Mwitore, Mwitore,Mwitore. Nimekuita mara tatu! Mwache mwanamke huyo mahakamani kwa kufuata sheria zote. Pili, nyumba mwachie iwe yake na wanae lkn kabla ya kumkabidhi nyumba akugawie sehemu ya eneo lilobaki ingawa limeandikwa kwa jina la watoto,uza eneo hilo kawanunulie sehemu nyingine watoto mbali na hapo, baki na hati za eneo jipya ,utawakabidhi watoto baadae. Iwapo atakata acha kila kitu nenda zako na talaka mkononi. Mwitore, mwanamke huyu atakuua. Ama kwa kumtumia mchepuko au kwa magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza. Huyu ni bad news kwa sasa. Bi mkubwa na wanae wanakupenda na kukuhitaji. Usiwe selfish ukawapa majonzi ya ujane na uyatima! Rudi kwa mkeo na wanao na wala usigeuke nyuma tena. Utakuwa umejiepusha na mengi. Umekuwa mwema sana pande zote mbili, baba na mume bora kabisa kuwahi kutokea, muungwana, msomi, mwenye upendo, baba ambaye kila mtoto anatamani awe baba yake. Mwitore rudi kwa bi mkubwa kaa naye angalau kwa miezi mitatu bila kumfikiria huyu chizi uone ulichokikosa kwa kutokuwepo kwako! Rudi nyumbani Mwitore kumenoga