Naomba ushauri: Mke wangu aliondoka na mtoto sifahamu anapoishi sasa, hataki kumleta mtoto nimuone

Naomba ushauri: Mke wangu aliondoka na mtoto sifahamu anapoishi sasa, hataki kumleta mtoto nimuone

Mimi naona ushirikishe wazazi au ndugu ikishindikana uende kwenye vyombo vya sheria, akikana mtoto sio wako fuata taratibu za kujua mtoto ni wako au la

(Maana wengi wakiambiwa mtoto sio wako wanasusa mazima) pambana ujue km mtoto ni wako au siyo, ikifahamika mtoto ni wako utamdai naww upatiwe haki yako ya kukaa nae, ikiwa umefahamu mtoto sio wako mfungulie mashtaka huyo mwanamke kwa kukuaminisha wewe huyo ni mtoto wako na gharama zote ulizotumia katika malezi ya huyo mtoto utayadai
Hapa inatakiwa aanzie polisi au wapi mkuu
 
Habari za weekend wana JF

Nilioa mwaka 2016, na tukabahatika kupata mtoto 1 wa kiume mwaka 2017 ambae ana miaka 4 kwa sasa na sehemu ya makazi yetu ni hapa Mbeya. Mapema 2020 mke wangu alianza kubadilika sana baada ya yeye kupata biashara nzuri ukilinganisha na ile aliyokuwa anafanya mwanzo.

Katika mabadiliko yake, alihitaji na yeye kwenda kuishi maisha ya peke ake. Nilitafuta suluhu sana za kuweka ndoa sawa ila hakukuwa na mafanikio na hatimae mwezi wa 6 mwaka huo 2020 aliondoka na kwenda kuanzisha maisha yake pamoja na mtoto.

Wakat anaondoka hakusema anapoenda kukaa na mtoto na mpaka sasa sipajui anapokaa na mtoto japo yupo Mbeya hapa hapa. Hayuko tayari kunambia anapokaa mbali na kuhitaji kupajua kwa ajili ya kupata access ya kumuona mtoto wangu. Kila nikiomba aniletee au nifate mtoto nikae nae hata weekend analeta sababu na anaweza kukuahidi kumleta ila ikifika muda analeta sababu na hutomuona tena.

Mtoto akiumwa siambiwi mapema, ila nakuja kuambiwa anapokuwa amelazwa hospital na ndo hapo namuona mwanangu. Tangu aondoke kwangu, mtoto amelazwa hospital mara 3 na mara zote hizo nakuja kuambiwa kashalazwa, naenda kumuona na kumhudumia mpaka anaruhusiwa, akisharuhusiwa tu ndo humuoni tena. Nimeshajaribu kuongea nae juu ya umuhimu wa sisi kumpa malezi ya wazazi wote hata kama hatuishi na mtoto pamoja, kumpa mtoto nafasi ya kuwa ananiona au ananitembelea lakini hakuna matokeo chanya. Cha kusikitisha, mtoto anamruhusu kuwatembelea marafiki zake tena umbali mrefu na hata kwa ndugu zake mtoto anaenda hata kukaa baadhi ya siku ila siyo kumruhusu kuja kwangu au mm kumtembelea mtoto.

Sasa kama mwanaume mwenye hisia na moyo usio wa chuma na mwenye maumivu, nimechoka na haya maisha ya kuishi na mtoto wangu kwa kumuona kila anapolazwa hospital. Nahitaji kufanya maamuzi magumu.

Akilini mwangu kwa sasa nna mawazo mawili ambayo nahitaji mojawapo kufanyia kazi, moja ni kumsusia mtoto kabisa abaki nae milele au niende ngazi za sheria ambazo wataweza kunisaidia hili swala kwa kuzingatia sheria ya malezi ya mtoto hasa pale wazazi wanapotengana.

Naomba mawazo yenu ndugu zangu wenye uzoefu na changamoto hizi angalau nijue naamua kwenda mbele na wazo gani hapo.

Nitapitia ushauri wenu kwa ajili ya msaada.

Polee mkuu
Sasa kama unamuona mtoto anapolazwa kwa nini usiproccess kumchukua akiwa hapo hapo hospitali?

Fuata utaratibu, nenda ustawi wa jamii
 
Back
Top Bottom