Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Kweli alikuroga na mganga wake alisha kufa
 
Siku 2 rumande na mkeo wa ndoa hakujua upo wapi? Hakuhangaika kukutafuta?
Itakuwa ni wale wanawake wasio ulizaga lolote, mie najua Mme nyumba saa 10-11 yupo nyumbani, muda ukizidi tu lazima tuambiane yupo wapi sasa ulale lupango nisijue hakuna kitu kama hicho!
 
Kama waishi pamoja kwanini usifanye upelelezi wako uwakamate huko huko kwao mwambie mbele ya wazazi wake mie kuanzia Leo ndiyo basi, watoto wachague kwangu au kwa mama yao, kwanza ni wanawake wakiolewa tu basi, kwanza umwambie mkapime DNA huenda huyo mdogo si wako kaka mkuu.
 
Sasa huko ndiko unakolitafuta, angalia huyo kimada wako yupo tayari kwa lolote na inaonekana ulimng'ang'ania sana
 
Mwanamke akimkinai mwanaume kurudi katika hali ya kawaida ni ngumu sana, baba achemshe kichwa
 
Wee nawe ndio umechanganyikiwa Sasa miaka 50 ndii unaona ame expire?
Miaka 50 mbona anadai
Wapo wazee wa 70 na wako fit
Mtu ameeleza shid za mke wake SI umsikilize
Tatizo jf wajuaji mko wengi
 
Wanapunyuliwa na michepuko na maradhi juu mwisho wanawapelekea wake zao nyumbani, lakini MUNGU huwa anayaona machozi ya wanawake, halafu huwa hawaoni mifano ya walio watangulia, ndiyo ile sikio lakufa halisikii dawa
 
Masikini alikuona bwege, kaka embu nenda kanisani kwako tubu tena mbele ya mkeo wakuombee ufahamu wako urudi, ningekuwa mkeo ningehamia kwenye hiyo nyumba nimuone huyo kirukanjia wako, watu mnawake wavumilivu kupitiliza
 
Wee nawe ndio umechanganyikiwa Sasa miaka 50 ndii unaona ame expire?
Miaka 50 mbona anadai
Wapo wazee wa 70 na wako fit
Mtu ameeleza shid za mke wake SI umsikilize
Tatizo jf wajuaji mko wengi
Wewe ndo mjuaji hafu humu JF wababu na wabibi tuko wengi na wewe umeamini huo umri shauri yako
 
Yaani mama yako kukwambia uwe unakaa na wenzio huko nawe ukaingia mzima mzima, mama yako aliona mkeo atakutawala mpaka uwasahau wao, wazazi wengi huona wivu kwa watoto wao kwanini mtoto asiwasikilize wao badala yake penzi lote kwa mkewe na ndiyo maana alishakuja mpaka kwa huyo sijui nyumba ndogo ambayo unalala Miguu nje kichwa ndani
 
Dododo tena yamekuwa hayo mmmmm!!!?
 
Haaa haaa haaa wanakula dozi zakutosha [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Yaani kwasababu kaondoka ana mwezi ndiyo unaona afadhali? Daa si bure wewe badala yakuweka msimamo nakuona wewe unasubili uachwe si wewe kuacha MUNGU wangu pole sana, nakushauri ongea na mkeo vizuri nendeni kwa mchungaji wakakutoe hilo pepo si hali yakawaida hiyo, huyo hakuachi Bali anakuchezesha segere, huko anakula bata na anayempenda wewe unafanywa zuzu samahani lakini, embu omba kwa kufunga angalau siku 3 MUNGU akupe chakufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…