Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Jamani nipo safarini nje ni wiki ya tatu sasa huyu mtu nimeambiwa amerudi ,nisaidieni nifanyeje, mimi narudi wiki ijayo.amesikia nimesafiri na mtoto alibaki pale nyumbani ,katumia mwanya huo kurudi
Piga simu kwa mtoto wako mwambie amfikishie ujumbe aondoke kabla hapajapambazuka lasivyo mtagawana majengo ya serikali

Kingsmann
 
Kwamba aliondoka nyumba uliyomjengea alafu amerudi tena au...??? Nyumba hiyo si umfukuzeee????
ndio nataka ushauri wa namna ya kumfukuza nikirudi, sipendi mambo ya polisi naomba wenye ujuzi na mambo ya polisi mnisidie , unamfukuzaje mtu kama huyu ambaye hana hata aibu na mtoto nilimkatia ticket aende kwa bibi yake akamkataza na tiketi akauza
 
Kinyago umechonga mwenyewe saivi kinakutisha! Inamaana hauna maamuzi kabisa! Si na nyumba ulisema unauza na umerudi kwa bi mkubwa sasa tena mchepu karudi wapi?
kinatisha haswa, naomba ushauri namna ya kumwondoa nikirudi, amekaa huko huu ni mwezi wa nane na nusu na sijawahi kuwa na mawasiliano naye
 
jamani msikae kimya naomba ushaur kwa wajuzi wa mambo haya, najuta kama nini kumfahamu mtu huyu
 
jamani msikae kimya naomba ushaur kwa wajuzi wa mambo haya, najuta kama nini kumfahamu mtu huyu
Kwani wakati Unamjengea Jina la Hati ya nyumba uliandika ya nani??? Hati ya kiwanja je??? Huyo mwanamke unaweza mfukuza hapo kama hivi vyotr vipo kwa jina lako na hamjawahi kuishi pamoja at least kwa mwaka pia ufanye mpango ukamzunguke polisi kulee hilo tuu otherwise nyumba itauzwa hiyo mgawane au wewe utaambiwa Umuache hapo aishi na mwanao na Kingine kama Umeoa huyo mwanamke hana chake kabisa hapo ila Tu ishu ni Kwa mkeo vitaumana.
So jiandae kupigania mali zako lakini kwa mkeo hizi habari kufika ni lazima.
 
Habari zishafika na watoto wakubwa wanajua wanaishi na baba km mtwari tu sasa hata thamani ikashuka
 
Suluhu ya wake wawili ishatolewa na dini...

Rasimisha na ijulikane umeoa wawili..si unaona huwezi kuwa na mmoja?.
Kuwa FAIR kwa wote wawili...
Wape mapenzi sawa na mahitaji sawa...

chanzo cha migogoro ya mitala mara zote huwa ni UNFAIR TREATMENT...unataka huyu awe hivi yule vile..

Kama huwezi ishi na wawili FAIRLY komaa na huo uchi mmoja na yale yoote anayokufanyia hadi siku unaingia kaburini.,

vinginevyo jiandae kwa story kama ya huyu Baba hapa

Mwitore kosa lako ni kutomrasimisha Bi Mdogo ili atulie
 
Sijawahi kusikia mtu anateswa na mchepuko
Anateseka kwa sababu huyu sio mchepuko huyu ni mke wake wa pili
Watu mko pamoja 20 yrs+ na mna watoto ni ndoa hiyo

tofauti na mke mkubwa cheti tu

wakati angelirasimisha hili
Familia na watoto wakajuana kungekua na utulivu sana kila mke mji wake..
Baba be strong uset mwelekeo unaoutaka kwa familia yako kwa wake zako..sisitiza hutaki bifu na usipendelee...ukilemaa ndo kama hivi
 
Trust me wewe baba,Mungu amejibu maombi ya mkeo amini usiamini alivyojua unamcheat na umezaa huko nje kama nimwombaji alimlilia Mungu mno nafikiri hukuwahi tu kujua ni jinsi gani aliumia.

kwahiyo hizi mambo zote zilivyotokea kwanza ulikua umelogwa ndo ukweli mwenyewe hili halina mjadala ndo maana mfanyakazi mwenzio alikushangaa unavyopelekwa, unafikiri yeye hakuwa na mchepuko?

Jingine jiulize hadi wadogo zako wanamwona huyo mchepuko kimeo ila wewe umekomaa tu,japo hupendi aitwe mchepuko lakini ukweli ni mchepuko tu.

Mungu hua hawahi wala hachelewi ndo umepata malipo ya machozi ya mkeo aliyomlilia Mungu miaka mingi pengine hata aliweza kufunga ili mwuunganiko wenu usambaratike.

kwakua Mungu anazo njia nyingi kama vile farao alivyokua mbishi kuwaachia wana wa Israel alitumia njia na matukio mengi sana hadi akasurrender.

Ndivyo imekua kwako,maumivu ya usaliti umeyaonja tena na zaidi chozi la mwanamke mwaminifu haliendi bure hasa akiwa na Mungu,japo mmejaribu kujihami kwa maneno kuonyesha Kua hata mkeo yaweza Kua amefanya madudu.

Kuhusu ujio wa yule mchepuko nafikiri mpango wa kupauza uendelee aidha wawemo ama la! wewe tafuta mteja lakini tokea mwezi Feb unatafuta mteja kama vipi gawa kiwanja anza kuuza ambako hakuna nyumba,then uje umalizie kwenye nyumba.

Ni kama hali imekua ngumu kwa watu kununua eneo lote,akienda mahakamani ndo itaamua umlipe kiasi gani.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Nimekupata
 
Ha ha ha ha balaaa. Hongera sana ndugu yangu. Pongezi za dhati sana kwako
 
Shida kubwa ya wanaume ni kuishi kwa kutaka kuficha ficha mambo...
Mtu unamletea mke mdogo ulimuandaa kisaikolojia kwamba utamuolea mke wa pili?.
Mapenzi una maintain ama umehamishia nyumba ndogo?

kweli Mungu hachelewi

Kaka Mwitore kaa tulia jiulize kwa nini ulihitaji/unahitaji wanawake wawili?jiulize sana
WHY?
Js because u can?
Wewe ni mwanaume una hitaji hilo?
Mkeo mkubwa hakukutosheleza?
Unawapenda wote wawili?
Ulipenda watoto wengi?

pata sababu

Kama ni genuine need ambayo Mungu kaweka moyoni mwako waeleze wote wawili..
Rasimisha...jamii ikutambue hivyo na familia nzima...
Wape uhakika wa mapenzi yako kwao...

Short of that...endelea kuomboleza
Ulitegemea mke mdogo aishi kificho miaka yote bila ndoa rasmi?

Polygamy is not for the faint hearted...
Its double trouble but on the positive side its double blessings na faraja na attention na kila kitu

issue ni mwanaume umejipanga kufurahia na kukabiliana nayo ama mnaingiaga kichwa kichwa kama huyu mtoa mada?. Hehe
 
Unamshauri aruke mkojo akanyage nini?

aache watoto seriously??kosa lao ni nini?.
kutafuta mtu mpya sio suluhu
Arekebishe makosa aliyofanya kwa hawa wawili

hakuna lisilozungumzika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…