Trust me wewe baba,Mungu amejibu maombi ya mkeo amini usiamini alivyojua unamcheat na umezaa huko nje kama nimwombaji alimlilia Mungu mno nafikiri hukuwahi tu kujua ni jinsi gani aliumia.
kwahiyo hizi mambo zote zilivyotokea kwanza ulikua umelogwa ndo ukweli mwenyewe hili halina mjadala ndo maana mfanyakazi mwenzio alikushangaa unavyopelekwa, unafikiri yeye hakuwa na mchepuko?
Jingine jiulize hadi wadogo zako wanamwona huyo mchepuko kimeo ila wewe umekomaa tu,japo hupendi aitwe mchepuko lakini ukweli ni mchepuko tu.
Mungu hua hawahi wala hachelewi ndo umepata malipo ya machozi ya mkeo aliyomlilia Mungu miaka mingi pengine hata aliweza kufunga ili mwuunganiko wenu usambaratike.
kwakua Mungu anazo njia nyingi kama vile farao alivyokua mbishi kuwaachia wana wa Israel alitumia njia na matukio mengi sana hadi akasurrender.
Ndivyo imekua kwako,maumivu ya usaliti umeyaonja tena na zaidi chozi la mwanamke mwaminifu haliendi bure hasa akiwa na Mungu,japo mmejaribu kujihami kwa maneno kuonyesha Kua hata mkeo yaweza Kua amefanya madudu.
Kuhusu ujio wa yule mchepuko nafikiri mpango wa kupauza uendelee aidha wawemo ama la! wewe tafuta mteja lakini tokea mwezi Feb unatafuta mteja kama vipi gawa kiwanja anza kuuza ambako hakuna nyumba,then uje umalizie kwenye nyumba.
Ni kama hali imekua ngumu kwa watu kununua eneo lote,akienda mahakamani ndo itaamua umlipe kiasi gani.
Sent from my SM-G9250 using
JamiiForums mobile app