Sitarajii kuunganisha kwa Uzi huu.
Nimeona mdau akiuliza namna ya kuingiza pesa kupitia mtandao. Naomba nikujibu na njia kadhaa lakini ukae ukijua kupata japo $1 kwenye mtandao sio rahisi hata kidogo Yani Kama ndio njia unayotarajia upate pesa yakula baada ya kuanza lazima ulale njaa. Kwanza itakuchukua muda mrefu kuanza na kuielewa vizuri pia unaweza kuanza na kukata tamaa baada ya kutoambulia kitu kwa muda mrefu. Uvumilivu na consistent nimuhimu Sana.
1. Affiliate marketing , hapa utapromote huduma ya kampuni fulani halafu wao watakulipa mrabaha. Yapo makampuni mengi yenye hiyo huduma nje na ndani ya Tanzania. Jiulize unaweza kupromote bidhaa za Aina gani mtandaoni au huduma. Commission kwa kampuni nyingi Ni kuanzia 5%-40%
2. Content creator
a) YouTuber fungua channel ya YouTube post content upate subscribe na saa 4000. ukidhi hivyo vigezo utaomba kujiunga na matangazo ya AdSense , baada ya hapo utatakiwa kuweka contents za kutosha za kuwavutia watazamaji ili upate hela. (Tafuta taarifa zaidi Google)
B) blogging , chapisha content Kama Google wanavyotaka ukishapata visitors wakutosha utajiunga na makampuni mbalimbali ya matangazo , au matangazo binafsi
c) Twitter , tafuta follower wakutosha twiter (X) verify account yako , jiunge na programs Yao ya matangazo wataanza kukulipa.
D) Facebook page
3. Kuwa freelancer , katika mitandao ya upwork freelancer n.k huku unajisajili then unatafuta kazi unayoiweza kulingana na zilizopostiwa. Mfano graphics design , article writing, translation. N.k
4. Direct link Promotion
Hapa unajiunga na kampuni za matangazo direct watakupa link yenye matangazo kazi yako Ni kuishare au kutafuta traffic kwaajili ya hayo matangazo kwa njia yoyote unayoijua wewe
Kampuni hizo Ni
1 .
Adsterra
2.
Monetag
Click kampuni husika kusoma zaidi. Kwa wale wenye follower wengi Twitter au x hii itakuwa rahisi kwao
5. Kuwa na idia ya App
6. Kuna online survey
7. Kindle publishing : hii Kama wewe Ni maandishi unaweza kuandika mswada mzuri then unauaplod kwenye kampuni ya Amazon then watauuza utapokea pesa. Kwa waandishi ambao hawana Majina ningumu kuuza japo copy moja.
Hizo Ni baadhi na maelezo sijaweka ya kutosha lakini utatakiwa kujifunza zaidi na zaidi. Hizi njia Ni rahisi kwa MTU ambaye tayari ana watu wakutosha kwenye mitandao ya kijamii, Kama hauna ningumu Sana na unaweza kuachia njiani Muhimu nikupambana . Pia nimuhimu kusoma Sheria za nchi yako zinasemaje katika njia husika