Sasa baada ya kupokea lile fungu la kwanza
30m, mimi haraka sana nikaenda kupunguza madeni yangu, hata hivyo Hays kwisha,
Na yeye nikamwita kwamba tukae chini ili ile 15m yake tuipangie matumizi ya kwanza kabisa,
Ushauri wangu ilikuwa tununue kiwanja kwanza,
Sehemu ambayo sio ghari sana, Hapo sasa ndio kimbembe kilipoanza,
Ila kufupisha story nilimwambia basi wewe unataka tuanze na nini? Akanijibu hiyo pesa anataka afanyie biashara wakati ujenzi unaendelea, nikamwambia biashara mbona tumefanya na tunasnguka, hata hivvyo sio mbaya wewe kutaka kufanya biashara lakini ni bora tuwe na kiwanja kwanza.
Kusema kweli zogo lilikuwa kubwa ananipayukia na mimi natumia ubaba wangu sasa kulazimisha, ndio alipoamka kwenye kiti(tulikuwa tumekaa nje na watoto wanacheza hapo nje).
Alichoniambiakwa sauti kuu na kali ni kwamba
TOKA HAPA NA VISENTI VYAKO UNAVYONIPAGA,
Du ! Leo naambiwa visenti, yaani huyu mwanamke nimekopa pesa, nimempeleka ufundi cherehani, nimemfungulia saloon , grocer, mghahawa, dala dala, mtaji wa kuku wa kisasa.
Anaanguka namyanyua, anakopa vicoba anashindwa kumaliza nammalzia,
Nalipa watoto karo kwa mwaka jaribia Mil 6 na bado watoto ndio kwanza wanasafari, kwa nini ananivunjia heshima namna hii?
Kusema kweli sikujua kama niliokota jiwe au mti au ufagio, nimpige nao akawahi kukimbia, na mimi nikaanza kumfukuza, kama sijamrushia kila kitu ambacho mpaka leo sikijui, nikaanguka chini, yeye akaendelea sijui wapi , kusema kweli sikumwona,
Kuangalia nyuma naona watoto, kumbe na wenyewe wakawa wameshika mawe wanataka kunipigia nayo, nikaamka ili niwafukuze nikaenda chini tena , sasa hapo ndio nikaanza kusikia maumivu, na watoto wale kule wamesimama, sasa na wenyewe wanapaza sauti,
KWA NINI UNAMPIGA MAMA YETU SI UENDE KWENU!!!!!
Nitaendelea