Ndugu Ahsante sana kwa mawazo na na ushauri,
Kuhusu hapo namba 1
Mama yangu hakunitaka niwe Na mchepuko,
Ila kipindi hicho nilikuwa bado kijana sana na ndio nimepata mtoto wa kwanza,
Alitaka tu kunifunza kama mzazi namna nzuri ya mtoto wa kiume kuishi,
Maana aliona kila nikitoka kazini break ya kwanza ni home
Sasa kwa uzoefu wake wa maisha aliona sio sawa
Ni bora nikitoka kazini niwe kwanza na vijana wenzangu huko kubadilishana mawazo
Kama umegundua hii tabia yangu moja kwa moja nyumbani labda Ndio imenifikisha hapa kutawaliwa na mke, maana mawazo mengi ya kihuni au namna ya kumnyanyasa mwanamke nilikuwa sina ( yaani ile roho mbaya ya kiume)
Namba mbili 2 hapo,
Mimi ni mpiganaji wa kutaka kumiliki mali
Ndio maana Alhamdulilah maisha yangu na uwekezajinimejitosheleza hilo sina wasiwasi nalo
Nikisema leo hapa Dar niuze Mali zangu zote leo nirudi kijijini, uhakika wa 700 m upo, na malipo
Nikiendeleza maaneo yangu angalau niongeze kama vyumba 30 vya wapangaji
Naiona 1 B, inaninyemelea,
Kwa hiyo uwezo wa kuachia mali yangu kumpa mtu ambaye kaniumiza NO tena nasema kwa sauti NO, nitaenda mpaka kushtakia kwa Mungu,
Maana mali yangu ninauhakika sijamdhulumu mtu yeyote,
Ni damu na nguvu yangu.
Hapo mwanzo nilisema kama huyu mtu asingeonyesha namna yoyote ya kutaka kuizungumzia nyumba hasa hasa wakati wa ugonvi,
Na kukawa na mwelekeo wa kuachana kwa roho yangu ilivyo ningemuachia nyumba,
Ila mpaka nimegundua ana mwanaume bado kweli nimwachie nyumba au tugawane nusu kwa nusu Hapana, big Hapana
Mwaka 2018, yalipozidi kuwa magumu na kunilaza polisi, kesho yake alikuwa kunitoa yeye na ndugu zake 3 dada zake wawili na Baba yake wa hiari wahapa Dar, ambaye kusema kwa kw a miaka yote niliyoishi na huyu mwanamke sijawahi hata kusikia akimzungumzia
Baada ya kinitoa, alishauliwa asilale nyumbani kwangu mpaka nitulie maana ninaweza kumfanyia kitu mbaya,
Sasa wakati tunaagana yule baba akashauri tufanye kitu kama kikao nyumbani kwangu kesho yake,
Tukaagana na mimi nikaridhia nikaona sasa ni muda mzuri wa kutoa yamoyoni yote mbele ya ndugu zake na huyo baba
Wakati mimi nimefika nyumbani, nikampigia yule mdogo wake kwa ajili ya matayalisho ya chakula kwa wageni kesho,
Sasa ile anapokea simu, nilitumia namba yasimu nyingine ambayo hakuwa nayo, ile ya kwanza ilivunjika kioo pale Polisi na ni Iphone na ya kazini kwangu!
Kusema kweli nilipishwa hiyo sh 700000
Ok sasa wakati anapokea ile simu kumbe kulikuwa na mjadara unaendelea pale yeye na mke wangu,
Nilimsikia mke wangu kwa sauti kubwa ile ya kupandisha hasa, akisema
MIMI NIMESHASEMA ILE NYUMBA NI YA KWANGU, YEYE AENDE ZAKE HUKO,.
Baadaye akanyamaza nadhani mdogo wake alimwambia ni mimi nipo kwenye simu,
Nikamuuliza mpaka namsikia huyo mtu anaropoka hivyo.
Yule dada akanyamaza, na mimi si kuendelea kumuuliza, nikampa maagizo ya kesho tu
Sasa ona kweli huyo mtu ni wa kumpa senti tano yangu.?
Kesho yake kwenye kikao yule mzee na wadogo zangu watatu wa kiume na dada zake 2 na majirani 5 na mjumbe, baada ya maelezo yangu marefu kusema kweli kila mtu alishika mdomo,
Lakini wale wadogo zangu watatu hawakuvumilia, walinyanyuka kwa hasira na kumkimbilia yule mwanamke na kutaka kumpiga watu wakaingilia pale na mimi kwa hasira niwaambia waache yule ni mke wangu,
Wakanielewa wakaacha lakini walilia sana,
Wakatoka nje huku wanalia na kusema, hatukujua kama kaka yetu unasumbuka hivi na huyu mwanamke,
Kaka ambaye umetusomesha umetutunza wote
Mbona mama...... ( bi mkubwa) hakuwa hivi, I I ingekuwa ni huyu kweli sisi tungefika hapa?
Mmoja tena akakurupuka kwenda kutaka kumpiga nikamkatalia, ni kikao kikaishia hapo,
Wakati namsindikiza yule baba aliniambia neno moja tu, KUWA MWANAUME!!!