Naomba ushauri: Mke wangu aliondoka na mtoto sifahamu anapoishi sasa, hataki kumleta mtoto nimuone

Ndiyo mkuu maana ni copy yangu kabisa hata ukimwona kwa picha. Shida ipo kwa mwanamke tu
Unaweza kukuta we unamfananisha ila wala hamfanani,

Ila kwa hayo maelezo kuna uwezekano mtoto huyo ana baba mwingine na huenda huyo ndio baba halisi,

Halafu huyo mtoto inabidi mumfanyie uchunguzi wa kina, yani toka 2020 mpaka 2021 ameshalazwa mara 3?? Hili inabidi mjadiliane ili kuhakikisha afya ya mtoto inakaa sawa, na hii ni muhimu zaidi ya hayo mahusiano yenu,
 
Mtoto anamfanya biashara nahisi kuna mtu mwingine pia anahudumia huyo mtoto,pole sana mkuu, DNA ila jiandae kisaikolojia inawezekana pia mtoto si wako,huko kusema ni copy yako ni kutaka kujiaminisha tu mkuu kiukweli hata wewe una doubt kama ni wako,kuondoa ukungu wa wasiwasi wanasayansi wapo lol pima tu mkuu huna jinsi.
 
Binafsi nahisi huyo mtoto sio wako kwa vinasaba kabisa!
 
Fanya uchunguzi wa kimya kimya utafahamu alipo mtoto
 
Huyo mwanamke ni mjinga sana, sasa mtoto anahusika vipi katika kuachana kwenu!! Hawa ndio kesho na keshokutwa unamkuta nae anatukana wanaume kutelekeza watoto kumbe ulikuwa upumbavu wake.

Umehusisha ngazi ya familia ktk hilo? Ikishindikana nenda kisheria ila usifikirie kabisa kumsusia mtoto, hana hatia jamani na hahusiki kwenye hizo drama za mama yake.
 
Nmehusisha familia zte ila yake haijatoa ushirikiano, wanajua kabisa binti yao anachokifanya maana wao mtt anawatembelea ila siyo kunitembelea mimi. Kufanya hizo juhudi zote bila mafanikio ndo kumenifanya nitake kuchagua aidha kumwachia mtoto kabisa au kwenda ngazi za kisheria.
 
Wapotezee
 
Pole sana kwa changamoto kama una uhakika mtoto ni wako fuata sheria ni haki yako mtoto kutambua kuwa wewe ni Baba yake.
 
Chukua hili mkuu
 
Ana mtu mwengine anaishi nae..
Kutunza mahusiano yake mapya anaona bora ajiweke mbali nawe pamoja usiende ukavuja penzi la mtu anae mpenda..

......... Anampenda mwanae lkn wewe mwisho wako kwake kukufanyia kitu mbaya na utajuta, usimuwaze yuko vingine sasa......

Umeona wazazi wake wana kuona boya kwa sababu wanajua kila kitu juu yenu na nakushauri....
Nenda Ustawi wa jamii nina imani utapata ufumbuzi wa maana..
 
Unajuaje pengine mtoto sio wako anakuepushia na maumivu utakayopata mbeleni,
Ushauri
Achana nae kabisa usiwahi kumuulizia habari za mtoto tenaaa, kama ni wako atakutafuta
 
Kama una hakika mtoto ni wako VUMILIA tu kipindi hiki atakuja tuu... Ni haki yako kumuona mwanao kama anakukataza sheria zipo nenda ustawi wa jamii ukaripoti
 
Yote hayo ya nini piga kimya uendelee na mishe zako mzee akikupa taarifa za mtoto kuumwa mwambie malete kwako ndio utahudumia kwanini ujichoshe na mtu asiejari.

Achana nae siku akiiona umhimu wako atakutafuta asipoona basi mtoto akikua atakutafuta.

Mimi yupo alinifanyia hivyo na kuni broke juu nilikaa kimya sikumtafuta yalivyo mshinda huko akaja mbio kuomba msamaha tulee mtoto sasa hivi nikimwambie amlete mwanangu hata usiku saa nane atamleta.
 
Shukrani mzee na nmekuelewa kwa huu ushauri wako
 
Mkuu,Mpe mimba nyingine.Or Else Get another woman and she will stop bothering you.All in All.Mimi naona huyo demu anakuona boya so we endelea nae taratibu ila mpotezee kinamna maana atakuchosha akili for no reason.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…