Mm pia nipo hivo tangu mdogo mpaka chuo na baada ya kumaliza chuo nilipenda kukaa mwenyewe ndo naenjoy naangalia movie naandika mstari utakaogusa moyo wangu, nasoma vitabu naandika kitu ambacho ni applicable kwangu
Kama ni weekend nitanunua mahitaji ijumaa kwahyo weekend yote nitakuwa chumbani naweza nisionekane nje na km naenda choo cha nje nasubiria hamna movement za mtu kuwepo nje ndo niende
Nimepata kikazi cha kujishkiza na interact na watu ila nakuwa nataman muda uishe nikatulie chumbani kwangu na sipend kuonana staffs wenzangu muda ambao sio wa kazi nikimwona kwa mbali nitapita njia nyingine
Tatizo langu mm naogopaga watu hasa ambao sijawazoea naonaga kuliko kwenda mjini kwenye watu wengi bora niende porini na notebook nikasome summary
Naogopaga majadiliano sana maana naweza ongea kitu kwa haraka baadae nikienda kujifungia chumbani nikiwaza au nimeongea vibaya nimemkera inaniumizaga sana au nilitakiwa kusema kitu kwa usahihi ila kutokana na majibu ya haraka nikatoa jibu sio sasa baada ya hapo nitawaza sana nikiwa mwenyewe
Sasa mwenyewe sijui km ni tatizo au sio tatizo ila mm naona hiyo tabia ndo inanipa amani
Mimi sio psychiatrist au psychologist lakini kwa maelezo yako clearly ni kama dalili za Anxiety Disorders.
Kuna aina nyingi za Anxiety Disorder na mtu mmoja anaweza kuwa nazo nyingi kwa wakati mmoja.
Kiufupi hizi ni baadhi ambazo sifa zake zinaendana na maelezo yako.
1. Social Anxiety Disorder = Hii inafanya na kupelekea mtu kuwa na hofu anapokuwa kwenye mchanganyiko na makundi makubwa ya watu.
Na watu wenye hii Disorder wanaogopa sana mitazamo mibaya au tuseme negative evaluation kutoka kwa watu wengine.
Na mara nyini hupata panic Attack ambayo inatrigger hali ya fight or flight system yaani unaanza kutetemeka, kutoka jasho, mapigo ya moyo kuongezeka, na mwili kuishiwa nguvu na kuongea kwa kigugumizi au kutetemeka pia kupumua kwa tabu.
2. Agoraphobia = Hii inafanya na kupelekea mtu kuwa na uoga na hofu ya kutoka nje ya nyumba yake mwenyewe hivyo kupelekea kukaa ndani tu.
Mtu mwenye hii Disorder huhisi na kuamini maeneo aliyopo sio salama na hakuna njia ya kujikwamua.
Hii hali inajumuisha maeneo ya wazi, mikusanyiko ya watu, vituo vya usafiri, madukani au nje ya nyumba tu.
Mtu mwenye aina hii ya Disorder hukumbwa na hofu na uoga wa kudharirika na pia kukumbwa na panic attack hadharani hivyo ili kuepuka hayo hujitenga kwa kujifungia ndani kwake.
Generalized anxiety disorder = Hii hufanya na kupelekea mtu kuwa na (worry) hofu au uoga usio na chanzo, sababu wala msingi wa kueleweka kwa kila kitu kwenye mambo ya kila siku.
yaani uoga wa matukio, kazini, shuleni, barabarani, kwenda chooni, kwenda dukani, kutoka nje, kuongea, kufanya presentation, afya, vifo, familia, mahusaino, maswala ya kazi na uchumi. yaani kila kitu.
Hizi Disorders ni destroyer of opportunities and life, sababu itamfanya mtu kudevelop aina mpya kabisa ya maisha ili kuaccommodate hizo disorders.
Mostly watu wanadhani wao ni introvert kitu ambacho kinaweza kuwa kweli au kisiwe kweli.
ila kama hizi disorders haziharibu maisha yako basi hakuna tatizo.
NB: mimi sio daktari bali nimetoa mchango tu, hivyo kama mtu amesoma hii na ana sifa nilizoweka hapa basi usiweke akilini na kuamini wewe una hizo disorders bali chukulia kama opinion na perspective tu au mtazamo wa stranger from somewhere.