Naomba ushauri: Nahisi mdogo wangu ana matatizo

Naomba ushauri: Nahisi mdogo wangu ana matatizo

Status
Not open for further replies.
Naona maswali yangu hujayajibu, ila nilikuwa nataka nihitimishe , huenda mdogo wako akawa na shida inaitwa Autism spectrum disorder au usonji kwa kiswahili.

Moja ya viashiria vyake hasa kwa watu wazima ndo kama ulivyotaja hapo juu ingawa baadhi ya maswali hujajibu.
Nalifahamu hilo tatizo na sidhani
 
Naona maswali yangu hujayajibu, ila nilikuwa nataka nihitimishe , huenda mdogo wako akawa na shida inaitwa Autism spectrum disorder au usonji kwa kiswahili.

Moja ya viashiria vyake hasa kwa watu wazima ndo kama ulivyotaja hapo juu ingawa baadhi ya maswali hujajibu.
Nilikujibu labda kama hukufuatilia
 
Ndo hivyo inaweza kuwa haijamuathiri sana ila kama ana repeated routine, she doesn't care what others feel, and always wants to be alone, she is an autistic.
Nikifikiria sidhani kwasababu yeye hana aibu anaweza hata kuongea mbele za watu
 
Anyway saivi nimeamua kumwacha kwasabu ye kwake ni kawaida kabisaaa
 
Habari zenu

Nina mdogo wangu wakike umri ni early 20s, amemaliza chuo mwaka jana mpaka sasa yupo tu home

Ana tabia yakupenda sana kuandika (vitu mbalimbali kwenye notebook zake) na kusoma vitabu na articles mbalimbali pia anaangalia sana movies, kinacho nifanya niulize ni kwasababu amezidi hadi nahisi labda anatatizo sisi hatujui kwasababu kashakua mtu mzima, Zamani nilidhani labda utoto ila ndo kwanza anavo kua ndo ana improve tabia zake, muda wote anakua na ki notebook awe nnje amekaa, awe anaangalia movie etc

Ni mengi sana naweza kueleza. Nauliza kwa wenye uelewa anaweza akawa na tatizo kichwani au ni hali ya kawaida

Naongeza

Kama ni shule amesumbua sana hostel alishindwa kukaa kufika alipo fika ni shukran za foundation alio wekewa (last born)

Kasoma shule kama 6 form 1 mpaka 4. Akiichoka anajieleza vizuuuri nakuahidi anaacha utoro. Lakini wapi na amefaulu kwa mpango wa Mungu tu

Kama uhuni hana kabisaaa akitoroka anarudi home kufanya mambo yake

Sasa hizo akili mnazo sema ni zipi
Ni malezi tu ya kumlea mtoto kimama mama haiwezekan mtoto asome shule eti akiichoka tu anahamishwa. Hana talent yoyote ni ujinga tu aliojaza kichwani
 
Ndo maana nikasema hii condition ni complicated, viahshiria hutofautiana ila kuna vinavyokuwa common.

Ukimuita jina lake anarespond haraka?
Kawaida tu ... Akiskia anaitika, enheee hapendi kuongea kwa sauti kubwa(kufoka) kwahiyo ukiwa mbal ukiita Dddd anaweza piga simu au atatoka kimya kimya
 
Mm pia nipo hivo tangu mdogo mpaka chuo na baada ya kumaliza chuo nilipenda kukaa mwenyewe ndo naenjoy naangalia movie naandika mstari utakaogusa moyo wangu, nasoma vitabu naandika kitu ambacho ni applicable kwangu
Kama ni weekend nitanunua mahitaji ijumaa kwahyo weekend yote nitakuwa chumbani naweza nisionekane nje na km naenda choo cha nje nasubiria hamna movement za mtu kuwepo nje ndo niende

Nimepata kikazi cha kujishkiza na interact na watu ila nakuwa nataman muda uishe nikatulie chumbani kwangu na sipend kuonana staffs wenzangu muda ambao sio wa kazi nikimwona kwa mbali nitapita njia nyingine

Tatizo langu mm naogopaga watu hasa ambao sijawazoea naonaga kuliko kwenda mjini kwenye watu wengi bora niende porini na notebook nikasome summary

Naogopaga majadiliano sana maana naweza ongea kitu kwa haraka baadae nikienda kujifungia chumbani nikiwaza au nimeongea vibaya nimemkera inaniumizaga sana au nilitakiwa kusema kitu kwa usahihi ila kutokana na majibu ya haraka nikatoa jibu sio sasa baada ya hapo nitawaza sana nikiwa mwenyewe

Sasa mwenyewe sijui km ni tatizo au sio tatizo ila mm naona hiyo tabia ndo inanipa amani
Mimi sio psychiatrist au psychologist lakini kwa maelezo yako clearly ni kama dalili za Anxiety Disorders.
Kuna aina nyingi za Anxiety Disorder na mtu mmoja anaweza kuwa nazo nyingi kwa wakati mmoja.

