeba mikaa kwa pkpk(Busta) spea wanazonunua Sana Ni original za haojue,sinoray na fekon.Na Bei zake sio mbaya sn ukinunua direct kutoka kwao.
Unazichukulia wap chief hizo spare original!
Ni faraja sana kusikia hivyo... tunaomba pia kama hamtojali mtujuze ni spea zipi zinauza haraka ili mtu anaeanza awe na uhakika mzuri wa kuuza akiwa na mtaji mdogoNaendelea Vyema kaka nilianza mapema February na mtaji wa 5m na maendeleo ni makubwa sana namshukuru Mungu,,,ingawa hapo kati changamoto kubwa nimekumbana nayo ni mafundi tu ila nimejifunza sana na kuadvance
Pia muda huo nimejifunza kukisoma na kuelewa kila spea kwenye pikipiki zote kuanzia boxer,tvs,haoujue,gn za kawaida n.k spea zake, inavyofanya kazi na mahali inapofungwa.
Kiufupi biashara ni nzuri sana ila inahitaji umakini sana na eneo zuri lenye mzunguko wa kutosha faida lazima uione.
Nachukulia kkoo kwenye maduka ya sinoray,haojue na ht hon lg.Wana maduka yao pale kkoo ht ukitaka namba ntakupaUnazichukulia wap ( dukani) chief hizo spare!