Wakuu.
Natamani kuingiza hela kwa upande wa internet naombeni msaada kwa wabobevu hata elfu 5 kwa siku
Toa Forex, betting
Zipo njia nyingi unazoweza kutumia ili kutengeneza kipato kupitia mtandao na baadhi ya njia hizo ni kuuza ujuzi na maarifa uliyo nayo mtandaoni
Unauzaje ujuzi wako ? Unatakiwa kwanza ujue jinsi ya kujiposition kwenye soko kupitia social media marketing
Kile kitu unachokijua ni biashara tosha ya kukuingizia pesa mtandaoni mfano inaweza kuwa wewe ni mtaalam kilimo au doctor wa mifugo
Ujuzi huo ni biashara tosha unachotakiwa kufanya ni kusimamia kipengele cha matokeo yanayopatokana baada ya walengwa wako kutumia huduma yako
Inaweza kuwa kuna mfugaji anachangamoto ya kuku wake kufa sana hivyo wewe ukawa unauza suluhisho la namna ya kudumisha Afya ya kuku na kuzuia tatizo la kuku kufa
Utaanzaje ?
1.Kwanza ni kujua soko gani unalenga (Je ni wafugaji wa kuku,je ni wafugaji wa mbwa,je ni wakulima wa mahindi ? Je ni wafanya biashara wanao safiri nje hawajui lugha ? N.k)
2.Mahitaji ya soko lako ni nini zaidi (Watu wanao sumbuka na changamoto ambayo wewe una suluhisho lake wanataka matokeo gani?)
3.Kupeleka suluhisho sokoni
Hapo sasa sulisho utakalo peleka inaweza kuwa kupitia huduma ya mafunzo kwa walengwa au kuwauzia vitendea kazi vyenye kuleta matokeo fulani ambayo hayapatikani kutokana na vitendea kazi vibovu au ukosefu wa elimu
Kipengele hiki kinahusisha marketing (kuuza huduma au bidhaa kwa walengwa wako ili uweze kuipata pesa yao)
Ntaandaa uzi maalum kwaajili ya hili jambo ambapo ntaelezea kwa undani kuhusu mbinu za kutengeneza kipato kupitia internet
Binafsi internet ndiyo inanisaidia kuendesha maisha yangu ikikosekana basi sina maisha