Kiufupi hizi ni baadhi ambazo sifa zake zinaendana na maelezo yako.
1. Social Anxiety Disorder = Hii inafanya na kupelekea mtu kuwa na hofu anapokuwa kwenye mchanganyiko na makundi makubwa ya watu.
Na watu wenye hii Disorder wanaogopa sana mitazamo mibaya au tuseme negative evaluation kutoka kwa watu wengine.
Na mara nyini hupata panic Attack ambayo inatrigger hali ya fight or flight system yaani unaanza kutetemeka, kutoka jasho, mapigo ya moyo kuongezeka, na mwili kuishiwa nguvu na kuongea kwa kigugumizi au kutetemeka pia kupumua kwa tabu.

2. Agoraphobia = Hii inafanya na kupelekea mtu kuwa na uoga na hofu ya kutoka nje ya nyumba yake mwenyewe hivyo kupelekea kukaa ndani tu.
Mtu mwenye hii Disorder huhisi na kuamini maeneo aliyopo sio salama na hakuna njia ya kujikwamua.
Hii hali inajumuisha maeneo ya wazi, mikusanyiko ya watu, vituo vya usafiri, madukani au nje ya nyumba tu.
Mtu mwenye aina hii ya Disorder hukumbwa na hofu na uoga wa kudharirika na pia kukumbwa na panic attack hadharani hivyo ili kuepuka hayo hujitenga kwa kujifungia ndani kwake.

Generalized anxiety disorder = Hii hufanya na kupelekea mtu kuwa na (worry) hofu au uoga usio na chanzo, sababu wala msingi wa kueleweka kwa kila kitu kwenye mambo ya kila siku.
yaani uoga wa matukio, kazini, shuleni, barabarani, kwenda chooni, kwenda dukani, kutoka nje, kuongea, kufanya presentation, afya, vifo, familia, mahusaino, maswala ya kazi na uchumi. yaani kila kitu.

Hizi Disorders ni destroyer of opportunities and life, sababu itamfanya mtu kudevelop aina mpya kabisa ya maisha ili kuaccommodate hizo disorders.
Mostly watu wanadhani wao ni introvert kitu ambacho kinaweza kuwa kweli au kisiwe kweli.
ila kama hizi disorders haziharibu maisha yako basi hakuna tatizo.

NB: mimi sio daktari bali nimetoa mchango tu, hivyo kama mtu amesoma hii na ana sifa nilizoweka hapa basi usiweke akilini na kuamini wewe una hizo disorders bali chukulia kama opinion na perspective tu au mtazamo wa stranger from somewhere.
 
Mm pia nipo hivo tangu mdogo mpaka chuo na baada ya kumaliza chuo nilipenda kukaa mwenyewe ndo naenjoy naangalia movie naandika mstari utakaogusa moyo wangu, nasoma vitabu naandika kitu ambacho ni applicable kwangu
Kama ni weekend nitanunua mahitaji ijumaa kwahyo weekend yote nitakuwa chumbani naweza nisionekane nje na km naenda choo cha nje nasubiria hamna movement za mtu kuwepo nje ndo niende

Nimepata kikazi cha kujishkiza na interact na watu ila nakuwa nataman muda uishe nikatulie chumbani kwangu na sipend kuonana staffs wenzangu muda ambao sio wa kazi nikimwona kwa mbali nitapita njia nyingine

Tatizo langu mm naogopaga watu hasa ambao sijawazoea naonaga kuliko kwenda mjini kwenye watu wengi bora niende porini na notebook nikasome summary

Naogopaga majadiliano sana maana naweza ongea kitu kwa haraka baadae nikienda kujifungia chumbani nikiwaza au nimeongea vibaya nimemkera inaniumizaga sana au nilitakiwa kusema kitu kwa usahihi ila kutokana na majibu ya haraka nikatoa jibu sio sasa baada ya hapo nitawaza sana nikiwa mwenyewe

Sasa mwenyewe sijui km ni tatizo au sio tatizo ila mm naona hiyo tabia ndo inanipa amani
Upo Kama Mimi
 
Sasa kila bure kulala bure bills hana unataka aishije sasa...what really define a person ni responsibility alizonazo na namba anavyozi handle
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom